Ufaulu wa Masomo ya sekondary na Mafanikio vyuoni na Makazini

Bagabuje

Member
Apr 22, 2017
28
15
Zoezi la ufukuzaji wa wafanyakazi wenye vyeti feki vya secondary imenifanya nitafakari na kuona nibora nipate mawazo yenu wadau kuhusu jambo hili.

Kinacho nishangaza hasa ni ukweli kuwa watu hawa walipata sifuri katika masomo ya sekondari lakini waka ghushi ama kununua alama za ufaulu ambazo sio zao na kuingia vyuoni wakafanya vizuri na kupata Ajira na hatimaye kuwa wafanyakazi mahili na tegemeo katika vitengo vyao kuliko wale waliopata ufaulu wa juu Sekondari Jambo hili ninanifanya nijiulize.

Kuna sababu gani upoteze muda wako kusoma hadi Kidato cha sita wakati hata kidato cha nne aliyepata daraja sufuri anaweza kufanya vizuri chuo kikuu?

Kuna uhalali gani wa kuwanyima watu wanaosemekana kufeli shule za sekondari kujiunga na elimu ya juu wakati watu waliokutwa na vyeti vya kughushi wame tuthibitishia kuwa, kumudu masomo ya elimu ya juu (chuo) si lazima uwe umepata ufaulu wa juu Sekondari?

Mfano mzuri ni Bwana BASHITE pamoja na kusemekana kuwa vyeti si vyake lakini utendaji wake ni wakiwango cha juu sana kuwapita watu waliopata daraja la kwanza sekondari

Sitaki kuamini kuwa watu wote hao walifanikiwa kumaliza masomo yao ya vyuo kwa ujanja ujanja(Rushwa), maana kama ingekuwa hivyo wasinge mudu majukumu yao ya kazi na wangekuwa wamesha fukuzwa kazi kabla ya KUTUMBULIWA.

Acha waondolewe japo inauma.
Kwa sasa tanzania inawatu sahihi Wengi wenye kujaza hizo nafasi kiasi kwamba hata Kuna mtu ameenda chuo na hawezi kudeliver expected results Kuna wenye sifa zaidi ya wanne wenye Uwezo wa kudeliver.
Kwa sasa binafsi sioni sababu ya kutetea vitu visivyosahihi
 
Waache watumbuliwe, watanzania tuache kupenda njia za mikato...Mafanikio hayaji kwa short cuts.
 
Back
Top Bottom