Chunda
Senior Member
- Apr 7, 2016
- 182
- 251
Harufu ya ufisadi imetanda katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kuhusu mabadiliko yaliyosababisha kuongezeka kwa gharama za ujenzi (Variations) kwa jengo la ghorofa tatu kwa zaidi ya asilimia 40, tofauti na mkataba wa awali. Ujenzi wa jengo hilo sasa unahusishwa na vitendo vya kifisadi vinavyohusisha Menejimenti ya Chuo hicho, Mkandarasi anayetekeleza mradi huo pamoja na Mtaalamu Mshauri wa mradi.Taarifa ambazo Raia mwema imezikusanya kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zinaonyesha kuwa hadi Decemba mwaka jana, jengo hilo lilikuwa limegharimu shilingi bilioni 3.8, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya shilingi bilioni 1.2 kutoka mkataba wa awali.
Takwimu hizo zinathibitihwa na kauli ya Mkuu wa Chuo hicho, Dk Richard Masika, katika hotuba yake kwenye mahafali ya Chuo Januari 16, mwaka huu, ambapo alikaririwa akisema kuwa jengo hilo limegharimu takriban shilingi bilioni 4. Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa balozi wa Norway nchini, Hange-Marie Kaarstad, ambaye nchi yake ni moja ya wafadhili wakubwa wa Chuo hicho. Jengo hilo ambalo ni madarasa ya wanafunzi wa kitivo cha Ujenzi na Kilimo cha Umwagiliaji (Civil and Irrigation Building) pamoja na ofisi za wakufunzi, ujenzi wake ulianza mwaka 2011.
Nyaraka mbalimbali zilizofikia Raia Mwema zinaonyesha kuwa katika mkataba “mama” wa ujenzi wa jengo hilo gharama zake halisi zilikuwa shilingi 2,681,850,463.00. Chuo hicho kilisaini mkataba wa ujenzi huo na kampuni ya ukandarasi ya Nordic construction yenye anwani ya posta 13391 ya jijini Dar es Salaam, Julai 27, mwaka 2011. Katika mradi huo mtaalamu mshauri ni kampuni ya Kapwani Architect ya Arusha na mradi ulipaswa kutekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa mujibu wa mkataba, ambapo ujenzi wake ulitakiwa kukamilika kati ya Julai na Agosti, mwaka 2012.
Ongezeko la Gharama
Hata hivyo, gharama za mradi huo ziliongezeka kwa kiasi cha shilingi 740,766,676.00, Januari 2013, ikiwa ni miezi sita zaidi kinyume cha makubaliano ya kukamilisha ujenzi. Katika barua yenye kumbukumbu namba KA/ATC/08, meneja wa mradi kutoka kampuni ya Kapwani Archtect kupitia mkurugenzi wake, Rashid Kapwani, alimwandikia mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Dk Richard Masika kumfahamisha kuhusu ongezeko hilo la fedha kukamilisha mradi. Naambatanisha ripoti ya mkadiriaji wa ujenzi wa mradi kampuni ya M/S2M ambayo ilikasimu kampuni ya M/S JB Cost care Consult Ltd, ongezeko la gharama ni “740,766,676.00” inasomeka sehemu ya barua hiyo.
Ongezeko hilo ni zaidi ya asilimia20 ya bei iliyokuwa kwenye mkataba wa ujenzi kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na gharama za ongezeko ilipaswa kuwa shilingi 536,370,092.00 kama ingekuwa lazima. Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka Chuo hicho, kati ya mwaka 2013/2014 gharama hizo ziliongezeka na kufikia zaidi ya shilingi bilioni 1.2 hivyo kwenda kinyume cha Sheria hiyo ya manunuzi ya umma.
Taarifa hizo zinabainisha kuwa hadi kufikia mwezi machi mwaka huu, jengo hilo ingawa linatumika halijakabidhiwa rasmi kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo marekebisho katika ujenzi kutokana na “ulipuaji” uliofanywa na mkandarasi. Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma Namba 7 ya mwaka 2011 kifungu cha 77 (2) ongezeko la gharama katika mradi wa ujenzi lazima ziwe chini ya asilimia 20 ya gharama halisi iliyopo kwenye mkataba halali. “Kwa mantiki hiyo utaona kuwa gharama za ujenzi katika mradi huo zilifikia karibu asilimia 40 ya gharama halisi zilizopo katika mkataba wa ujenzi na hali hiyo inatokana na kuwepo kwa vitendo vya kifisadi baina ya Menejimenti ya Chuo, Mkandarasi na Meneja wa mradi”. Kilidai chanzo chetu kutoka ndani ya Chuo hicho.
Harufu ya Ufisadi
Kinachodaiwa kuwa kuna harufu ya ufisadi katika mradi huo kinaonekana katika ongezeko la gharama za mradi ambapo mchanganuo wake unaonyesha dosari nyingi. Kwa mujibu wa mchanganuo huo ambao raia mwema inayo nakala yake, unaonyesha kuwa kiasi cha shilingi 86,627,500/= zilihitajika au kutumika kwa ajili ya milango. Kiasi hicho kinaelezwa kuwa ni kikubwa ukilinganisha na idadi ya milango katika jengo hilo ambayo haizidi 50 na fedha hizo zikigawanywa kwa kiasi cha shilingi 300,000/= kwa kila mlango ingenunuliwa milango zaidi ya 280.
Hata hivyo taarifa za ndani zinaonyesha kuwa milango iliyotumika katika ujenzi huo ni ile ya dharura (flash doors) ambayo raia mwema imehakiki katika maduka mengi ya vifaa vya ujenzi mjini Arusha huuzwa kati ya shilingi 80,000/= na 100,000/=. Mmoja wa wataalamu wa ujenzi aliliambia gazeti hili kuwa inashangaza kama kiasi hicho cha fedha kiliongezwa kama gharama, kwa kuwa hakuna mkataba wa ujenzi unaosainiwa bila kujumuisha gharama za milango. “Sijui kama mkataba wa awali inakuwaje milango haikujumuishwa? Maana haiwezekani hilo jengo lingekabidhiwa bila milango na hoja yangu ni kwamba milango haiwezi kuwa sehemu ya ongezeko la gharama” alieleza mtaalamu huyo kwa sharti la kutokutaja jina lake gazetini. Utata mwingine katika mchanganuo huo unaonekana katika ongezeko la gharama za ujenzi wa kibanda cha walinzi (askari hut) ambapo shilingi 42,223,173/= zilitumika. Taarifa zinaonyesha fedha zimetumika isivyo kutokana na kibanda hicho cha walinzi kutokuwamo katika mkataba wa ujenzi wa jengo na kipo mbali kabisa na eneo la ujenzi.
Aidha pia mchanganuo huo unaonyesha kuwa kiasi cha shilingi 18,665,500/= na 30,270,500/= zilitumika kwa wakati mmoja kujenga tenki la maji la chini ya ardhi (underground water tank) ambalo hata hivyo linadaiwa kuwa lilikuwapo. Ongezeko la gharama zingine zenye harufu ya ufisadi ni pamoja na shilingi 81,600,000/= kwa ajili ya ununuzi wa vyuma na nondo za ujenzi ambazo taarifa zinadai kuwa hazikununuliwa kabisa.
Kwa mujibu wa nyaraka kutoka ndani ya Chuo hicho zilizotumwa kwenye mamlaka mbalimbali za serikali, inadaiwa kuwa katika ujenzi mkandarasi, kampuni ya Nordic alifyatulia matofali ya ujenzi katika eneo la Chuo na kutumia rasilimali za chuo kama umeme na maji. Madai hayo yanaonyesha kuwa Mkuu wa Chuo Dk Richard Masika na makamu wake Dk Masoud Senzia walipewa matofali zaidi ya 20,000 yaliyobaki katika ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zao binafsi. Mchanganuo wa kitaalamu unaonyesha kuwa matofali hayo yangeweza kujenga madarasa ya shule ya msingi au sekondari zaidi ya 22.
Kauli za wahusika
Akizungumza na Raia mwema mwishoni mwa wiki, Dk Richard Masika alisema anauguliwa na mama yake mzazi, mkoani Kilimanjaro na kwamba alikuwa katika wakati mgumu kuzungumzia suala hilo kwa kina. Hata hivyo alisema kuwa madai yote kuhusiana na uongozi wake chuoni hapo yamekwisha wasilishwa katika mamlaka mbalimbali za kiserikali na walikuwa bado hawajatoa uamuzi wowote. “Kwa mfano suala la ujenzi wa jengo hilo lilikwisha kufanyiwa uchunguzi na mamlaka mbalimbali za kiserikali na kufanyia pia ukaguzi, ikiwamo ofisi ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Kwa hiyo, mimi siwezi kulizungumzia tena wakati mamlaka za juu wanazo taarifa zote na ndiyo wenye uamuzi” alisema Dk Masika.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dr Masoud Senzia alikanusha kuchukua sehemu ya matofali yaliyobaki katika ujenzi na kubainisha kuwa taarifa hizo ni potofu na zinapikwa na baadhi ya watumishi wa Chuo huku akiwataja kwa najina. “Hakuna popote tarifa imetolewa kuwa kuna matofali yamepotea au kuibiwa hapa chuoni, kama nilivyokueleza hayo ni majungu na fitina tu kutoka kwa watumishi wa Chuo. Hao ndio wamekuwa mwiba kwa Chuo chetu kutokana na chuki walionayo baada ya wengine kusimamishwa kazi na wengine kuvuliwa madaraka yao” alisema Dk Senzia.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Nordic Construction Ltd, Nobert Safari, alisema suala la ongezeko la gharama hizo za ujenzi haliko chini ya mkandarasi bali mtaalamu mshauri na mtaalamu wa ukadiriaji wa vifaa vya ujenzi. “Kwanza huo mradi umenitia hasara kubwa tu kutokana na ucheleweshaji wa malipo, mpaka sasa bado sijalipwa fedha zangu na hiyo imesababisha mimi kuingia hasara” alisema Safari bila kutaja kiasi cha fedha anazodai chuoni hapo. Juhudi za kumpata meneja wa mradi, Rashid Kapwani wa kampuni ya Kapwani Architects hazikuweza kufanikiwa baada ya simu yake kutokuwa hewani kwa muda mrefu.
Hii si mara ya kwanza kwa Chuo Cha ufundi Arusha na uongozi wake kuhusishwa na ufisadi ambapo mwaka 2014, gazeti hili liliwahi kuripoti kuhusu matumizi mabaya ya fedha na madaraka yaliyofanywa na Mkuu wa Chuo hicho.
Chanzo: Raia Mwema