UGANDA: Mtu mmoja ajaribu kumshambulia Askofu kwenye Madhabahu kwa gogo wakati wa misa ya Pasaka

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929


Katika hali isiyo ya kawaida, mwanaume mmoja akiwa amebeba gogo alikimbilia kuelekea katika madhabau ya kanisa la St. Paul Namirembe wakati wa misa ya Pasaka ambapo Askofu Wilberforce Kityo Luwalira alikuwa akiongoza Misa hiyo

Mwanaume huyo aliye tambulika kwa jina la Herbert Kaddu alifika Kanisani hapo akiwa kwenye gari na kuliegesha katika njia kuu ya kuingia Kanisani hapo

Alipofika alipambana na Polisi kisha kuwashinda na kuingia Kanisani hapo, kila kitu kilikuwa sawa mpaka mwishoni mwa misa ambapo mtu huyo aliibuka na gogo akiwa amelishikilia na kunaza kukimbia kuelekea madhabauni

Baadae Polisi walimshinda nguvu na kisha kumkamata na kumpeleka katika kituo cha zamani cha Polisi cha Kampala kwa mahojiano

Askofu Luwalira amesema "Nimeshuhudia nguvu za giza katika kipindi changu nilichofanya kazi kama Askofu, ila kitu chenye nguvu kabisa nimeona nguvu ya Mungu"

Sababu za Mwanaume hiyo kufanya kitendo hicho hazikufahamika mara moja
====
There was drama at St. Paul's Cathedral Namirembe during Easter prayers, after a man clad in backcloth ran towards the altar where Bishop Wilberforce Kityo Luwalira was conducting service.

A man identified as Herbert Kaddu came driving a Super Custom vehicle and parked it at the church's main entrance before jumping out.

He beat police security and gained entry into the cathedral. All was well until the end of the service when Kaddu ran to the main corridor of the church while holding a big stick towards the holy altar.

The ushers in the cathedral attempted to stop the man in vain. He was later overpowered by police and whisked off to Old-Kampala Central police station for interrogation.

Bishop Luwalira says the man looked possessed and couldn't be stopped.

"I have seen the power of darkness during my service as Bishop but the most powerful thing is that I have seen the power of God," said Luwalira.

He told his congregation not to blame security officers attached to the church since such incidents happen to even to high profile people with heavy security, adding that church doesn't have a guest list since it is a place of prayer where people are not invited.

He promised to cause a meeting with the security officers to identify the security lapses and Kaddu's motive.
 
Waafrika wanaanza kufukuza watu wanaoshabikia dini za watu, ni jambo zuri.....bado kushambulia misikiti tu.
 
yawezekana ndio sababu watumishi wengine wana mabodgadi wakutosha
 
Labda kukamilisha habari ingepatikana sababu ya kutaka kulifanya hilo huwenda alikosewa na akashindwa kuzimudu hasira zake kama binadamu japo si jambo jema.
 
Natumai mko wazima wakuu

Kwa lile jaribio la mashambulizi ya ASKOFU wa Uganda wiki uliyo pita,
Niliona Kuna njemba kama nne zilimbeba yule jamaa kama kiroba cha makinikia, nikathibitisha Ile kauli kuwa
Catholic Church ina jeshi Lake maalum lililovaa kofia ya dini

Sijuii Niko sahihi wakuu......
 
Natumai mko wazima wakuu
Kwa lile jaribio la mashambulizi ya ASKOFU wa Uganda wiki uliyo pita,
Niliona Kuna njemba kama nne zilimbeba yule jamaa kama kiroba cha makinikia, nikathibitisha Ile kauli kuwa
Catholic Church ina jeshi Lake maalum lililovaa kofia ya dini

Sijuii Niko sahihi wakuu......
Hauko sahihi [HASHTAG]#Kinjekitile70[/HASHTAG]
 
kuna wengine hawajaiina hiyo ila washukuru lile kanisa mule ndani lilijengwa kiulinzi ama kwa kujua au kutokujua ile mbao ilimzuia yule jamaa...
 
Back
Top Bottom