alisha wahi niambia hicho ni kiswahili cha pwani hukoMie=mimi
Hujajibu swali langu. Kama wewe ndiyo ungekuwa umefanyiwa huo ugaidi ungependa wengine wakae kimya ili lengo la magaidi lisifanikiwe?Lengo ni kupigana na ugaidi kwa kuudhoofisha matakwa yao.
dah! hapa ndio umetutisha zaidi. magaidi kwa lengo gani. siasa, dini au pesa? magaidi wasiodai kitu ni wa aina gani!
asante mkuuTerrorism maana yake ni vitisho, hata nyumbani unapomkemea mwanao ni vitisho "terror".
Inabidi ubadili njia na uanze kumlea bila kutishana.
Chini hapo nimesema, sijuwi. Ni mjadala.
Nashindwa kuelewa kwa nini serikali tukufu ya CCM iko kimya_ hata wabunge wake wanapokuwa wanakabiliwa na matishio ya kutekwa?
Watanzania hatuwezi tukakaa kimya eti tuwakomeshe magaidi kwa kimya chetu!!!.
FaizaFoxy Ndugu yangu nitaumia kiasi gani nikisikia umetekwa na kuteswa?
Je moyo Wangu utahimili kukaa kimya kweli?
Nitafanya niwezalo . Nikishindwa kulipa kisasi basi nitaandika.
Kamwe sitokaa kimya.
Kuna watekaji walitajwa kwa majina na miongoni mwao ni Ramadhan Igwondu, je alichukuliwa hatua gani?
Serikali yetu ya Leo imekuwa Crime Organiser ndio maana iko kimya na hata kwa maswali mazito inakuja na majibu mepesi.
Kama hukifafanui hicho kitu "moles" hamna haja ya kukiandika.Kuna kitu kinaitwa moles kwenye intelijensia.
Sa ndugu yako mfano akitekwa inaama ukae kimiya usitangaze sababu utakuwa una promote ugaidi sister???,,au,,,,,,ivi inawezekana Dola ikafanya ugaidi au matukio ya kigaidi,,,au ili neno gaidi ni kwasisi waislam tu dunianiKinachoendelea sasa hivi Tanzania ni ugaidi (terrorism).
Lengo la ugaidi ni kuwatia watu hofu na kufikisha ujumbe kwa wengi kwa njia ya hofu.
Matukio yanayoongelewa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao yote ya kijamii mpaka nchi za nje kwa sasa ni hayo, kuanzia watu kutekwa, kutolewa bastola hadharani, mauaji ya Kusini huko, watu kukutwa kwenye viroba, kupotea kwa watu na mengi mengineyo, yote yanaashiria ugaidi.
Magaidi hujitokeza na kusema sisi ndiyo tuliyoyafanya hayo ili waogopwe au matakwa yao yatimizwe au hukaa kimya na kuwachochea kivingine kwa lengo hilo hilo.
Matukio ya ugaidi yanapotokea pia hujitokeza wengine ambao hutumia fursa hiyo kufikisha ujumbe wao kwa njia tofauti.
Kwa yanayotokea Tanzania, ukweli ni kuwa, kuna wanaofanya huo ugaidi wa kutisha na kuna wanaotumia huo gaidi kama ni fursa kwao kufikisha ujumbe wao ama kwa kuongezea ugaidi mwingine au kwa kuendeleza hofu kwenye jamii na vyombo husika.
Watanzania tunachotakiwa kufanya ni kukaa kimya na kufunga hii mijadala yote na kuwacha kuripoti matukio yote ya kigaidi ili kushindana na ugaidi.
Gaidi kama matukio yake hayaongelewi kazi yake inakuwa haijafanikiwa.
Kila tunapoyaongea na kuyasambaza ndiyo furaha ya magaidi na ndiyo lengo lao, wengi wajawe na hofu.
Kwanini? Mie sijuwi.