UFAULU HAUJI KWA MANENO NA VITISHO

Jimmy George

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,733
1,643
Habari wadau wa elimu

Inasemekana kuwa malengo ya serikali(TAMISEMI) Mwaka huu ni kuwa ufaulu darasa la saba uwe asilimia 82 na ufaulu darasa la nne uwe ni asilimia 100. Sikatai ni mipango mizuri na ina lengo la kuinua elimu yetu.

Ila najiuliza wakati wanajaza OPRAS zao kwenye malengo(shabaha) ya utekelezaji waliangalia changamoto zilizopo? Maana ninachoona mm malengo walioyaweka ni KUWATISHIA NGAZI ZA CHINI hakuna shabaha walizoweka kufanikisha haya. Mambo yafuatayo yako vile vile watawezaje kufikia malengo hayo?:
1.Shule nyingi zina upungufu wa walimu(nyingi zina walimu 7)
2. Fedha za captation ni ndogo kuwafanya walimu waweze kuchapa mitihani ya majaribio mara kwa mara(fedha zenyewe bado zipangiwe matumizi,mara michezo,mara kulipia walimu chakula na usafiri waendapo vikao na semina za wakuu wao n.k)
3. Idadi kubwa ya wanafunzi inayosababisha walimu kushindwa kufanya upimaji wa kina
4. Watoto kuishi mbali na shule kufika wamechelewa na wengi wao kuwa watoro kushindwa kuhudhuria masomo ipasavyo na wengi wa wanaokaa mbali ndiyo hushusa ufaulu(suluhisho limetolewa watoto wale shule lakini si jamii zote Tz zina mwamko wa elimu na kuchangia chakula)
5. Maagizo na vikao vingi kiasi cha kufanya muda wa mwalimu kufundisha uwe mdogo na muda mwingi kutekeleza wanayopewa(mfano kutoa takwimu fulani,vikao vya hapa na pale n.k).
6. Mazingira duni ya walimu kufanya wawe na ari ya kufundisha(mazingira mabaya,ukosefu wa vifaa,kukosa ushirikiano wa jamii zisizothamini elimu)
7. Kauli za vitisho za viongozi zinazofanya walimu wafanye kazi kwa uoga na kupelekea wengine kuchakachua,kuwalazimisha walimu kufundisha masaa ya ziada(mfano wa kauli "utafukuzwa kazi endapo hutafanya haya na yale")
8. Na nyingine nyingi zinazojulikana

SERIKALI IPUNGUZE CHANGAMOTO ZILIZOPO NA NDIPO WAJE NA MALENGO YANAYOTEKELEZEKA(na nashauri wakiwa wanaweka malengo wawe wanatumia shule zenye changamoto nyingi kuwekea malengo yao na si shule za mjini zenye changamoto chache)
 
Back
Top Bottom