Ugali sasa ni chakula cha anasa kuliko wali

Teleshkova

Member
Joined
Feb 14, 2017
Posts
76
Reaction score
136
Kufuatia ongezeko kubwa la bei ya unga Jijini Dar es Salaam na labda sehemu zingine za nchi, sasa ni bayana kuwa ni rahisi mtu kumudu kula wali kuliko kula ugali. Kilo ya unga katika baadhi ya mitaa inauzwa hadi Sh. 2,200/= ilhali kilo ya mchele inaweza kupatikana kwa Sh. 2,000/=.

Kufuatia hali hii tujiandae kwa yafuatayo:

-ugali kuwa chakula cha sherehe, harusi na matukio mengine maalumu maana si chakula cha gharama?
-wanafunzi na wafungwa kuanza kutumia wali kama chakula kikuu na ugali kama chakula cha anasa
-nyumba kuu yaani familia kufurahia wali huku michepuko wakigeukia ugali maana si ndio chakula cha anasa?
-wataalamu wa mapishi na lishe watalazimika kubuni pilau ya ugali ili ichukue pahala pa pilau ya wali ambayo sasa si chakula aghali na special tena
-kula ugali kila siku kunaweza kupelekea kuikosa mbingu maana ni kupenda anasa za dunia.
NK

[HASHTAG]#liferealities[/HASHTAG]
 
WACHA TUKOME,WAUZA MAINDI WALIISHAAMBIWA WAUZE MAINDI KWA BEI WANAYOTAKA NA ANAELALAMIKA KWAMBA MAINDI YAMEPANDA NA YEYE AKALIME SHAMBA LA MAINDI.
 
Uku kwetu wenye ela ndo wanakula ugali tu ss masikini ndo mchele dairy mpaka tunachoka hatareee
 
Yaani huku kwetu ukila ugali watu wanakuhoji hela umepata wapi! Yaan sasa hivi kitaani kwetu ni mwendo wa wali, maandazi, na chapati....ugali tumewaachia wakulima wenyewe(wapanga bei)
 
Najaribu kupiga picha nini kitatokea kwa wanafunzi wa shule za bweni watakapotangaziwa "kutokana na kupanda kwa bei ya Sembe chakula cha kila siku kinakuwa wali,ugali inakuwa mara moja kwa wiki siku za weekend au sikukuu "
 
Mimi natabiri wataandamana hadi kwa DC. Watanzoo huwa hatueleweki. Nafikiri tunarithishana aina pekee ya akili duniani. Hahahahaaa
 
huku kwetu mchele mzuri tunapata kwa tsh 1800/= unga unauzwa kwa tsh. 2200/=
yaani ni mwendo wa kubadili mapishi ya wali tu.
Jumamosi wali wa chumvi na mafuta tu.
Jumapili wali wa vitunguu
Jumatatu wali wa njegere na karoti
Jumanne pilau.

wakulima wa mahindi endeleeni kujipangia bei.
 
Wapi huko mkuu niwe nachukua mchele kilo kadhaa na kuziuza kwetu kwa 2000 kwa kilo?
 
Chenga za mchele 1200, Kwa familia ya watoto Wanne zikinunuliwa Kilo 2400 + 500 ya mafuta wanakula Siku siku nzima na kesho yake Asubuhi wanywea Chai.

Ila sio Ugali 2200+Mboga, huu mnakula Mchana tu na Umeisha!

Na Wali mnaweza hata kula mkavu bila mboga ila Sio Ugali

Tuanze kuusahau Ugali sasa.
 
Yaani huku kwetu ukila ugali watu wanakuhoji hela umepata wapi! Yaan sasa hivi kitaani kwetu ni mwendo wa wali, maandazi, na chapati....ugali tumewaachia wakulima wenyewe(wapanga bei)
Usiwasingizie wakulima, wakulima hawapangi bei kutokana na ubepari uliopo nchini mwetu, wanaopanga bei ni walanguzi,madalali na wafanyabiashara, wakulima wanaburuzwa tu.
 
Tusubili mavuno bei itashuka tu.... Muwe wapole
 
Back
Top Bottom