Ufisadi's Puppets vs Intellectuals cum scholars | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi's Puppets vs Intellectuals cum scholars

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Geza Ulole, Dec 18, 2009.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,065
  Likes Received: 3,993
  Trophy Points: 280
  18th December 09
  Wanaharakati waunga mkono maazimio ya MNF

  Mwandishi Wetu

  Wanaharakati mbalimbali wamesema maazimio yaliyotolewa kwenye kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), yalikuwa na nia nzuri.
  Wanaharakati hao ni kutoka mashirika ya FemAct, SAHRiNGON, Legal and Human Rights Centre (LHRC), The Leadership Forum, Tamwa, TGNP, HakiArdhi, ForDIA na Wildaf (T).
  Akizungumza kwenye mkutano wa wanaharakati hao jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa LHRC, Francis Kiwango, alisema kumekuwa na taarifa mbalimbali kutoka kwa viongozi na baadhi ya wanajamii kusikika wakikemea na kukosoa maazimio ya kongamano hilo.
  Kongamano hilo lilifanyika kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 2, mwaka huu liliandaliwa na MNF kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
  Kiwango alisema maazimio ya kongamano hilo yalikuwa ni mawazo ya wananchi na viongozi wa Tanzania wenye uzoefu na uongozi, utawala na ukuzaji demokrasia nchini.
  "Kwa maoni yetu sisi kama wanaharakati wa haki za binadamu tunaona yalikuwa na manufaa kwa taifa letu, yalitolewa na wazee, wastaafu, wasomi, viongozi wa dini, viongozi wa siasa na watu mbalimbali waliotumikia taifa letu siku za nyuma," alisema na kuongeza:
  Tumeshtushwa na tunasikitishwa na kauli za kejeli zinazoendelea kutolewa dhidi ya maazimio na waandaaji wa kongamano hilo."
  Aliongeza kuwa maoni yao kuhusu kejeli zinazoendelea kusambazwa, ni ubinafsi na mmomonyoko wa maadili ya uongozi.
  Kwa upande wake, Mratibu wa Programu ya Kuboresha Utawala (Africa), Deus Kibamba, alisema taifa makini haliongozwi na propaganda, bali huongozwa na sera sahihi, utawala bora, utawala wa sheria, uwazi, uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi, kuheshimu haki za binadamu na ushirikishaji wananchi katika maamuzi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Ananilea Nkya, alisema inatakiwa wananchi waingiwe na hasira na chuki juu ya ufisadi, na wasiogope kusema ukweli juu ya viongozi wanaofanya uovu.
  Mwanaharakati kutoka FemAct, Anna Mushi, alisema viongozi wenye maadili walitakiwa kukubaliana na maoni ya watu ili kujitathmini utendaji na kufanyia kazi maoni ya watu.
  Baadhi ya waliowashambulia watendaji wa MNF kuwa waliitisha kongamano hilo kukosoa utendaji wa Rais Jakaya Kikwete ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Kagera, Pius Ngeze; Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba; Waziri wa Kilimo, Ushirika na Masoko, Steven Wasira; Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania (Bahakita); Umoja wa Wainjilisti Tanzania; Rais wa Tanzania Democratic Alliance (Tadea), John Lifa Chipaka na Mwenyekiti wa United Peoples Democratic Party (UPDP), Fahmi Dovutwa.


  NIPASHE
  http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=11378

  Naomba wenye nia njema na nchi hii wachukue muda kutoa wasifu wa watu (kielimu, upeo, integrity, exposure, patriotism, facts analysis n.k.) hawa niliowa-highlight in red kabla sijaambiwa ati niko-biased! naombeni maoni yenu! And please lets your argument come from a free spirit na sio interest fulani (kama mambo ya udini au ukabila)! Maana nimechoka sasa na distortion of realities in this country!
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Stephen Wassira ana kila sababu ya kutokuunga mkono maazimio yaliyotolewa na kongamano la Mwalimu Nyerere Foundation kwasababu za maslahi yake binafsi; huyu bwana alikuwa na dhiki kwa muda mrefu mpaka akafikia kufanya biashara za kimachinga akiuza samaki pale Namanga- DSM, mpaka pale alipookolewa na Jakaya na kupewa ujiko!! Yeye na mgosi Makamba lao ni moja, tumbo street kwanza mambo mengine baadae!!
   
Loading...