Uganda Yatishia Kuingia DRC

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,067
Serikali ya Uganda imetishia kuwafuata hadi ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, watu wanaowashambulia raia wake katika eneo la Ziwa Albert.


(Rais Joseph Kabila)

Waziri wa masuala ya kikanda wa Uganda Philemon Mateke, ameiambia Sauti ya Amerika kwa mahojiano ya simu kwamba Uganda imefikia hatua ya kutovumilia tena kile ametaja kama uchokozi kutoka kwa watu wa DRC, wanaoingia Uganda na kuwapiga, kuwauwa na kuwajeruhi raia wake hasa katika ziwa Albert.

“Tunawaomba Wakongo, waache kutuchokoza. Tumekuwa wenye ustaarab kwa mda mrefu. Kazi yetu kama serikali ni kuwalinda raia na mali yao” amesema Waziri Mateke.

Mateke amesema Serikali ya Uganda imekuwa ikitumia mbinu za kidiplomasia kusuluhisha migogoro kati yake na DRC, ikiwemo suala la kukabiliana na waasi wa Allied Democratic Forces, ADF, lakini sasa mashambulizi kutoka DRC yamezidi na kwamba Uganda ipo tayari kujibu mashambulizi hayo kwa nguvu za kijeshi.

“Wakiendelea kutuchokoza, tutajibu. Tunachoka. Hatuna uvumilivu tena. Sehemu wanakotoka watu hawa hakuna uongozi thabithi. Kwa hivyo, hatuna watu wa kuzungumza nao kumaliza mashambulizi yao. Hata jana Jumanne wameuwa watu 12 katika eneo la Ziwa Albert,” ameendelea kusema waziri Mateke.

Juhudi za kuwapata maafisa wa DRC kujibu tuhuma hizi kwa njia ya simu hazikufaulu.

Waziri Mateke ametaja kundi la ADF kuwa kundi sumbufu lakini hatari, ambalo serikali ya Uganda ilikuwa karibu inalishinda nguvu kabla ya serikali ya DRC kuwazuia wanajeshi wa Uganda na sasa kundi hilo limegeuka tena kuwa hatari kwa DRC na majirani zake, akiongezea kwamba muda utafika, watakabiliana nao vilivyo.

Msemaji wa Jeshi la Uganda, UPDF, Brigedia Richard Karemere, ameiambia VOA kwamba wana taarifa kwamba wanao tekeleza mashambulizi dhidi ya wavuvi katika Ziwa Albert, ni maafisa wa Jeshi la Kongo kwa ushirikiano na makundi ya wapiganaji.

Keremere amesema kwamba kwa sasa wanajeshi wa Uganda wako mpakani tayari kukabiliana na kundi la ADF pamoja na kundi lolote lile linaloweza kuingia Uganda na kulezea kwamba wapo tayari kuingia DRC iwapo serikali ya Joseph Kabila itawaruhusu.

Chanzo: VOA
 
Huyo kiongozi wa kijeshi toka uganda anatakiwa kukumbuka waasi wa ADF asili yao ni Uganda na mashambulizi yote yanayofanywa na ADF yanakuwa planned nchini uganda. Sijaona haja y'a yy kupiga kelele km wanataka kwenda kuongeza nguvu Kwa kikundi chao cha ADF kilichopo Nord kivu hususani Beni waende sio kuhadaa Watu.
 
Wanatuzuga tu hapa,wote wajomba zao katika kudokoa mawe, wameona ADF wameanza kulegea wanataka support ya kuingia kuwapelekea mikate na kukaa nao ili UN wasipige kelele Karemere mbona mjomba wako yupo huko huko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…