Konnie, kuna mdogo wangu miaka ya nyuma alikuwa anasoma Visiga Sec. Aliwahi kutuhadithia kuwa mwanafunzi mwenzao asiombe atembelewe na ndugu zake,na kati ya hao,awepo wa kike...
Ilikuwa balaa.. Huyo bidada atazongwazongwa,atasindikizwa,hata wageni wengine watasahaulika..!
Nakumbuka kumuuliza kama hakuna mwanamke hata mmoja shuleni kwao.. Alisema wako wanne tu,nao ni masista,halafu ni VIKONGWE,vilivyokongowea mno!