Mr Antidote
JF-Expert Member
- Jan 11, 2015
- 953
- 1,303
Habari zenu wadau
Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kushukuru Mungu kwa afya na pumzi tuvutayo bila malipo.
Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Nimefanya uchunguzi binafsi nikagundua watz wengi tumekua na katabia fulani ka ufisadi. Achana na wanasiasa ambao ni mafisadi papa na tuangalie kundi mojamoja .
Waalimu:
Hawa ni moja mafisadi ambao walijificha kwenye muavuli wa tuition na michango midogo midogo ambayo ilikua ikiwaumiza sana watz wa hali ya chini.
Mafundi:
Hawa ufisadi wao umejificha katika wizi wa vifaa vya ujenzi kama vile cement nk
Makanisa:
Hapa ufisadi umejificha katika jina la kumtolea Mungu kupitia sadaka, fungu la kumi, zaka, mavuno n.k. Hawa hufanikiwa zaidi kwa kuwa wanatumia maandiko vibaya kuwapa waamini wao maneno malaini ya kuwafanya watoe ili wafaidike wao.
Abiria:
Hapa nazungumzia watumiaji wa daladala hawa wako tayari kushuka bila kulipa nauli endapo konda akijisahau. Wengine hijikausha kabisaa wakati wakidaiwa nauli.
wadau makundi yapo mengi sana hatutaweza kuyamaliza yote. Lakini jambo la msingi hapa ni kujitathimini sisi wenyewe mmoja mmoja. Je mimi si fisadi? Au unamuonyeshea kidole rostam, lowassa nk. Je wewe ungepata nafasi kama yao ungeweza kuresist hiyo dili?
Take back time nilipokua nakua i remember i used to be ka-little fisadi. Nakumbuka i used kupandisha bei vitu kwa mama nlipokua nikitumwa sokoni ili nipate japo 200 ya kutumia, je hivi sio vielement vya ufisadi? Wangapi tumefaanya hizi mambo utotoni?
Hitimisho:
Vita ya ufisadi inaanza na mmoja mmoja kwa kutambua kwamba hiki ninachofanya si kitu sahihi, NO MATTER HOW LIFE IS GETTING HARDER manake hicho ndio kisingizio kikubwa cha ufisadi wa watz wengi.
Wasalaam