Uganda inapaswa kuwa na siku maalumu ya kuishukuru Tanzani.

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,048
3,227
Habari hii nimeitohoa kutoka kwenye moja ya thread inayozungumzia Historia ya
"Shekilango" , ndani yake imeelezea kwa ufupi ni kwa namna gani serikali ya Tanzania iliipigania Uganda.
Watanzani wengi waligharimika maisha yao wakiwamo viongozi wetu shupavu wa kiserikali wakati huo , kwa misingi hiyo nimeona ipo haja ya Serikali ya Uganda kua na siku ya maalumu ya kusema Ahsante na tutawakumbuka daima Ndugu zetu Tanzania.


Ni hayo tu niliyoyatizamia.



MATATIZO YA UGANDA
Mara baada ya Mapambano ya Vita vya Kagera, Mwanzoni mwa mwaka 1979 Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania vilifanikiwa kumng'oa Madarakani Dikteta Amin wa Uganda na kumpachika Ndugu Yusufu Lule kama Rais wa Muda wa Taifa hilo Jirani. Lule hakudumu sana madarakani kwa kuwa mwezi Juni, 1979 naye aling'olewa madarakani kwa kutofautiana na Baraza la Ushauri la Taifa la Nchi hiyo juu ya uteuzi wa nafasi za Mawaziri, na nafasi yake kuchukuliwa na Ngudu Godfrey Binaisa.

Miezi kadhaa baada ya kuchukua madaraka kwa Binaisa katika Serikali ya Uganda bado mambo ya kuendesha nchi hiyo hayakuonekana kwenda vizuri, Changamoto za kujenga upya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita zilikuwa kubwa, huku Jeshi jipya la nchi hiyo likiwa na kashfa ya kufanya ukatili kwa wananchi na pia kushiriki kwenye uhalifu na uporaji. Ili kuimarisha mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo ilimbidi Rais Nyerere ambaye bado vikosi vya Jeshi lake vilikuwa havijaondoka Uganda, ampeleke Waziri Hussein Ramadhani Shekilango kwenda kusaidia mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo.

Mwezi Mei, 1980 ilizuka sintofahamu kubwa katika Utawala wa Uganda, Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Jeshini Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo (zamani akiitwa Chief of Staff) Ndugu David Oyite Ojok na kumteua kuwa Balozi wa Uganda Nchini Algeria, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni nidhamu mbaya ya Jeshi la nchi hiyo hasa kwenye masuala ya Ukatili kwa wananchi na Uporaji.

Uamuzi huo wa Rais Binaisa haukumfurahisha Kiongozi huyo Namba 2 wa Jeshi la Nchi hiyo, hivyo alikataa Uteuzi mpya, na wanajeshi waliokuwa Watiifu kwake wakatangaza kumuondoa Madarakani Rais Binaisa aliyekuwa akilindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Hekalu la Rais la Entebbe.

Misururu mirefu ya Magari ikaonekana katika Jiji la Kamapala, ambapo Wanajeshi watiifu kwa David Ojok walikuwa wakiyapekuwa magari yote yaliyokuwa yakitoka na kuingia ndani ya jiji hilo ili kuhakikisha hakuna silaha, huku pia wakikiteka Kituo cha Redio cha Taifa cha Nchi hiyo.

Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo.

Kung'olewa kwa Binaisa kulifanywa na Tume maalum ya Watu sita, ambayo ilikuwa ni sehemu ya Baraza la Ushauri la Taifa lililomng'oa Rais Lule, huku matendo ya Tume hiyo pamoja na Ojok kwenye wiki hiyo yakihusishwa zaidi na Rais Milton Obote aliyekuwa ughaibuni, ambaye aling'olewa Madarakani na Amin mwaka 1971. Obote alikanusha kuhusika na matendo hayo ya Ojok yaliyokuwa yakiteteresha hali ya ustawi wa nchi hiyo japo haikubadili ukweli kuwa marafiki hao lao lilikuwa moja.

katika hali ya matatizo yote hayo, Waziri Hussein Ramadhani Shekilango pamoja na Balozi Kilumanga waliamua kupanda Ndege kwenda kumpa habari za namna hali halisi ya mambo ilivyo nchini humo Rais Nyerere ambaye alikuwa kwenye Ziara ya Kiserikali Mkoani Arusha. Safari hiyo ndiyo ikawa mwisho wa maisha yao.

Ilikuwa siku ya huzuni mno kwa kumpoteza Waziri huyo damu changa, Tarehe 11 Mei, 1980, ndege ya Kijeshi iliyowachukua Shekilango, Balozi Kilumanga pamoja na Wanajeshi wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianguka katika vilima vya Jiji la Arusha na Abiria wote kupoteza Maisha, wakiacha huzuni na majonzi mazito kwa Watanzania.

Msafara wa Rais ukakatisha ziara na shughuli ya Mapokezi ya Miili ya Mashujaa wetu hao ndiyo ikawa Ratiba rasmi, huku Rais Nyerere akionyesha kwa dhati namna alivyohuzunishwa kwa kumpoteza Waziri huyo Mchapa Kazi kwa Taifa. Majonzi zaidi yakiwa kwa Wanakorogwe waliopoteza Kijana wao Msomi wa Makerere aliyejitolea kuwatumikia kwa dhati.

Shekilango alizikwa Kijijini kwao Jitengeni, Korogwe, Mkoani Tanga, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu, mpaka leo akibaki Mbunge kipenzi cha watu wa Korogwe na akisifika Serikalini kwa hatua yake ya kurudisha Madaraka Mikoani. Kwa kumuenzi kuna Shule yenye jina lake Jimboni Korogwe.

Mamlaka za Uongozi wa Jiji la Dar es salaam kwa kutambua mchango wa Shekilango kwa Taifa, ikaamua kuipa Barabara mpya iliyokuwa inajengwa wakati huo jina la Shekilango ili kumuenzi shujaa huyu.

Mola amlaze Pema Hussein Ramadhani Shekilango
 
Museveni apandishwe cheo na JWTZ kuwa general maana alipigana vita ile bega kwa bega na JWTZ
 
Be serious bana...awe general kweli????? Vitani alikua na cheo gani? Kikosi gani?

TAYARI NI MAGER GENERAL, SASA SIJUI HICHO KINGINE MTAKIITAJE AND TO YOU MY BROTHER Waonekana haujui lolote kuhusu Museven na amepigana Vita vingapi hadi sasa
 
Back
Top Bottom