Ufisadi wa kutisha idara ya uhamiaji

Ufisadi wa kutisha idara ya uhamiaji

rungulugujo

New Member
Joined
Dec 26, 2010
Posts
2
Reaction score
0
Ni jambo la kushangaza kuona kuwa pamoja na kelele zinazopigwa na viongozi wetu wa serikali kuhusu kuachana na matumizi mabaya ya fedha za serikali idara ya Uhamiaji imeingia kwa makusudi na kununua mtambo wa kudurufu nyaraka wenye thamani ya Tsh 1bn kutoka kampuni ya GLOBA AGENCY ya mjini DSM bila kufuata taratibu za manunuzi.Mtambo huu umeshafungwa huko kijichi ndani ya majengo ya Uhamiaji bila kufuata taratibu za manunuzi,KATIBU MKUU na WAZIRI WAKE walitembelea kijichi na kuingizwa mkenge na maafisa Waandamizi wa Idara ya kuwa mtambo huo unasaidia sana katika kupunguza ukosefu wa nyaraka za Idara wakati siyo kweli kwani Mtambo huo unatoa copy tu baadhi ya nyaraka na hadi sasa kampuni hiyo inadai idara zaidi ya Tsh 300,000,000/=.cha kushangaza kampuni hiyo inatumia jengo,malighafi za kutengeneza vitu hivyo,umeme na watumishi wa Idara.huu ni wizi ambao sisi watumishi hususani wa kiwamdani kijichi tumeamua kulifikisha suala hili kuptia vyombo vya habari ili wakubwa waweze kuona kilio chetu na jinsi mali ya umma inavyoliwa nawachache.wahusika wa mradi huu ni kamishna wa fedha na utawala pamoja na watumishi wakitengo cha mipango na store ambao ndiyo wanajua mchezo huu mchafu
 
Duuh aisee hii inatisha kwa kweli....! Sijui ni lini huu wimbo wa "Ufisadi" utaisha masikioni mwetu. Manake kila unapogusa kuna ufisadi...!
 
Ufisadi unaletwa na serikali yenyewe, kitu kama hicho hakiwezi kufanywa na uhamiaji peke yao labda kama mwenye thread kakosea kiasi cha pesa. 1bn kwa ajili ya photocopier machine au naota?
 
Duhi!kweli huyo waziri na katibu wake wamefunikwa;maana nilishindwa kusafiri kwenda Kampala kwa kukosa hati ya dharula katika ofisi Za uhamiaji Arusha waka nielekeza Moshi nako nilikosa nikarudi Arusha wakaniambia niwapatie elfu 50 wanitumie Kondoa Dodoma ndio zina patikana:kweli hii imetulia
 
katika uhamiaji si hayo tu,kuna mambo mengi sana,hata watumishi wa idara hii wanapuuzwa mawazo yao,hawasikilizwi,pia viongozi hawana nafsi ya kuwasikiliza watendaji wa chini ila wapo tayari kusikiliza majungu na kuyatendea kazi bila kumhusisha yule mtendaji wa chini anayepigwa jungu.inauma sana kuona viongozi wa namna hii wasio na uwezo wa kutafakari na kufikiri
 
Back
Top Bottom