Ufisadi wa Sh1.4 bil waibuka TFF

Ufisadi wa Sh1.4 bil waibuka TFF

Nokla

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2012
Posts
3,190
Reaction score
1,780
Dar es Salaam.

Ndoa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) sasa iko shakani baada ya kampuni hiyo kubwa nchini kutishia kusitisha udhamini wake wa zaidi ya Sh17 bilioni kutokana na kubaini matumizi mabaya ya mamilioni ya fedha, Mwananchi inaweza kukuthibitishia.

TBL na TFF zilisaini mkataba huo wa udhamini wa timu ya Taifa ya soka, Taifa Stars mwaka 2012 ukiwa na thamani ya Dola 10 milioni za Marekani kwa miaka mitano na huu ni mwaka wa pili wa mkataba huo wa kihistoria kwa ukubwa ambao ulianza Mei, 2012.

Habari ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kuwa ufisadi huo uligundulika kwenye akaunti ya fedha za udhamini wakati wa ukaguzi wa robo nne za mwisho katika kipindi cha udhamini kinachoishia Mei, 2014.

Ukaguzi huo ulionyesha kuwa kulikuwa na matumizi ya zaidi ya Dola 903,000 (sawa na zaidi ya Sh1.4 bilioni) ambayo yalifanywa bila ya kuheshimu masharti ya mkataba na kwa kukiuka kanuni za fedha za TFF.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi na katibu mkuu, Celestine Mwesiga hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo kwa kuwa wako safarini Uswisi, wakati juhudi za kumpata mkurugenzi wa masoko wa TBL, Kushila Thomas hazikufanikiwa.

Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hajui lolote, wakati Kaimu Katibu Mkuu, Danny Msangi alimtaka mwandishi kusubiri hadi Alhamisi wakati viongozi hao watakapokuwa wamerejea nchini.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe hakuweza pia kujibu chochote alipoulizwa kuhusu suala hilo na badala yake alisema alikuwa kwenye kikao.

Hata hivyo, kwa mujibu wa habari hizo za uhakika, mkurugenzi huyo wa masoko wa TBL alimwandikia rais wa TFF (Malinzi) kueleza kusikitishwa na kitendo cha shirikisho hilo kushindwa kuonyesha vielelezo vya kuthibitisha matumihayo, licha ya wakaguzi kuwapa fursa ya kujibu na kuwasilisha vielelezo.

Katika fedha hizo, TFF inadaiwa kutumia zaidi ya Dola 381,000 (sawa na zaidi ya Sh600 milioni) kwa shughuli ambazo ziko nje ya makubaliano ya mkataba, wakati matumizi mengine ya zaidi ya Dola 174,000 (zaidi ya Sh270 milioni), pia yanatia shaka.

"Huu ni ukiukwaji wa wazi wa makubaliano ya udhamini ambayo yanaipa TBL haki ya kufanya uamuzi kwa mujibu wa mkataba, ukiwemo wa kuvunja makubaliano ya udhamini," inaeleza barua hiyo ya Julai 22, 2014 aliyoandikiwa rais wa TFF.


Mkurugenzi huyo alitoa nafasi nyingine kwa TFF kupitia upya matokeo hayo ya ukaguzi huo na kutoa majibu husika katika kila suala lililoibuliwa na kuambatanisha na nyaraka za ushahidi wa matumizi.

"Hii inatakiwa ifanywe ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya barua hii. Kwa sasa, fedha hazitatolewa hadi hapo masuala yaliyoibuliwa kwenye ukaguzi yatakapotatuliwa," inaeleza barua hiyo.

Katika kujibu barua hiyo, TFF iliiandikia TBL Julai 23 kueleza kuwa kutokana na kukabiliwa na mechi muhimu ya marudiano ya kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 dhidi ya Msumbiji iliyofanyika Agosti 3, na hali kadhalika mechi ya timu ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 dhidi ya Afrika Kusini, wafanyakazi wote wamejikita kwenye maandalizi ya michezo hiyo.

"Imani yetu ya dhati ni kwamba TBL, kama mmoja wa wadau wakubwa, si katika soka tu bali maisha ya Watanzania, inaelewa kwamba jitihada ambazo tunafanya sasa ni jitihada zenu pia na ni lazima kwamba shirikisho letu lijikite kikamilifu kwenye kazi muhimu iliyo mbele yetu," ilieleza barua hiyo ya rais wa TFF.TFF inatakiwa ipate mafanikio na kwa kufanikiwa, bia ya Kilimanjaro itapata sifa kubwa. Kwa hiyo, kwa heshima, tunaomba, katika wakati huu muhimu katika historia ya timu yetu ya taifa, suala hili liwekwe pembeni hadi hapo tutakapocheza mechi ya marudiano, Agosti 3 na kurejea Dar es salaam. Tunaomba mtuvumilie hadi Septemba 1, 2014."

Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema kuwa miongoni mwa matumizi ambayo TBL inahoji ni malipo ya deni la zaidi ya Dola 160,000 alizolipwa bosi mmoja wa juu wa TFF, kitu ambacho ni kinyume na masharti ya mkataba, takriban Dola 30,000 zilizohamishwa kutoka kwenye akaunti hiyo bila ya maelezo wala vielelezo vya kuthibitisha matumizi.

Pia, Dola 14,000 zililipwa kwa kutumia profoma invoice, kinyume na kanuni za fedha, hali kadhalika malipo kwa makocha, viongozi wa TFF, tiketi za ndege, posho za mikutano, gharama za kambi na safari za watendaji ambayo hayana vielelezo vya uthibitisho.

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, makamu wa rais wa TFF, Karia alisema: "Binafsi nilikuwa nje ya nchi kwa kipindi kirefu, nimerudi, sijaambiwa chochote na katibu wala barua ya TBL sijaiona.

Nadhani katibu ndiye mtu sahihi anayeweza kuzungumzia hilo, sijaiona hiyo barua wala TBL hawajaniambia chochote na kutaka suala hilo aulizwe meneja wa masuala ya fedha, Danny Msangi ambaye pia ni anakaimu nafasi ya katibu mkuu ambaye yupo nje ya nchi kikazi."

Naye Msangi alisema: "Mimi sijaona hiyo barua, wala sijui chochote. Naomba umsubiri katibu anarudi Alhamisi (kesho) ndiye ataweza kulizungumzia. Inawezekana barua hiyo ipo kwake kwangu haijafika."


Mwananchi
 
Lol! Malinzi maji shingoni sasa... bora ujiuzulu kuzuia madudu mengine kuibuka. Maana......
 
Kusema kweli mm nmepoteza imani na malinzi toka alivyohamisha ofisi
 
TFF ipewe faida ya shaka (benefit of doubt). Tusubiri jawabu yao, kama wanayo. Bila ya hivyo inakuwa ni mapema mno kuijadili mada hii. Hiyo ni kwa usalama wetu. Maana tukianza kuwatia hatiani na baadaye ikaja kubainika kwamba hakuna ubadhirifu au upotevu, hatujui tutafungiwa kufanya nini wala miaka mingapi! Tusije tukamshtukia Ndumbaru tuliyekutana naye kwenye jela ya TFF anatangulia kumaliza muda wake kabla ya sisi!
 
jamani mpeni mda malinzi maana tangu ameingia madarakan amekuta hali ya mambo ndani ya shirikisho sio shwari madeni kibao yaliyoachwa na raisi aliyepita leodiger tenga na changamoto lukuki, kama tunavyoweza kuwapa mda makocha wa timu zetu za taifa pamoja na vilabu ningependa na yeye apewe mda
 
Dar es Salaam.

Ndoa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) sasa iko shakani baada ya kampuni hiyo kubwa nchini kutishia kusitisha udhamini wake wa zaidi ya Sh17 bilioni kutokana na kubaini matumizi mabaya ya mamilioni ya fedha, Mwananchi inaweza kukuthibitishia.

TBL na TFF zilisaini mkataba huo wa udhamini wa timu ya Taifa ya soka, Taifa Stars mwaka 2012 ukiwa na thamani ya Dola 10 milioni za Marekani kwa miaka mitano na huu ni mwaka wa pili wa mkataba huo wa kihistoria kwa ukubwa ambao ulianza Mei, 2012.

Habari ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kuwa ufisadi huo uligundulika kwenye akaunti ya fedha za udhamini wakati wa ukaguzi wa robo nne za mwisho katika kipindi cha udhamini kinachoishia Mei, 2014.

Ukaguzi huo ulionyesha kuwa kulikuwa na matumizi ya zaidi ya Dola 903,000 (sawa na zaidi ya Sh1.4 bilioni) ambayo yalifanywa bila ya kuheshimu masharti ya mkataba na kwa kukiuka kanuni za fedha za TFF.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi na katibu mkuu, Celestine Mwesiga hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo kwa kuwa wako safarini Uswisi, wakati juhudi za kumpata mkurugenzi wa masoko wa TBL, Kushila Thomas hazikufanikiwa.

Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hajui lolote, wakati Kaimu Katibu Mkuu, Danny Msangi alimtaka mwandishi kusubiri hadi Alhamisi wakati viongozi hao watakapokuwa wamerejea nchini.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe hakuweza pia kujibu chochote alipoulizwa kuhusu suala hilo na badala yake alisema alikuwa kwenye kikao.

Hata hivyo, kwa mujibu wa habari hizo za uhakika, mkurugenzi huyo wa masoko wa TBL alimwandikia rais wa TFF (Malinzi) kueleza kusikitishwa na kitendo cha shirikisho hilo kushindwa kuonyesha vielelezo vya kuthibitisha matumihayo, licha ya wakaguzi kuwapa fursa ya kujibu na kuwasilisha vielelezo.

Katika fedha hizo, TFF inadaiwa kutumia zaidi ya Dola 381,000 (sawa na zaidi ya Sh600 milioni) kwa shughuli ambazo ziko nje ya makubaliano ya mkataba, wakati matumizi mengine ya zaidi ya Dola 174,000 (zaidi ya Sh270 milioni), pia yanatia shaka.

"Huu ni ukiukwaji wa wazi wa makubaliano ya udhamini ambayo yanaipa TBL haki ya kufanya uamuzi kwa mujibu wa mkataba, ukiwemo wa kuvunja makubaliano ya udhamini," inaeleza barua hiyo ya Julai 22, 2014 aliyoandikiwa rais wa TFF.


Mkurugenzi huyo alitoa nafasi nyingine kwa TFF kupitia upya matokeo hayo ya ukaguzi huo na kutoa majibu husika katika kila suala lililoibuliwa na kuambatanisha na nyaraka za ushahidi wa matumizi.

"Hii inatakiwa ifanywe ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya barua hii. Kwa sasa, fedha hazitatolewa hadi hapo masuala yaliyoibuliwa kwenye ukaguzi yatakapotatuliwa," inaeleza barua hiyo.

Katika kujibu barua hiyo, TFF iliiandikia TBL Julai 23 kueleza kuwa kutokana na kukabiliwa na mechi muhimu ya marudiano ya kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 dhidi ya Msumbiji iliyofanyika Agosti 3, na hali kadhalika mechi ya timu ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 dhidi ya Afrika Kusini, wafanyakazi wote wamejikita kwenye maandalizi ya michezo hiyo.

"Imani yetu ya dhati ni kwamba TBL, kama mmoja wa wadau wakubwa, si katika soka tu bali maisha ya Watanzania, inaelewa kwamba jitihada ambazo tunafanya sasa ni jitihada zenu pia na ni lazima kwamba shirikisho letu lijikite kikamilifu kwenye kazi muhimu iliyo mbele yetu," ilieleza barua hiyo ya rais wa TFF.TFF inatakiwa ipate mafanikio na kwa kufanikiwa, bia ya Kilimanjaro itapata sifa kubwa. Kwa hiyo, kwa heshima, tunaomba, katika wakati huu muhimu katika historia ya timu yetu ya taifa, suala hili liwekwe pembeni hadi hapo tutakapocheza mechi ya marudiano, Agosti 3 na kurejea Dar es salaam. Tunaomba mtuvumilie hadi Septemba 1, 2014."

Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema kuwa miongoni mwa matumizi ambayo TBL inahoji ni malipo ya deni la zaidi ya Dola 160,000 alizolipwa bosi mmoja wa juu wa TFF, kitu ambacho ni kinyume na masharti ya mkataba, takriban Dola 30,000 zilizohamishwa kutoka kwenye akaunti hiyo bila ya maelezo wala vielelezo vya kuthibitisha matumizi.

Pia, Dola 14,000 zililipwa kwa kutumia profoma invoice, kinyume na kanuni za fedha, hali kadhalika malipo kwa makocha, viongozi wa TFF, tiketi za ndege, posho za mikutano, gharama za kambi na safari za watendaji ambayo hayana vielelezo vya uthibitisho.

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, makamu wa rais wa TFF, Karia alisema: "Binafsi nilikuwa nje ya nchi kwa kipindi kirefu, nimerudi, sijaambiwa chochote na katibu wala barua ya TBL sijaiona.

Nadhani katibu ndiye mtu sahihi anayeweza kuzungumzia hilo, sijaiona hiyo barua wala TBL hawajaniambia chochote na kutaka suala hilo aulizwe meneja wa masuala ya fedha, Danny Msangi ambaye pia ni anakaimu nafasi ya katibu mkuu ambaye yupo nje ya nchi kikazi."

Naye Msangi alisema: "Mimi sijaona hiyo barua, wala sijui chochote. Naomba umsubiri katibu anarudi Alhamisi (kesho) ndiye ataweza kulizungumzia. Inawezekana barua hiyo ipo kwake kwangu haijafika."


Mwananchi

Kama Rage alifungwa kwa ufisadi katika kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT) nahisi Jamal Malinzi na wenzake wanaweza kufikishwa mahakamani kwa ufisadi huu ikiwa taarifa hii ni ya kweli. Ikumbukwe haya ni madudu yanayohesabika kuwa ni Makosa ya Jinai hakuna suala la kuwa 'Mambo ya Soka Hayapelekwi Mahakamani'. Nadhani Dr. Ndumbaro anaweza kupata kibarua cha kuiwakilisha Jamhuri dhidi ya viongozi wa TFF, ikiwa hivyo sipati picha hali ya Malinzi et al. itakuwaje!
 
Last edited by a moderator:


Pia, Dola 14,000 zililipwa kwa kutumia profoma invoice, kinyume na kanuni za fedha, hali
kadhalika malipo kwa makocha, viongozi wa TFF, tiketi za ndege, posho za mikutano, gharama za kambi na safari za watendaji ambayo hayana vielelezo vya uthibitisho.

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, makamu wa rais wa TFF, Karia alisema: "Binafsi nilikuwa nje ya nchi kwa kipindi kirefu, nimerudi, sijaambiwa chochote na katibu wala barua ya TBL sijaiona.

Mwananchi


Hapo wamenikumbusha ya MANJI na YANGA, Mchezaji anasjiliwa kwa 100,000 then kwenye kitabu wankubalina kuw ainandikwa 500,000 alafu 400,000 inayozidi wanapiga, na kwenye mshahara hivyohivyo,

Unaulizwa unataka ngapi ohh mimi 5, basi sisi tutakupa 10, 5 yetu.

hakika hata huyu kocha wa sasa naamini mshahra wake kuna uwezekano haupati wote ila angawana na wajanja wachache.

CC: Jamal Malinzi
 
Last edited by a moderator:
Kama Rage alifungwa kwa ufisadi katika kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT) nahisi Jamal Malinzi na wenzake wanaweza kufikishwa mahakamani kwa ufisadi huu ikiwa taarifa hii ni ya kweli. Ikumbukwe haya ni madudu yanayohesabika kuwa ni Makosa ya Jinai hakuna suala la kuwa 'Mambo ya Soka Hayapelekwi Mahakamani'. Nadhani Dr. Ndumbaro anaweza kupata kibarua cha kuiwakilisha Jamhuri dhidi ya viongozi wa TFF, ikiwa hivyo sipati picha hali ya Malinzi et al. itakuwaje!

Mkuu hseria za TFF naamini unatakuwa unazijua, Je ni annai mwenye haki ya Kumshtaki raisi wa TFF na Viongozi wenzie?
 
Back
Top Bottom