Ufisadi waua CARTGILL (T) Ltd! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi waua CARTGILL (T) Ltd!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SpK, Feb 24, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. S

  SpK Member

  #1
  Feb 24, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wadau,

  Jamaa yangu mmoja kanitumia mail ananiambia kulikoni kampuni ya Cargill imefilisika?

  Kampuni ya Cargill haijafilisika! Bali management ya Cargill Tanzania imefilisika kimawazo, managers hawakuwa na mawazo yenye faida, utawala wao sio wenye faida, uongozi wa si wakuleta faida kwa kampuni bali faida mifukoni mwao na familia zao!!!!!

  Hawa jamaa si watu wa ajabu, bali watanzania tulio wengi ndo watu wa ajabu na huenda kwenye ubongo wetu kuna walakini especially kwa tunaokabiziwa makampuni ya kigeni kuyasimamia!!

  U know what? Cargill wanaweka Country Controller katika kila nchi ambayo wana branch. Wenye kampuni wanakutumia kila kitu hadi pesa ya kununulia pamba kwa wakulima, billions of dollars kila mwezi kipindi cha msimu, utake nini watakupa, only what they want from u make sure unafanya kazi, onyesha mapenzi ya dhati kwenye kampuni kwa kuilinda!! Badala yake wewe Mtanzania mwenzangu una-make sure hupati loss kwenye mfuko wako binafsi.

  Baada ya kuona Tanzania wanapata loss in more than 14 yrs consecutively ndo maana wakaona ni bora plant ya Tanzania waihamishie kwingine like Cargill Zambia, Malawi or elsewhere. Walichofanya wakamwambia General Manager (country controller) ambaye ni GM awatangazie employees wote kwamba we’re coming to close the Branch in Tanzania due to failure in running the business in this country!!!

  Kwa sababu yeye ndo source of the losses hakuweza kuwatangazia watu b4 hadi Vice President – Cargill Regional Cotton Africa alipotia timu na Regional HR – Cargill Cotton Africa wakaitisha kikao na kuifunga rasmi Cargill Tanzania kwa sababu ya uzembe wetu sisi wabongo!!!!!

  Hata hiyo Termination letter aliiandika GM mapema kabisa but akashindwa kuwakabidhi watu soon, badala yake akawakabidhi employees baada ya kikao cha VICE PRESD kwisha. Akaweka kwenye barua hiyo sababu feki: low volume, bad weather, economic recession ambazo siyo valid kwa tunaoijua Cargill Tanzania na Cargill Inc kwa ujumla, bali poor management yake yeye ndo imeangusha Cargill hapa Tanzania.

  Sector ya pamba na kilimo kwa ujumla kwa mkoa huu, kampuni hii ilikuwa kama role model, game charger katika kuleta setup ya bei nzuri kwa mkulima wa pamba.

  Kutokuwepo kwa kampuni hii katika nchi ya Tanzania ni pigo kubwa kubali usikubali! Number kubwa ya watu wa Mkoa wa Shinyanga na Wilaya zake: Maswa, Bariadi, Meatu, Kishapu, Kahama, Bukombe, and nearby areas walikuwa wakiishi kwa msaada mkubwa wa Cargill Tanzania Ltd.

  1. Siyo siri wadau, wenyeji karibu wote wa kijiji cha Lalago – Maswa yalipokuwa makao makuu ya Cargill Tanzania walikuwa wakiendesha maisha yao kwa kutegemea kampuni hii. Naamanisha wale wote ambao ni Mama Lishe, wenye maduka na nyumba za wageni, transporters, vijana ambao walikuwa wakifanya vibarua wanapata kitu kidogo, n.k.

  2. Kampuni hii ilikuwa changamoto kubwa kwa maendeleo kwani ilikuwa ikitoa misaada mbalimbali ya kimaendeleo kama vile michango kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa shule za msingi na sekondari pamoja na idara zingine mbalimbali.

  3. Kampuni hii alikuwa ni mlipaji mzuri wa kodi mabalimbali kwa serikali na mashirika binafsi. Kwa mfano Cargill imekuwa ikilipa bill za TANESCO kiasi kisichopungua milioni 24 kila mwezi, TTCL gharama za simu kiasi cha milioni 1.5 kila mwezi, TRA (WHT, PAYE, SDL) kiasi cha zaidi ya milioni 10 kila mwezi. Society Levies kiasi cha zaidi ya milioni 100 kila msimu, bill za mafuta ya diesel GBP kiasi cha zaidi ya milioni 500 kila msimu, na wateja wengine kibao wa kampuni hii kama vile GALAME, SHINYANGA MWANANCHI GARAGE, SHINYANGA INDUSTRIAL EQUIPMENT, TASS, PRECISION AIR, WALJIS TRAVEL BUREAU LTD, MANJIS KEY SPEIALIST, ITAL SHOES, MOEVENPICK ROYAL PALM HOTEL, NEW AFRICA HOTEL, na wengine kibao.

  Impact ya kufungwa kwa kampuni hii si ndogo na ni kubwa sana kwa wadau wa pamba, wakulima, wanavijiji wa maeneo hayo, wateja wa kampuni hii n.k.
   
  Last edited: Feb 26, 2009
 2. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2013
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wabunge wa Shinyanga muda si mrefu wataanza kupiga kelele za kutaka bei ya pamba ipande wakati mizizi wameikata wenyewe!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...