Ufisadi wa 6.7Bilioni Wilayani Kishapu Shinyanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa 6.7Bilioni Wilayani Kishapu Shinyanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bornvilla, Mar 23, 2012.

 1. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani hapa limewasimamisha kazi maofisa waandamizi 13 wa halmashauri hiyo baada ya kuipitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Uamuzi wa kuwasimamisha kazi watumishi hao, ulifikiwa juzi katika kikao cha Baraza hilo baada ya kuipitia na kuijadili taarifa hiyo iliyobaini matumizi mabaya ya fedha za umma na wizi wa zaidi ya Sh bilioni 6.7.

  Baada ya majadiliano ya muda mrefu na uchambuzi wa kina uliofanywa na madiwani katika kikao hicho kuhusu taarifa hiyo, waliamua hatua stahili zinazofaa kuchukuliwa dhidi ya watumishi waliozembea ni kuwasimamisha kazi.

  Kabla ya kufikiwa kwa uamuzi huo, Baraza lilikaa kama Kamati ambapo watumishi, waandishi wa habari na wananchi walioalikwa walitakiwa kutoka nje.

  Baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Justine Sheka aliwaita watu wote waliotakiwa kutoka nje ya ukumbi, ili kupisha mjadala wa kuwajadili watumishi wanaotuhumiwa kuhusika na upotevu au wizi wa fedha hizo kurudi ndani.

  Sheka aliwataja majina waliosimamishwa kazi kuwa ni Mhandisi Leonard Mashamba, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Alex Kapula, Mweka Hazina, Muhidini Mohamed; Ofisa Kilimo na Mifugo Wilaya (DALDO), Kadigi Herman, Mtunza Fedha, Mussa Limbe, Mhasibu Boniphace Nkumingi, Ofisa Ugavi, Medison Matalana na Ofisa Ugavi Msaidizi, Elias Simiyu.

  Wengine ni Mratibu wa Mradi wa Global Fund, Edwin Nzela, Mhasibu Mussa Kilulya, Mratibu wa Mradi wa Ukimwi, Leonard Koyo, Fundi Sanifu wa Idara ya Maji, Grashan Mumba na Mratibu wa Mradi wa Kilimo wa Wilaya (DASIP), Sara Pula.

  Mwenyekiti huyo wa Halmashauri alisema, kusimamishwa kazi kwa baadhi ya wakuu wa idara na vitengo kuna lengo la kupisha uchunguzi unaoendelea kufanyika hivi sasa kutokana na taarifa hiyo ya CAG.

  Mbali na Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni Diwani wa kata hiyo, Amos Sagara, Diwani wa kata jirani ya Nyamaraga, Antony Manga, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Nyangoko Paulo na maofisa watendaji wa kijiji na kata hiyo pamoja na wakazi zaidi ya 800 walihudhuria mkutano
   
 2. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimewakubali madiwani wa CCM!
   
 3. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kama hayo mmeyachukulia hatua mnstahiri pongezi
   
 4. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  kwa anayejua juu ya sheria na kanuni iliyowapa mamlaka madiwani ya kuwasimamisha watumishi hao naomba atuongoze kwa majadala huu, kwani tunawe mwisho wa siku tukasikia wanalipwa kwa usumbufu na hatimaye kuingiza halmashauri yetu kwenye tatizo
   
 5. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mfano wa kuigwa
  OTIS
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  lakini si mfano wa kupigiwa mstari!!!!!
   
Loading...