Ugonjwa wa mafindofindo

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,942
3,606
96949ae96beeb2882464b4ca504dece5.jpg
c7fd663157d2a2330ca5abd8808e2330.jpg
72d05254ea7414b48383c29105266e2c.jpg

UGONJWA WA MAFINDOFINDO

Kumekuwa na uelewa mdogo wa suala la vidonda vya koo maarufu kama mafindofindo katika jamii zetu. Watu wengi wamekuwa wakiamini uognjwa huu unasababishwa na utumiaji wa vitu vya baridi kama vile ice cream na barafu.

Dhana hii potofu imesababisha wazazi wengi kuwapiga marufuku watoto wao kutumia wakidhani ndio chanzo kikuu. Leo nitaelezea ugonjwa huo wa mafindo findo ama kwa kitaalamu tonsillitis.

Mafindofindo ni mjibizo wa tezi iitwayo tonsil, ambayo husaidiana na tezi nyingine katika mwili kupambana na vimelea mbalimbali vya magonjwa kwa kutengezea askari mwili. Tezi hizi ziko mbili na zinapatikana pande zote mbili mbele na nyuma ya koo. Zina rangi ya pinki na mara zinapovimba baada ya maambukizi hubadilika na kuwa nyekundu.

Mafindofindo ni ugonjwa ambao huambukizwa kwa njia za hewa, ambapo vimelea vya magonjwa kama vile bakteria na virusi huenezwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia mbalimbali.

Moja wapo ni kupiga chafya, kukohoa, kugusa zana zenye vimelea na kughusisha midomoni au masikioni, ugonjwa huu huwapata watoto zaidi ingawa huweza huwaathiri pia na watu wa rika nyingine.
Dalili kuu za ugonjwa huu ni vidonda kooni, mara nyingi mgonjwa hulalamika kuwa na vidonda kooni ambavyo huambatana na maumivu makali wakati wa kumeza chakula.

Dalili nyingine zinazoambatana na vidonda kooni ni uvimbe wa tezi unaodhihirika mbele ya shingo, homa kali, kichwa kuuma, mafua, harfu mbaya kinywani, kufifia au kupotea kwa sauti na mwili kuchoka. Vidonda kooni ambavyo huambatana na dalili nyingine kama vile mafua, kupiga chafya na kikohozi mara nyingi husababishwa na virusi.

Kwa sababu hiyo, matibabu ya dawa katika hali hiyo si ya lazima kwa sababu mwili unaweza kupambana katika kuondoa vijidudu hivyo. Endapo vidonda vya koo havitaambatana na dalili yoyote kama nilizozitaja, moja kwa moja kinachodhaniwa ni maambukizi ya bakteria.

Njia mbadala za kutibu ugonjwa huu ni pamoja na kupumzika, kusukurua kinywa kwa kutumia maji vuguvugu yenye chumvi na kunywa maji mengi.
Dawa za maumivu na homa hutolewa na wakati mwingine sawa za vijaviuasumu (antibiotic) huweza kutumika iwapo maambukizi ni ya bakteria.

Endapo ugonjwa hautapatiwa tiba ya haraka madhara mbalimbali huweza kujitokeza kama vile homa ya rheumatic, magonjwa ya sikio, figo, tezi nyingine pia katika mwili zaweza kuathiriwa pia kwa kutengeneza usaha.
Mwendelezo wa maambukizi ya tezi hizi za koo, huweza kusababisha mafindofindo sugu. Hii ni kutokana na kuendelea kuzaliana kwa bakteria ambao hutengeneza vifuko vidogo vidogo kwenye tezi hizo.

Ndani ya vifuko hivi hutengenezwa mawe madogo yaliyo na mchanganyiko wa salfa ambayo huleta harufu mbaya ya kinywa. Mara nyingi mafindofindo sugu hutibiwa kwa njia ya upasuaji. Hii huamriwa na daktari endapo maambukizi hayo yatakuwa yameendelea kumsumbua mgonjwa kwa kipindi kirefu. Upasuaji utamsaidia mgonjwa kuepuka madhara kwenye mifumo mingine.

Ili kuepuka kupata maambukizi katika mfumo wa hewa ni vyema kuzingatia usafi wa mwili na mikono.
Epuka sehemu ambazo utakaa muda mrefu ambazo zina vihatarishi kama vile msongamano wa watu na vumbi.
kwa maswali muone daktari.
 
Asante... Nimeeamka tu leo najikuta nina homa na nikimeza kitu koo linauma balaa

Mti wenye matunda.
 
Shukran kwa elimu kama mimi nimeshafikia hatua ya huyo dada hapo chini,kwa mwenye kujua japo nipate tiba mbadala hayo mavimbe yatoke maana op. ya koo naona kama nitaunganisha jumla nalifikiria dona na kibua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom