Ufisadi Ardhi

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
eti serikali inatafuta bilioni 3 kukomboa shamba ililoliuza kwa milioni 600 ? upuuzi gani huu serikali inafanya, kwa mtaji huu hata sidhani kama viongozi wa nchi hii walistahili hata kuongoza vijiji maana wanaingizwa mjini kwa utapeli wa kama wa karata. Eti mwekezaji alinunua shamba milioni 600 akaenda Kenya akakopa bilioni 3 sasa ameshindwa kulipa hivyo serikali inatafuta bilioni 3 ikakomboe shamba kuwapa vijiji 10 vinavyozunguka hilo shamba. Huu ni utapeli wa wazi hizo bilioni 3 zitumike kuhamisha baadhi ya vijiji ili vibaki vichache vilime ardhi waliyonayo kama wanaweza kuuza hilo shamba wakapata bilioni 3 wauze ilimradi sharia za nchi zifuatwe na masharti aliyopewa mwekezaji wakati wa kuuziwa shamba yakikiukwa litaifishwe lakini hatuwezi kuingizwa mjini kwa utapeli wa kijanja. Ela hii ikilipwa jamani watanzania hii itakuwa biashara nzuri tunanunua mashamba kutoka serikalini kwa bei ndogo tunachukua mikopo nje tunaweka mifukoni, wanakuja kuuza shamba serikali inalipa mkopo. taasisi iliyokopa ina mali kwa nini isilipe kwa kutumia mali zake na bado inaendesha utapeli waziwazi maana mtu anajisema ana nguvu za mungu kusaidia watu wengine kuwaombea wakikutana na matatizo ya kiuchumi sasa imekuwaje wakashindwa kulipa.
 
Back
Top Bottom