Baadhi yetu tunaamini kile tunachokiamini ni kizuri mno, kiasi kwamba lazima tukifikishe kwa wengine hata kama hawataki, watatushukuru baadaye... Jambo ambalo linaondosha hata maana ya neno lenyewe.Wazo zuri naunga mikono yote miwili pia mimi ni mkristo ila kelele zimezidi. Kuna Ibada mmoja ilifanyika muda si mrefu na watu kama 20 walikufa wakati ibada hiyo inaendelea na mpaka leo mimi (sijui wewe) sijasikia lolote la maana kuhusiana na ajali hiyo unategemea makelele tu yawe ya kanisa au msikiti ndio yatawastua unaowalenga kufikisha ujumbe huo wakusikie. Yangu macho na masikio
Wekeni soundproof acheni kelele zisizo na msingi kututangazia matatizo yenu na sisi tuna yetu ila tumekula nayo buyu tuUtakapobanwa ndipo utakapojua unapiga kelele kukera watu au unapiga kelele za kulia kuomba msaada.
Nimefuatilia kwa muda mrefu swala hili kinachowanyima wengi usingizi na judhani sababu ni kelele za nyumba za ibada ni misongo ya mawazo na maisha magumu kama mtu yupo bar analala fofofo licha ya makelele na mziki mkubwa sembuse ukiwa nyumbani
Chief unganeni kama mtaa, muiteni Mtaalamu wa Mipango Miji(Ofisi ya Mkurugenzi) aje awasaidie kutafsiri kibali Cha kufungua Kanisa eneo hilo. Na Kama matumizi ya Ardhi yamezingatiwa!?Baadhi ya nyumba za ibada huhusishwa na kero ya kelele kwa majirani. Huu hapa ni ufumbuzi:
1. Kila jengo la ibada lenye vipaza sauti vifunguliwe kwa manufaa ya walio ndani ya majengo tu.
2. Majengo ya ibada wanaweza kusababisha kelele wapendavyo, lakini watumie udhibiti wa kelele zisifike nje ya majengo yao.
3. Kengele na Adhana za kuita watu ibadani zisichukue zaidi ya muda fulani kama ilivyo kawaida.
4. Viongozi wa dini zote wasaini voluntarily "Code of Conduct" yenye kuahidi kuzingatia suala la udhibiti wa kelele.
5. Serikali iandae mwongozo wa kugredi nyumba za ibada kulingana na ukubwa wa kelele (decibels) zinazofika nje ya mipaka ya nyumba hizo za ibada, kwa kuzingatia "Code of Conduct" tajwa hapo juu.
Matokeo yake, ndani ya nyumba za ibada patakuwa na kelele kadiri waaminio wanavyotaka, pasi na kuleta kero kwa majirani wasiohusika.
Sawasawa basi nikurudishe nyuma wakati teknolojia ya vipaza sauti haijabuniwa kabisa.,NENO LITAWAFUATA HUKOHUKO
Ha ha - Pole sana kwa taarifa yako hazisaidii kitu .Waanzilishi wa hizo dini hawakutumia vipaza sauti na walifanikiwa sana kuwaelimisha watu. Kelele hazimfanyi mtu kuelimika kwenye mada yeyote iwe siasa , dini mziki n.k.NENO LITAWAFUATA HUKOHUKO