Ugumu wa maisha, ukosefu wa hela ni nyimbo zilizofanya vizuri kuliko wa darasa kwa watanzania

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
2b3fdd9dc3700017e50df72a6d76045d.jpg
a7546f7ae4579f9f135c823f59085f93.jpg


Ukosefu wa hela mikononi na Hali ngumu ya maisha ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri na zimedumu kwenye Charts playlist za wananchi maana kila siku wanaimba nyimbo hizo mbilli hata Nyimbo mpya ya Darasa ilipotoka ilijitahidi kukaa lakini haikuzifunika nyimbo hizi mbili.

Nilijiuliza nini sababu iliyosababisha watu kuendelea kuimba nyimbo za Halí ngumu ya Maisha na upotevu wa hela mikononi nikakumbuka Jibu la Serikali yangu kuwa wanaolalamika hivo walizoea pesa za bure.

Nikajiuliza kweli maana hizi nyimbo hata viongozi wa Dini wanaziimba manake nao kumbe walikuwa miongoni mwa wanafaidika na hizo lakini nikaja kugundua sababu mbalimbali zinazosababisha watanzania kuzidi kuimba nyimbo hizi mbili licha ya WCB kutoa nyimbo nzuri na kufanya show za nguvu 2016.

Kumbe licha ya Serikali ya kuongeza Mapato yake lakini deni la taifa linaloongezeka kila siku ndio mwiba mkubwa unaosababisha mana kwa mujibu ripoti ya benki kuu zaidi ya asilimia 70 ni deni la nje hivo kodi yetu inayoelekezwa kulipwa huko hairudi tena kwenye mzunguko wa ndani ndio maana hela adimu.

Pia kwa mujibu wa ripoti benki kuu kupungua kwa misaada ya nje hasa kutoka Ulaya kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukataa kusaini mikataba mibovu pesa ambazo zingeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na kuzalisha ajira imeshindikana so inabidi serikali itumie mapato yake na mikopo ya ndani kuiendeleza.

Lakini naamini nyimbo hizi mbili zitaanza kupoteza umaarufu kwa wananchi japo itachukua muda kidogo endapo miradi hii itaanza kufanya kazi mfano Ujenzi wa reli ya kati (Standard gauge), bomba la mafuta Uganda na upanuzi bandari ya Tanga, Ujenzi wa Processing Zone ya Kurasini mhimili wa biashara kati ya China na Afrika

[HASHTAG]#kijanamzalendo[/HASHTAG] [HASHTAG]#ilovetz[/HASHTAG] [HASHTAG]#maoniyangu[/HASHTAG] [HASHTAG]#Sangujoseph[/HASHTAG]
 
Wimbo wa ugumu wa maisha wachache sana hawajauimba
Akiwemo mzee mwenyewe. Maana yeye chakula, nguo, huduma zote mpaka sabuni ya kuogea tunamnunuliakwa kodi zetu sie mashetani. Haki ya nani hakuna raha kama hiyo, ndio maana sie tukikosa anasema tulizoea dili. Sasa sijui mie muuza kahawa na kashata nilikuwa na dili gani! Labda kupunguza sukari kwenye kashata?
 
Mtasema mengi sana lakini msoto utabaki pale pale, maana kwa akili za waliopo huko juu unaona kabisa hawana uwezo wa kulitoa taifa kwenye hali ngumu tuliyo nayo. Huyo mkubwa wao ukimsikiliza kila siku anaongea pumba tupu.
 
Back
Top Bottom