Ukiangalia yanayoendelea uganda kupitia mtoto wa museven ambaye ni CDF ni uwezekano wa uganda kuwa kama zimbabwe kwanini nasema hivi
Mtoto wa museven Muhoozi Kainerugaba ananafasi kubwa ya kurithi kiti cha baba yake kama Rais- imagine jamaa alivyokua na mawenge vile anakua Rais ni wazi kuna mda unawaonea huruma sana uganda sababu museven ni kama anaipigania familia yake na hajali kabisa maslai ya wananchi wote wa uganda
Marekani ni nchi ambayo ni superpower na pia ni kiranja wa dunia ana mapungufu mengi sana ila ndo kiongozi wa dunia, kuna viongozi wa nchi walitumia njia za Muhoozi Kainerugaba kudeal na marekani matokeo yake waliumiza sana wananchi wake mfano mzuri ni zimbabwe leo hii wanakimbilia south africa mbinyo wanaoupata ni mkubwa sana kutoka marekani na washirika wake
Ukiwa maskini hutakiwi kuwa na hasira nikimaanisha hakuna ulazima wa kuwajibu marekani hasa pale wanapotoa tamko lolote juu ya nchi zetu hizi za africa hata alichofanya samia juzi kuwajibu mabolozi kule moshi alikosea sababu hakukua na ulazima wa kufanya hivyo