Uganda Inakusudia Kuishtaki Tanzania na Kenya kwa zuio la bidhaa zake katika nchi hizo

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Nchi ya Uganda, ambayo ni mwanachama wa EAC, anakusudia kuwashtaki wanachama wenzake, Tanzania na Kenya kwenye mahakama ya East Africa, kama mazungumzo hayatazaa matunda.

Nchi ya Kenya inashutumiwa na Uganda kwa kuzuia bidhaaa zikizozalishwa Uganda kama vile sukari, maziwa na nyama; huku Tanzania ikishutumiwa kuzuia sukari iliyozalishwa Uganda kuingia nchini.

Watawala, vizuizi vya biashara ndani ya nchi wanachama, hamwoni vinaidhoofisha EAC?

Najua, sababu kubwa ni kwamba kumekuwa na malalamiko au hisia kuwa baadhi ya nchi wanachama, wazalishaji wao huagiza bidhaa nje, kisha kuziweka tu label zinazoonesha bidhaa hizo zimezalishwa katika nchi wanachama ili bidhaa hizo ziweze kupata msamaha wa kodi zinapoingia nchi wanachama.

Je, hakuna uwezekano kwa nchi wanachama, kuunda chombo kimoja cha pamoja kitakachoangalia ubira wa bidhaa, na pia kuthibitisha bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi wanachama? Bidhaa hizo zingeweza kuwekewa nembo ya ubora ya EA, na zikauzwa ndani ya nchi wanachama bila usumbufu.

Waafrika tumekuwa watu wa kulalamika sana. Mara wazungu wanatuonea, lakini hata inapokuja sisi wenyewe Waafrika kwa Waafrika, kwa nini hatuaminiani?

Serikali yetu zinapotengeneza ugumu wa wafanyabiashara wao kufanya biashara na Tanzania, tunatengeneza mazingira magumu kwa watanzania kufanya biashara kwenye mataifa yao.

Nimesikia kuwa ujenzi wa bomba la mafuta toka Uganda mpaka bandari ya Tanga, unaanza wiki ya pili ya mwezi March 2021. Bomba hili lilikuwa likigombewa pia na Kenya, lakini Uganda wakaichagua Tanzania. Sisi Tanzania kwa kuzingatia kazingira hayo ya Uganda kuamua kupitishia bomba la mafuta toka nchini kwao kuja Tanzania, na siyo kwingineko, bado kweli Tanzania ilitarajiwa kuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wa Uganda, kama taratibu zote za biashara zimefuatwa?

Kumbukeni maneno ya Kikwete, ukitaka kula, nawe ukubali kukiwa (sina uhakika kama nimenukuu kwa usahihi, neno kwa neno)

Kwa undani zaidi, rejea:

=========

Uganda to sue Kenya, TZ over exports blockade

Wednesday February 24 2021

Uganda will this week seek to find solutions to the continued blockade of its exports, failure of which, it will seek intervention of the East African Court of Justice.

Government, according to Ministry of Trade, will present its case before the East African Summit.

The summit, which involves a number of hybrid meetings, is ongoing and will climax with the Heads of States meeting.

Mr Emmanuel Mutahunga, the Ministry of Trade commissioner external trade, yesterday told Daily Monitor, government had been engaging and will continue to engage member states to solve the trade wars, with a further push expected during the during the ongoing summit.

However, Mr Mutahinga noted: “If this fails, our next route will be taking the matter to the East African Court of Justice.”

Ugandan manufacturers, especially those involved in the export market, have suffered at the hands of EAC partner states, which have continuously blocked entry of some goods without explanation.

A number of goods, key among them milk, sugar, poultry and beef products, among others have been blocked particularly from entering Kenya with claims that are not well explained.

Mr Daniel Birungi, the Uganda Manufacturers Association (UMA) executive director, said it was unfair that Uganda continues to play second fiddle, acting as a supermarket for other countries’ goods yet its products are denied entry into markets of partner states.
UMA last year gave government an ultimatum of up to last Christmas within which it had been required to address the blockades or mobilise within manufacturers for a way forward.

However, no details have been given two months after the expiry of the ultimatum.

Trade wars have cost Uganda in different sectors, especially sugar, where stockpiles have grown to nearly 150,000 tonnes after manufacturers and suppliers were closed out of some EAC member states.

Mr Birungi in the November statement which gave government an ultimatum said, it was surprising that EAC member states were finding “reasons to bar our products from entering Kenya and in some cases Tanzania.

In 2019, Tanzania blocked Uganda’s sugar from entering its market only to allow 20,000 tonnes in 2020 but that was also stopped.
Kenya continues to impose a ban on Uganda’s milk only easing the one on sugar to allow 90,000 tonnes.

However, Mr Jim Kabeho, the Uganda Sugar Manufacturers Association chairman last month told Daily Monitor they had not received permits to start shipping the sugar.

Trade decline
According to a Ministry of Finance economic performance report for the period ended November, during October, exports to East African Community region declined from $102.9m in October 2019 to $82.2m, marking a sustained decline in almost two calendar years.

During this period Uganda’s exports to East Africa suffered 20 per cent decline, representing a drop of $20.7m (shs75.5b) compared to the same period in 2019.

This was partly blamed on a hostile environment, characterised by non-trade barriers and blockades on a number of goods originating from Uganda.

Source: Daily Monitor
 
Wawashtaki tu. Maana huwezi kuwa na Washirika wanafiki, wabinafsi, wakaidi na vigeugeu!

Mara kadhaa unashangaa wafanyabiashara wanapewa vibali na kuagiza sukari kutoka Brazil na wakati majirani zetu kama hawa Uganda, Malawi, nk. Wana sukari ya kutosha tu na inayouzwa kwa bei nafuu kuliko hii ya kwetu.
 
Wawashtaki tu. Maana huwezi kuwa na Washirika wanafiki, wabinafsi, wakaidi na vigeugeu!

Mara kadhaa unashangaa wafanyabiashara wanapewa vibali na kuagiza sukari kutoka Brazil na wakati majirani zetu kama hawa Uganda, Malawi, nk. Wana sukari ya kutosha tu na inayouzwa kwa bei nafuu kuliko hii ya kwetu.
Tatizo roho zetu ni ngumu sana
 
Mnapoteza tu muda Wenu hakuna Siku ambayo Uganda ya Rais Museveni itagombana na Tanzania kwani Tanzania ni Nyumbani kutoka Moyoni kwa Rais Museveni pamoja na Familia yake nzima. Ingekuwa ni Kenya ya Kenyatta ningekubaliana nawe (nanyi) tena 100% kwakuwa najua Tanzania na Kenya zina Urafiki was Kinafiki na Uadui wa Kimkakati hasa kwa miaka hii ya hivi karibuni.
 
Mnapoteza tu muda Wenu hakuna Siku ambayo Uganda ya Rais Museveni itagombana na Tanzania kwani Tanzania ni Nyumbani kutoka Moyoni kwa Rais Museveni pamoja na Familia yake nzima. Ingekuwa ni Kenya ya Kenyatta ningekubaliana nawe (nanyi) tena 100% kwakuwa najua Tanzania na Kenya zina Urafiki was Kinafiki na Uadui wa Kimkakati hasa kwa miaka hii ya hivi karibuni.

Mbwiga ni mbwiga tu. Umesoma vizuri taarifa au umekimbilia kusema Uganda na Tanzania hazina shida??
 
kwamba waafrika tunaoneana sana hilo halina ubishi angalia sheria zetu tu utaliona hilo.
 
Hivi haya kwenye kikao cha maraisi wa EAC hawakuyazungumza? au kulikuwa na changamoto ya mawasiliano?
 
Sio kweli. Tunapendana sana. Lakini waache kutumia EAC kufanya biashara chafu. Tuwe na uhakika na wanachozalisha sio kufanya reparking ya bidhaa kutoka nje.
Mawazo ya wezi ni kuwa za kila wanayekutana naye atakuwa mwizi.
 
Back
Top Bottom