uzio usio onekana
JF-Expert Member
- Apr 21, 2019
- 889
- 2,806
Mafuta yawe kama uji? Unaijua nchi yenye stock kubwa kabisa ya mafuta?View attachment 1641532
Mm naona mwisho wa ugaidi ni teknolojia. na kwasababu nchi za kiarabu ndio zinazo fadhili ugaidi na
Jeuri yao yote ni mafuta dawa ni kugundua chanza kingine cha nishati. ili mafuta yasiwe na thamani yawe kama maji tu . Na huo ndio utakakuwa ndio mwisho wa ugaidi. Na tutakuja kuona waarabu pamoja na uvivu wao wote watakuja kufanya kazi gani.
Mafuta yawe kama uji? Unaijua nchi yenye stock kubwa kabisa ya mafuta?
Kwahiyo Ufaransa anajitekenya na kucheka sio?Ugaidi ni miradi ya haohao Westerners. Wanaiandaa, wanaifadhili na wanailinda. Kwa technology ilivtofikia kwa sasa duniani kama magaidi wangekua hawatakiwi wangeshafutiliwa mbali. Lakini jamaa lazima watengeneze adui bandia na wamlinde asiondoke ili watimize malengo yao ovu
Bahati mbaya sana inatengenezwa kwa namna ya kukuaminisha wewe uone huo ugaidi unatoka sehemu nyingine na sio kwao wenyeweKwahiyo Ufaransa anajitekenya na kucheka sio?
Yaani anajitumia magaidi wa kuua raia wake sio?
Dah inachekesha na inasikitisha sana Yani kwamfano Osama alilipua majengo marefu na ya muhimu zaidi marekani na kuua maelfu ya raia lakini bado wavaa vipedo wa kwa mtogole wanasema Osama alitumwa na marekani kulipua marekani.
HHahHa imebidi nichekeBahati mbaya sana inatengenezwa kwa namna ya kukuaminisha wewe uone huo ugaidi unatoka sehemu nyingine na sio kwao wenyewe
Nasisitiza tena wale wakaa milimani wa Kandahar na Kundus kule Afghan hawana uwezo wa kiteknolojia, intelijensia wala ufundi wa kuingia ndani ya Marekani, wakapita vizuizi vyote vya usalama, wakateka ndege zaidi ya moja za abiria, wakaruka juu ya anga la Marekani kwa muda wa karibia saa nzima eti wasionekane kwenye rada na hatimaye wazielekeze kwenda kugonga WTC na Pentagon. Kama kuna anayeamini Waafghanistan ndio walifanya hayo basi hakuna wa kumkomboa kwe ye utumwa huo wa fikra na akili