Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,209
- 4,406
UFUNUO WA VILAZA.
1)nasikia mirindimo,na sauti za vilio.
Yanaungua machumo,vinafungwa kimbilio.
Vinapungua vipimo,nguvu yawa egemeo.
Ufunuo wa vilaza,yohana nauandika.
2)wa kale angali wamo,wapo pia na vilio.
Ukishavuma mvumo,lafanya kazi chujio.
Sisimko la zizi mo,mjengoni ni kioo.
Ufunuo wa vilaza,yohana nauandika.
3)naona lachimbwa shimo,wakishika viminyio.
Tafakari azingamo,hapana kwao ni ndio.
Japo waze wa makamo,kinakufa shikilio.
Ufunuo wa vilaza,yohana nauandika.
4)waangamia mazumo,anakufa bwana mbio.
Yadidimia ilimo,limetoboka chujio.
Baragumu la mvumo,lapigwa bila sikio.
Ufunuo wa vilaza,yohana nauandika.
5)yawaka taa mbinguni,kwenye giza liso nuru.
Wabunifu akilini,watapangwa msururu.
Na matusi ya nguoni,wapewe kama kunguru.
Ufunuo wa vilaza,yohana nauandika.
Shairi;UFUNUO WA VILAZA.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@mail.com
1)nasikia mirindimo,na sauti za vilio.
Yanaungua machumo,vinafungwa kimbilio.
Vinapungua vipimo,nguvu yawa egemeo.
Ufunuo wa vilaza,yohana nauandika.
2)wa kale angali wamo,wapo pia na vilio.
Ukishavuma mvumo,lafanya kazi chujio.
Sisimko la zizi mo,mjengoni ni kioo.
Ufunuo wa vilaza,yohana nauandika.
3)naona lachimbwa shimo,wakishika viminyio.
Tafakari azingamo,hapana kwao ni ndio.
Japo waze wa makamo,kinakufa shikilio.
Ufunuo wa vilaza,yohana nauandika.
4)waangamia mazumo,anakufa bwana mbio.
Yadidimia ilimo,limetoboka chujio.
Baragumu la mvumo,lapigwa bila sikio.
Ufunuo wa vilaza,yohana nauandika.
5)yawaka taa mbinguni,kwenye giza liso nuru.
Wabunifu akilini,watapangwa msururu.
Na matusi ya nguoni,wapewe kama kunguru.
Ufunuo wa vilaza,yohana nauandika.
Shairi;UFUNUO WA VILAZA.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@mail.com