Ufaransa kuongeza Ufadhili zaidi Tanzania

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,495
PICHA-11-620x308.jpg

SHIRIKA la Maendeleo la Ufaransa (AFD) limeeleza kuwa, lina mpango wa kuongeza kiwango cha fedha za maendeleo ifikapo mwakani.

Emmanuel Baudran, Mwakilishi wa AFD nchini Tanzania ametoa kauli hiyo leo wakati alifanya mazungumzo na Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini alipokwanda kumtembelea.
Baudran ameeleza fedha ambazo zimetolewa kupitia mkopo wenye masharti nafuu zimeelekezwa katika Sekta za Maji, Nishati na Miundombinu ya usafirishaji.

Amesema mwakani shirika hilo limepanga kuongeza kiasi cha fedha kutoka Euro milioni 50 hadi Euro milioni 100 kwa mwaka kupitia mikopo ya masharti nafuu huku kipaumbele kikiwa ni sekta hizo za nishati, maji na miundombinu ya usafirishaji.

Akizunguza na Prof. Muhongo pia watumishi wengine wa wizara hiyo Baudran amesema, Tanzania ni moja ya nchi zinazopewa kipaumbele na shirika hilo.
Amesema, katika miezi ijayo AFD itajikita katika utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa Gridi ya Umeme ya Taifa, uboreshaji wa vituo 10 vya kupooza umeme pamoja na ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji umeme kutoka Geita mpaka Nyakanazi (220 KV).

Huu ni mpango wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kupanua Gridi ya Taifa kwa upande wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambapo itaunganisha Mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma.
Prof. Muhongo amelishukuru shirika hilo kwa ushirikiano wanaouonesha katika kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme nchini.

Amesema, juhudi hizo zitasaidia kutimiza lengo la serikali la kuwa na umeme wa kutosha na wa bei nafuu ambao utasaidia kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali.

Source: Mwanahalisi
 
Swala ni vipi tutazilipa! Mwaafrica bado anaamini msaada wa mzungu ndio kutoka kwenye umaskini.
Umaskini wetu utatoweka kama mwafrica akiacha ndoto za alinacha kuwa mzungu ndio jawabu ya matatizo yetu;muda mwingine tujiangalie wenyewe
 
Mkuu hakuna nchi isiyokopa duniani.
Hata mmarekani anakopa pamoja kuwa ni tajiri wa kufa mtu, mchina pamoja na kuwa anawakopesha wengine lakini na yeye pia anakopa.

Tatizo sio kukopa, tatizo ni tunakopa ili tuzalishe?? au ili tule??
 
PICHA-11-620x308.jpg

SHIRIKA la Maendeleo la Ufaransa (AFD) limeeleza kuwa, lina mpango wa kuongeza kiwango cha fedha za maendeleo ifikapo mwakani.

Emmanuel Baudran, Mwakilishi wa AFD nchini Tanzania ametoa kauli hiyo leo wakati alifanya mazungumzo na Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini alipokwanda kumtembelea.
Baudran ameeleza fedha ambazo zimetolewa kupitia mkopo wenye masharti nafuu zimeelekezwa katika Sekta za Maji, Nishati na Miundombinu ya usafirishaji.

Amesema mwakani shirika hilo limepanga kuongeza kiasi cha fedha kutoka Euro milioni 50 hadi Euro milioni 100 kwa mwaka kupitia mikopo ya masharti nafuu huku kipaumbele kikiwa ni sekta hizo za nishati, maji na miundombinu ya usafirishaji.

Akizunguza na Prof. Muhongo pia watumishi wengine wa wizara hiyo Baudran amesema, Tanzania ni moja ya nchi zinazopewa kipaumbele na shirika hilo.
Amesema, katika miezi ijayo AFD itajikita katika utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa Gridi ya Umeme ya Taifa, uboreshaji wa vituo 10 vya kupooza umeme pamoja na ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji umeme kutoka Geita mpaka Nyakanazi (220 KV).

Huu ni mpango wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kupanua Gridi ya Taifa kwa upande wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambapo itaunganisha Mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma.
Prof. Muhongo amelishukuru shirika hilo kwa ushirikiano wanaouonesha katika kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme nchini.

Amesema, juhudi hizo zitasaidia kutimiza lengo la serikali la kuwa na umeme wa kutosha na wa bei nafuu ambao utasaidia kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali.

Source: Mwanahalisi
Profesa Muhongo katika ubora wake, hapa ndo huwa namkubali huyu mzee wa fix, wacha wahangaike kumtengea chai M7,
 
Ha ha ha mzee anaweza sana sound aiseee na economic maneuvers.

Magu hakukosea kumuweka hapo aisee, kawaliza wakenya kimya kimya kwenye ishu ya bomba hawana hamu naye.
 
Back
Top Bottom