Ugonjwa wa Appendix. Dalili zake ni zipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Appendix. Dalili zake ni zipi?

Discussion in 'JF Doctor' started by Mokoyo, Jun 7, 2012.

 1. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wandugu naomba kufahamu dalili za ugonjwa wa appendex. Pia naomba kufahamu matibabu yake. Vilevile nikifahamu visababishi vya ugonjwa huu itakuwa bora zaidi

  Nawasilisha
   
 2. li sheng

  li sheng Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hahaaa naona sasa unataka kuwa daktari wa "appendicitis" sio appendex

  Ningeomba nikujibu kwa mtiririko ulio mwepesi zaidi

  Appendicitis ni maradhi ya Kidole utumbo (appendix) ambayo hutokana na kuathirika aidha kwa kuchubuka au kushambuliwa na vijidudu kutokana na kukorofishika kwa utendaji kazi wake wa kushafirisha mucous kwenda kwenye sehemu ya utumbo mkubwa kutokana na sababu mbali mbali kama ifuatavyo:

  Sababu:
  kukwama kwa kinyesi, kujikunja kwa kidole utumbo, kuvamiwa na vijidudu vinavyoishi ndani ya utumbo hususan mkubwa ambao huwa unasafirisha kinyesi, saratani ya uchango, kilema cha kidole utumbo, hata vyakula hususan vyenye uwanga mwingi vikiingia hushindwa kutoka na hukwama ndani ya kidole tumbo.

  Dalili:
  Dalili kuu ni maumivu ya tumbo kwenye kichembe au kwenye kitovu (mara nyingi), ambapo humea kwa nguvu kila mda ukienda na kuhamia upande wa kulia baina ya mfupa wa gungu na kitovu (Mc Burneys point) na maumivu huwa makali sana ambayo sasa huambatana na kichefuchefu na kutapika tumbo kuwa gumu ukimgusa mgonjwa anaruka na kushindwa kutembea kwa maumivu makali na homa .

  Utibabu (Hutafautiana kidogo baina ya chronic na acute lakini cha msingi ni) :
  1.
  Dawa za kuua vidudu (antibiotics) sikutaji zipi
  2. Dawa za kupunguza maumivu (analgesics)
  3. Upasuaji (APPENDICECTOMY)

  Madhara: Kama ukichelewa kutibiwa appendix inaweza kukosa damu kutokana na kubanwa, kuoza (gangrene) kupasuka, na kueneza uchafu ndani ya tumbo (peritonitis ) ambayo hatari sana.

  Ushauri: kama unadalili za ugonjwa huu ni bora kumuona Daktari mapema kwani kwenye jamii takriban ya 70% huugua ugonjwa huu ambao ukiwahi kutibiwa mapema hauna tatizo kubwa kama ukichelewa.

  Karibu tena.
   
 3. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  chakula chenye michanga pia huleta apendix.
   
 4. salito

  salito JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  mkuu shukran kwa kunielimisha.
   
 5. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu nashukuru sana kwa maelezo haya ya kujitosheleza. May God bless you. Amen

   
 6. li sheng

  li sheng Member

  #6
  Jun 9, 2012
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wakuu nashkuru kwa kuwa mumeridhika
  Asanteni wote
   
 7. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tunashukru wa kuu wa ufafanuzi maana hata mimi nilikuwa nilikuwa natatizo
   
 8. BABA TUPAC

  BABA TUPAC JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2016
  Joined: Sep 30, 2015
  Messages: 899
  Likes Received: 1,257
  Trophy Points: 180
  Ulitumia dawa gani kupona mkuu?
   
 9. f

  feith New Member

  #9
  Dec 13, 2016
  Joined: Sep 19, 2016
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Maumivu ya tumbo upande wa kushoto hiyo ni dalili ya appendicitis
   
 10. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2016
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  ni upande wa kulia mkuu na si kushoto
   
 11. Malampaka1

  Malampaka1 Member

  #11
  Dec 28, 2016
  Joined: Dec 11, 2014
  Messages: 20
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  pole sana mi nilipona hili tatizo Kwa oparation
   
 12. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2017
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Tujifunze
   
 13. r

  rubii JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2017
  Joined: Feb 22, 2015
  Messages: 11,320
  Likes Received: 9,931
  Trophy Points: 280
  Ulipona mkuu?
   
 14. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2017
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Tiba yake ni operation tu..kinyume na hapo,kila siku utakuwa mgeni wa daktari.
   
Loading...