Ufisadi BoT: CCM matatani

Ufisadi BoT: CCM matatani

Mlalila

Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
35
Reaction score
17
Historia ni mhimu kujua umetoka wapi, uko wapi na wapi unaelekea.


CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake vi mtegoni, na itabidi kuamua kusuka ama kunyoa kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba fedha zilizochukuliwa kutoka Benki Kuu (BoT) chini ya Mpango wa Ununuzi Madeni (EPA), ziliingizwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, uliokipa chama hicho ushindi wa kishindo, Raia Mwema imedokezwa.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimeiambia Raia Mwema kwamba kiasi cha Shilingi bilioni 40 kilichochukuliwa na kampuni ya Kagoda Agricultural Limited (KAL) ili zikafanye kile kinachoelezwa kuwa ni kazi "nyeti za usalama wa nchi" sehemu yake iliingizwa katika uchaguzi.
Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na Raia Mwema, wamesema kwamba wana taarifa kwamba baadhi yao walipata "msaada" ili kufanikisha uchaguzi wao majimboni japo kwamba "msaada" huo ulitofautiana kati ya mbunge na mwingine, kulingana na mhusika ni nani.

Endelea!!!!!!!

Mwaka 2005 tulijipanga na tulikuwa na kamati mbalimbali ndani ya chama kama za Uchaguzi, Fedha, Vifaa na pia kuna wanachama na mashabiki wetu walijitolea kuchangia vitu kama kofia na fulana, kwa hiyo suala la chama kujitosheleza lingewezekana kabisa," alisema Mangula.

Vyanzo vya habari vilivyozungumza na Raia Mwema vinasema kwamba kujitokeza kwa vigogo hao wa CCM kuzungumzia suala lilelile, kwa wakati uleule, ni ishara kwamba hilo si jambo la kupuuza, na kama CCM haitacheza karata zake vizuri, litaibukia kuwa kashfa kubwa kwa chama hicho na Serikali kwa ujumla.

"Wako (CCM) katika harakati za kujaribu kufunika mambo. Wanazima moto. Na inaelekea hata nyinyi wenye vyombo vya habari mnataka suala hili liishe hivi hivi. Lakini hili si jambo la kumalizika hivyo. Mwaka 2010 kutakuwa na uchaguzi hapa. Mkiliacha yatajirudia hayahaya na huenda wengine wakachota tena BoT," anasema mmoja wa vyanzo hivyo.

Vyanzo vya Habari pia vimeliambia Raia Mwema kwamba Kagoda Agriculture Company ilianzishwa kwa maelekezo ya Rais Benjamin Mkapa, na kwamba sababu za "usalama wa taifa" zilizotumiwa kuhalalisha kuchukuliwa kwa pesa hizo ndizo alizoambiwa Ballali na ndizo pia alizomwambia Meghji.

Aidha, nyaraka za kuuziana deni kati ya BoT na Kagoda zilisainiwa katika ofisi ya mwanasheria mmoja wa Dar es Salaam na katika kusaini huko, kulikuwa na Ofisa wa BoT na mmoja wa viongozi wa fedha katika kamati ya kampeni ya CCM. Raia Mwema limeonyeshwa na mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi huo wa BoT nakala ya hundi ya malipo kwa Katibu Mkuu wa CCM.


Chanzo:Raia Mwema - Ufisadi BoT: CCM matatani
 
Hili twalijua, hadi Serial killer chemba la choo anahusikaa
 
Hill jambo siyo jipya na linajulikana A to Z. Wasubiri mahakama na kutaifishwa mapema 2016.
 
Walivuta wote Min. milioni 5.

Rostam Azziz ana daftari alilowasainisha Wabunge wote hata hao SAFI mnaowaita JEMBE kutoka CCM.
 
Aise tumetoka mbali sana usafi wa ccm ambayo inapiganiwa na hawa wakila Mchemba ana Nape
 
Mtindo huo hautakwisha na ndo kikwazo cha maendeleo ya nchi hii.

Bajeti ya nchi hii ni bajeti ya kuendesha serikali mbili. CCM na serikali yenyewe tunayoonyeshwa. Yaonekana takribani nusu ya bajeti ya nchi inaingizwa CCM kinyemela pamoja na mifuko binafsi ya wanaohusika kuzihamisha. Kila wizara inaishia kupata sehemu ndogo ya bajeti iliyopitishwa bungeni.

Mtindo huo unaongeza ufisadi. Pesa zinapelekwa kinyemela CCM na hata matumizi yake yanakuwa ni ya kinyemela. ndo pesa zinazotumiwa vibaya kabisa na viongozi wa CCM na serikali. Majengo yote unayoyaona yakiinuka mijini hayatokani na biashara halali iliyolipiwa kodi. Ni pesa ya serikali inayovuja.

Iko siku tutaomba historia ya ulipaji kodi wa wahusika.

Nimefika pale Morogoro na kukuta mzee Makamba akisimamia ujenzi wa hoteli yake na ukiangalia ujenzi wenyewe ni kama wa mtu aliyeokota pochi lenye pesa, hahitaji mpangilio.
 
Mbona hilo jambo linajulikana n'a kila m-TZ n'a ndiyo kisa ya kutoroshwa Balali n'a baadaye tukatangaziwa kuwa amekufa wakati bado anadunda!! Kisa cha magamba kumtorosha ni kuwa yeye ndiye aliyekuwa shahidi muhimu sana wa skzndali hiyo ya EPA n'a angeamua kuweka mambo hadharani, basi hivi sasa CCM ingekuwa tu imesalia katika vitabu vyà historia kuwa katika kipindi fulani chama hicho ndicho kilikuwa ndiyo chama tawala cha nchi ya TZ!!!!
 
Afadhali ufisadi wa kuiba fedha (nasema kwa namna ya kifisadi) kuliko wa 'SUTI' jamani! Hivi nchi hii ni kama sote tumerogwa! Viongozi wetu wamekuwa vipofu, viziwi na wenye kiburi cha madaraka kuliko hata mobutu! Halafu mijadala kama hiyo mama makinda haitaki maana amewekwa hapo kwa maslahi ya chama siyo ya taifa. KAGODA, MEREMETA, RICHMOND, KASHFA YA RADA, MENO YA TEMBO, MIKATABA MIBOVU, AJIRA ZA UPENDELEO KWENYE TAASISI NYETI,......Haya! kifo Daudi Balali ndiyo funga kazi! CCM kiboko kwa uhalifu. Lakini hadi lini? Pale mtz atakapoacha kusikiliza ujinga wa mtu kama Mwigulu ambaye kazi kubwa siyo kujenga hoja bali kununua na kurubuni wanachama wa chama cha cdm wakati hao wanajiunga kwa hiari baada ya kuona kazi nzuri ya chama husika. BADO KITAMBO KIDOGO MABADILIKO YA KWELI YATATOKEA na ccm watashangaa kuona waliyemuita msaliti anaingia ikulu, kama wanabisha wakamuulize Dr salmin Amour a.k.a KOMANDOO dhidi ya kina maalim na kundi lake. Ukweli ni kwamba huwezi kuzuia mabadiliko wakati unapokuwa umetimia. PEOPLEEEEES...aluta continua
 
Ufisadi BoT: CCM matatani
Waandishi Wetu

Toleo la 013
23 Jan 2008.
habari hii ya mwaka 2008,mleta mada anatoa hapa leo.(mpaka wanaotoa taarifa wanatabiri uchaguzi wa 2010 ambao kimsingi ulishapita) lakini mleta mada analeta kama habari ya jana.haya bana!
 
Back
Top Bottom