2) Baada ya haya uyaonayo atatokea Rais atakayeifanikisha nchi ya Tanzania kuwekwa ktk ramani ya dunia hii ki-uchumi, ki-siasa na ki-michezo
Niiuliza: Ni wakati gani haya yatatokea? Si muda mrefu,
Nikauliza tena: mwaka gani? Hakuna haja ya kujua mwaka!
Nami nikaendelea kudadisi: Je mimi nitayaona haya mabo yakitokea? Ndiyo ktk mwanzo wake utapata nafasi ya kuyaona (kwa sasa mimi nina umri wa miaka 30 na life span ya Mtz 60-70 hivyo unaweja jua ni wakati gani yanaweza kutokea)
Nikauliza tena: Huyo Rais atakuja na mbinu gani?
Atatangaza hali ya hatari nchi nzima na kwamba umasikini ndiye adui yenu mkuu na kuhakikisha kila mwanadamu anafanya kazi kwa bidii mchana kutwa na hata usiku.Atahakikisha uzembe haupo na haya ndiyo atafanya;
a) Atabainisha maeneo yanayofaa kwa kilimo na kuya dedicate kwa watu wasio na kazi mijini na ataboresha sana sera ya kilimo
b) Atahakikiya hakuna ulevi wa watu kulala baa na baa zitapunguzwa mitaani kwa kuwafutia leseni walio ktk makazi ya watu na muda kukaa baa utapunguzwa
c) Vijiwe vyote vya kahawa vitafungwa...wataruhusiwa kunywea nyumbani kwao baada ya kazi
d)Magazeti ya udaku yatafungwa na kuanzishwa magezeti ya kuelimisha watu ktk masuala ya kilimo, ujasiliamali, elimu, michezo, mazingira na afya.
e) Migodi itaanzishwa kwa ubia na sellikali ikimiliki si chini ya 50%
Alipofika hapa nikauliza swali: Mpaka wakati huo kutakuwa madini bado yapo? Ndiyo wanayochukua sasa hivi haijafika hata 2% ya madini yote niliyoibarikia nchi yenu Tanzania.
f) Uteuzi wa watendaji wa serikali kuu (mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi wa makampuni ya umma, wakuu wa vyuo vya umma) watapigiwa kura ya ndiyo au hapana bugeni (wakati huo bunge litakuwa nguvu mno)
g) Rais atamsimamisha kazi kiongozi yeyote anayetajwa kwa tuhuma za rushwa na mtu au kikundi cha watu na kuamuru uchunguzi ufanyike
inaendelea punde...........