Ufisadi bodi ya kahawa moshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi bodi ya kahawa moshi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ngoshwe, Nov 11, 2009.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  UFISADI BODI YA KAHAWA MOSHI  Wana JF, hii ni taarifa iliyotumwa na Mwanajamii mwenzetu kupitia mtandao binafsi, kama kuna mmoja wetu anawea kufuatilia na kutupa ukweli wa habari hii, tafadhali ashughulikie na kuyaweka hewani yatakayojitokeza kwa manufaa ya nchi yetu, Naileta kwenu taarifa hii kama ilivyopokelewa:  “Kwenye gazeti la Mwanachi la tarehe 16 Apili 2008 iliandika habari ya kusikitisha kuhusu kupigwa mnada kwa jengo la kahawa lillopo Moshi linalomilikiwa na Bodi ya Kahawa (TCB) kutokana na deni la Tshs. 700 milioni inayodaiwa na Benki ya Exim.
  Tafadhali tunaomba vyombo vya habari vifuatilie suala hili kwa kina ili kujua:- (i) ni kampuni gani iliyodhaminiwa huo mkopo na Bodi ya Kahawa ambayo ni chombo cha umma kinachotegemea bajeti ya seriklai kwa asilimia mia moja na hakiruhusiwi kufanya biashara (i) wamiliki wa kampuni iliyochukua mkopo ni akina nani, na wana mahusinano gani na Bodi mpaka iwadhamini mkpo mkubwa kiasi hiki (iii) nani aliidhinisha Bodi itoe jengo la wakulima la thamani ya mamilioni kudhamini mkopo ambao maslahi yake kwa wakulima hayajulikani (iv) Bodi/wakulima wa kahawa wamenufaikaje na mkopo uliotolewa na Benki ya Exim kwa kampuni iliyodhaminiwa (v) Mkataba unasemaje na nani aliyesaini mkataba huo na kwa idhini ya nani………..????, Je serikali ilikuwa inajua haya mapema??/
  Inasikitisha sana kuona viongozi wa nchi hii hasivyokuwa makini na umaskini wa watu wao, inaumiza sana, mtu anapewa dhamana na anaitumia kwa maslahi yake binafsi na familia yake!!!!. Tafadhali tunaomba suala hili lichunguzwa kwa makini. Kuna taarifa za kuthibitika kuwa jengo hilo liliwekwa dhamana na iliyokuwa menejimenti ya Bodi ya kahawa kinyemela na hakuna faidia yeyote kwa Bodi hiyo kutokana na Mkopo uliochukuliwa toka Exim Benki. Taarifa zilizopo ni kuwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye sisi tunajua kuwa muda wake wa utumishi ulikwisha malizika akaongezewa tena pasipo ufanisi, aliliweka rehani jengo hilo kwa manufaa binafsi ili ajipatie kiasi cha Tshs. 300 milioni kwa ajili ya Kampuni yake inayoitwa African Consulting Group Limited . Hati ya umiliki wa jengo hilo ni No. 4757 LRM lilopo plot Na 52, Manispaa ya Moshi (taarifa zaidi zinajulikana na Mkurugenzi Mkuu huyo aliye maliza muda wake na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim). Mkurugenzi huyo (jina tunalo) ni mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyoliweka jengo hilo rehani na akiwa mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa alitumia nafasi hiyo na inadaiwa pasipo idhini ya Bodi ya Wakurugenzi wala Serikali (Wizara Kilimo) aliweka rehani jengo ilihali akijua kuwa Bodi ya Kahawa kama chombo cha umma haina maslahi yoyote na mkopo uliochukuliwa toka Benki ya Exim Benki na kampuni yake ambayo taarifa tulizonazo ina milikiwa na watu wanne wengine wawili wanajulikana kwa jina moja tu la Mtani.inasadikika mmoja ni marehemu...
  Inasikitisha sana kusema kuwa inawezekana mchezo uliotumika kuliweka jengo hilo rehani hautofautiani na “ufisadi”, kwani japo kuwa jengo hili linamilikiwa na Bodi ya Kahawa na lilijengwa kwa michango ya wadau wa kahawa kiiwemo chama kikuu cha wakulima wa kahawa Mkoani Kilimanjaro, (KNCU), wahusika hawakufahamishwa na pia hata Benki ya Exim ilikubali kuingia kwenye “ufisadi” huu pasipo kuwepo kwa ridhaa ya Bodi ya wakurugenzi wala Serikali. Ikumbukwe kuwa Exim Benki iliwahi kuhusika siku za nyuma na kushindwa kulipa deni la Mfuko wa Pembejeo wa Taifa na sijui mpaka sasa kama wameshalipa!.
  Tunazo taarifa kuwa usajili wa rehani ilifanyika kwa msajili wa ardhi kwa jina la mkopo uliochukuliwa na kampuni ya African Consulting Group Limited . inayomilikiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi na yeye ndie aliyewasilisha maombi ya Mkopo Benki, alisaini Mkataba wa Mkopo na wakati huo huo kusaini Hati ya Rehani kwa nafasi ya Mkurugenzi wa Bodi ya Kahaw, kudhamini mkopo uliochukuliwa na kampuni yake binafsi!!!!. Ni wazi kuwa Benki ya Exim(T)Limited ilikuwa inafahamu mchezo uliokuwa ukiendelea kwenye suala hili na kwa nia ya kujinufaisha kwa jasho letu wanyonge ikafumba macho. Hii Benki ya Exim inauzalendo kweli japo kuwa inajifanya kuwasaidia wakulima???????...
  Ili kunusulu jengo letu sisi maskini, tunaomba sana suala hili lichunguzwe kwa kina kujua ukweli kuhusu ufisadi uliofanyika na ikiwezekana kuwachukulia hatua wahusika. tunatumaini ukweli utajulikana haraka toka ndani ya Bodi ya Kahawa hususan Mwenyekiti wa Bodi, Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo, na aliyekuwa Mkuruhgenzi Mkuu wa Bodi, Wizara ya Ardhi, ofsi za Moshi ambapo Mkataba wa Rehani (Mortgage) ulisajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi, Menejimenti ya Exim Bank pamoja na Chama cha Ushirika cha wakulima wa Kahawa Mkoani Kilimanjaro, (KNCU). Kwa ufisadi huu Tanzania tunakwenda wapi!”

   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ?

  Thu 13 Jan 10:15PM

  ?

  *?
  Mkurugenzi mkuu TCB aendelea kusota gerezani

  Tuesday, 26 October 2010 20:06

  ?Mwandishi Wetu
  MKURUGENZI mkuu wa zamani wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Leslie Omari anaendelea kusota mahabusu Gereza la Karanga baada ya kushindwa kutimiza mashari ya dhamana kwa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili.

  Mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo, Shaddy Kyambile, ambaye alikuwa mkurugenzi wa fedha wa TCB, alitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa baada ya kusota gerezani kwa takriban saa 20.

  Masharti yaliyowekwa na mahakama ni pamoja na kila mshitakiwa kuweka mahakamani fedha taslimu Sh75 milioni na kuwa na wadhamini wawili watakaowasilisha mahakamani hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh45 milioni.

  Jengo la 'Kahawa House' lililokuwa likimilikiwa na Bodi ya kahawa Moshi (TCB)

  Wakili Godwin Sandi, ambaye anayemtetea Kyambile, aliithibitishia Mwananchi kuwa mteja wake aliachiwa jana saa 6:00 mchana baada ya ndugu na marafiki zake kukusanya nguvu ya pamoja na kutimiza masharti ya dhamana.

  Wakurugenzi hao wanatuhumiwa kuiwezesha kampuni ya African Consulting Group Limited (ACGL) kutumia hati ya kiwanja cha jengo la umma la Kahawa House kama dhamana na kukopa Sh330 milioni kutoka benki ya Exim.

  Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa Kilimanjaro, Simon Kobelo aliwataka washitakiwa hao kutimiza masharti hayo ya dhamana wakati wakisubiri kutolewa kwa uamuzi mdogo kuhusu ubishani wa kisheria.

  Wakili Sandi aliwasilisha hoja akidai kuwa kifungu cha sheria ya uhujumu uchumi namba 36 (4) (e) kinachotaka mshitakiwa kukabidhi mahakamani nusu ya kiasi cha fedha anachotuhumiwa kilishafutwa kwa kuwa kinakiuka katiba.

  Alifafanua kuwa Oktoba 4 mwaka huu, Mahakama Kuu ilitamka kuwa kifungu hicho kinakiuka katiba kwa kuwa kinawabagua watuhumiwa wasio na uwezo na kuipa serikali mwaka mmoja kukifanyia marekebisho.
  Kwa mujibu wa Sandi, katika kipindi hiki cha mpito cha kusubiri kufutwa kwa kifungu hicho, mahakama imepewa uwezo chini ya kifungu namba 148 (5) (e) kuweka masharti ya dhamana ya ama fedha taslimu au mali isiyohamishika.

  Mahakama itatoa uamuzi huo mdogo Ijumaa dhidi ya hoja za Wakili Sandi.

  Katika mashitaka hayo, mwendesha mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Maghela Ndimbo alidai kuwa mwaka 2003, washitakiwa ambao hawakuwepo kortini walikula njama ya kutenda kosa.

  Mwendesha mashitaka huyo aliendelea kudai kuwa mwaka huo, washitakiwa wakiwa waajiriwa wa TCB, walitumia vibaya madaraka yao kwa kuipa ACGL hati ya kiwanja cha Jengo la Kahawa ili iitumie kukopa fedha.

  Baadaye kampuni hiyo ilishindwa kurejesha mkopo huo baada ya mkurugenzi wake kufariki dunia, hali iliyoilazimu benki ya Exim kuamua kuuza jengo hilo, lakini serikali ikaingilia kati kuzuia na ndipo Takukuru walipolivalia njuga.
   
Loading...