kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,190
- 24,620
Kukiri Rais wa Ufaransa juu ya kufikia tamati ubeberu wa Magharibi duniani
Aug 29, 2019 04:51 UTC
Kwa karne kadhaa Wamagharibi wametekeleza ubeberu katika uga wa kimataifa iwe ni katika kipindi cha ukoloni au katika zama za ubeberu; daima walifanya unyonyaji dhidi ya wananchi na mataifa mengine ya dunia.
Katika kipindi cha vita baridi 'cold war' na baada ya kipindi hicho, Marekani ikiwa kinara wa Magharibi imefanya juhudi kubwa kueneza hegemonia na mamlaka yake ulimwenguni. Pamoja na hayo, hali ya mambo duniani pamoja na mfumo wa kimataifa umepata mabadiliko makubwa ya kimsingi na filihali, viongozi wa Magharibi wanakiri kwa vinywa vyao juu ya kufikia tamati zama za ubeberu wa Magharibi duniani.
Rais Emmanue Macron wa Ufaransa alikiri Jumanne katika hotuba yake katika Ikulu ya Rais ya Elysee kwamba, kipindi cha ubeberu wa nchi za Magharibi duniani kimefikia tamati. Rais wa Ufaransa alisema bayana kwamba, hivi sasa tunaishi katika kipindi cha kufikia tamati ubeberu wa Magharibi duniani; na jambo hili linatokana na makosa yaliyofanywa na Wamagharibi huko nyuma.
Rais Macron aliyekuwa akihutubia hadhara ya mabalozi wa nchi mbalimbali amesema kuwa, ulimwengu unashuhudia kuchomoza nguvu mpya ambazo kwa muda mrefu tumekuwa tukipuuza taathira zake. Rais Macron amesema hayo katika mkutano wa 'Kukabiliana na Changamoto za Dunia; Majukumu ya Ufaransa na Ulaya' uliofanyika kwa ubunifu wa Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa.
Rais Macron ameeleza kwamba, matukio ya hivi karibuni ulimwenguni bila shaka nayo yamekuwa na taathira kwa mfumo wa kisiasa ulimwenguni. Kukiri Rais wa Ufaransa juu ya kumalizika nguvu ya Magharibi kumefanyika kwa kuzingatia ukweli halisi wa mambo na usioweza kufichika katika uga wa kimataifa. Katika kipindi cha baada ya vita baridi, licha ya Marekani kufanya juhudi za kulinda mfumo wa kambi moja, lakini mwenendo wa dunia katika nyuga mbalimbali ulipelekea kudhihiri nguvu za kiuchumi, kisiasa na kijeshi katika uga wa kimataifa.
Hivi sasa ulimwengu wa Magharibi kinara wake akiwa Marekani unakabiliwa na ushindani mwingine kama China na Russia. China ambayo kwa sasa ni nguvu ya pili ya uchumi duniani baada ya Marekani, kwa mujibu wa utabiri uliofanywa hadi kufikia mwaka 2030 nchi hiyo itakuwa nguvu ya kwanza kubwa kwa uchumi ulimwenguni. Hili ni jambo ambalo linaufanya udhibiti wa kiuchumi na kibiashara wa Magharibi hususan Marekani utiliwe alama ya swali.
Russia nayo baada ya kipindi fulani cha kusambaratika katika muongo wa 90, kuanzia mwaka 2000 baada ya kuingia madarakani Rais Vladimir Putin, ilianza mwenendo wa ukarabati na kuhuisha nguvu yake na hivi sasa inahesabiwa kuwa mshindani mkuu wa kisiasa na kijeshi wa madola ya Magharibi hususan Marekani si barani Ulaya tu bali hata katika Asia Magharibi na Amerika ya Latini.
Licha ya Marekani kufanya bidii kubwa ya kuwa na nafasi kubwa na ya juu kuliko mataifa yote, lakini nguvu ya Washington kwa sasa inakabiliwa na changamoto katika nyuga mbalimbali za kimataifa na hivi sasa makundi na jumuiya mpya za kieneo na kimataifa kama Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai (SCO) na Kundi la Brix mkabala na Kundi la G7 linaloundwa na madola saba makubwa ya viwanda duniani zimeibuka na kuwa na nafasi kubwa.
Warusi wanaamini kwamba, kuna mjadala ambao si mpya sana baina ya madola ya Magharibi na nguvu nyingine hasimu katika uga wa kimataifa ambao upo katika hali ya kutokea. Russia na China zinaamini kwamba, matukio ya kimataifa na uhalisia wa mfumo wa dunia unaunga mkono nadharia hii kwamba, hivi sasa ulimwengu unaelekea upande wa kambi kadhaa. Hii ni katika hali ambayo, Marekani ikiwa kinara wa Magharibi inang'ang'ania kubakishwa mfumo wa kambi moja na imekuwa ikifanya juhudi za kujionyesha kwamba, yenyewe ni polisi wa dunia ikifuatilia malengo na matakwa yake kupitia uchukuaji hatua wa upande mmoja.
Ukweli wa mambo ni kuwa, Marekani inapinga vikali suala la kuimarishwa mitazamo ya pande kadhaa na imekuwa ikifanya juhudi ili kuhakikisha kwamba, mamlaka yake yanaendelea kutawala katika uga wa kimataifa na ikitumia mabavu iweze kuzitisha nchi nyingine matakwa yake.
Pamoja na hayo, ushahidi unaonyesha kuwa, Marekani imeendelea kutengwa siku baada ya siku kutokana na uchukuaji maamuzi na hatua za upande mmoja na za kibabe za Rais wa sasa wa nchi hiyo Donald Trump.
Tags
RUSSIA MAREKANI CHINA
MAGHARIBI