Ufisadi Wa Sita Ni Wakweli?

Chibingwa

Member
Jan 17, 2008
49
7
HABARI ZA KUTHIBITIKA!!.

Ufisadi wa Samwel Sitta

Ama kweli, ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni! Kama unadhani vigogo wa EPA ni mafisadi peke yao , basi ulikuwa hujamfahamu Spika wa Bunge SAMUEL JOHN TEGEZA SITTA ! Ukimsikiliza anapoongea unaweza kuamini kwamba kiongozi huyo wa Bunge ni msafi kutokana na umahiri wake wa kujivalisha sifa kemkem - Mr Misifa.
Unakumbuka hivi karibuni alivyomtukana Naibu Spika eti hawezi kusimamia mambo nyeti mpaka awepo yeye mwenye Bunge? ! Kisa nini? Kupenda sifa na kumdhalilisha mwenzake mbele ya umma, halafu bado anaendelea kuliita Bunge eti ni chombo cha kidemokrasia!
Tumebaini kwamba Sitta amekuwa akijimiminia sifa nyingi ili kulinda ufisadi anaoufanya usigundulike katika jamii yetu. Ngoja nikupe tone tu la madhambi yake kwa umma ili uone ni hatua gani utachukua, na ili na yeye ajipime kwa nafasi yake.
Angalia uchafu huu:-
- Anatumia vibaya fedha za umma. Amekuwa akitumia msaidizi wake kuchota mapesa kwa kisingizio kuwa ni masurufu ya safari za ndani na nje ya nchi. Kila safari ya siku moja ndani ya nchi huchukua shilingi Milioni tano (5,000,000/=), na kila safari ya siku moja nje ya nchi huchukua shilingi Milioni Kumi na Tano (15,000,0000/=).
Ameshindwa kufanya marejesho ya masurufu (imprest) hayo, licha ya kupeleka risiti kadhaa za kughushi/za uongo kwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Bunge.
Mpaka sasa anadaiwa jumla ya shilingi Milioni sitini (60,000,000/=) za masurufu.
- SITTA hupeleka risiti za uongo kwa Mhasibu Mkuu, zikionesha madai kutoka Oysterbay Pharmacy ya Shilingi Milioni Mbili ( 2,000,000/= ) aliyotumia kwa tiba kila wiki.
- Amekuwa akilazimisha hawara yake wa Hospitali ya Aga Khan naye alipwe posho kama wabunge anapokwenda naye Dodoma . Kwa mfano, hawara huyo alilipwa 'per diem' kuanzia tarehe 13/12/2007 hadi tarehe 31/01/2008 ( Siku 50). Huo ni Ufisadi mkubwa!

- Anaye kimada wake mwingine anayekwenda kwa jina la ASIA ambaye anaishi nyumba Na. 111 karibu na Mahakama ya Ardhi Upanga na amezaa naye. Huko mtaani kwao kimada huyo hujiita mama SITTA, na ni dada yake aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa iliyokuwa Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC). Mwanamke huyo muda wote hutumia gari la Ofisi ya Bunge STK 232 Toyota RAV 4.
- Pia anaye kimada mwingine (jina limehifadhiwa) ambaye anaishi kinondoni ( Livingstone), mtaa wa Honolulu katika nyumba ya kupanga inayomilikiwa na dada yake Kawawa. Nyumba hiyo inatazamana na Nyumba Na. KH.MK/No. 337 katika mtaa huo huo. Kimada huyo hutumia gari ya kiofisi ya Spika mwenyewe STK 3002.

- Vimada wote hao hupata huduma za maji na umeme kwa gharama za Ofisi ya Bunge. Kuna kipindi mke halali wa Spika, aliwahi kulalamikia hali hiyo. Kuna siku maji yalikatika nyumbani, mke wa Spika akaomba apelekewe ' bowser' la maji na Ofisi ya Bunge. Ohooo! Watekelezaji wakapeleka maji kimakosa kwa kimada. Mama Sitta akashtukia dili.
- Kuna taarifa kwamba mnamo Mwezi Oktoba 2007, Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) iligundua mapungufu makubwa katika matumizi ya fedha yaliyofanywa na Spika SITTA. nimedokezwa kuwa Spika aliwanyamazisha wajumbe wa kamati hiyo, ambapo aliwatishia kutowapatia posho na safari za nje kama wangeyafumua mapungufu yake hadharani! Hapo inaonesha kuwa wajumbe hao walipewa rushwa!!
- Kama JK anataka viongozi wa kisiasa na wa serikali watenganishe biashara na uongozi wa ku - 'sacrifice'kimojawapo, hilo litakuwa gumu kwa sababu Sitta alipokuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha cha Uwekezaji nchini (TIC) alitumia nafasi hiyo kuingia ubia na wafanyabiashara wengi wa Kigeni. Je, Wizara ya Maliasili na Utalii inatambua kuwa Spika ana hisa kwenye kampuni moja ya Kichina inayosafirisha nagogo licha ya marufuku yaliyowekwa?!
- Nililokupa hapo ni tone tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom