Ufanyike uchunguzi wa kina na wa sirisiri kwa viongozi wanaokufa ghafla

Ufanyike uchunguzi wa kina na wa sirisiri kwa viongozi wanaokufa ghafla

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
36,357
Reaction score
23,760
Ndugu zangu Watanzania,

Kama Msomi Na mchambuzi Nguli wa Masuala ya Siasa ,Kada kindakindaki Wa CCM,mzalendo wa Taifa hili niliyetayari kulifia Taifa langu na Mfuasi Nambari Moja Wa Rais Samia. Nilikuwa naona umuhimu na Maamuzi ya Makusudi kabisa Ya Kuanza kufanya Uchunguzi Wa Kina Na wa siri siri juu ya vifo vya Ghafla vinavyokuwa vimetokea kwa viongozi wetu.

Nasema hivi kwa sababu Uongozi unahitaji Akili sana ,Madaraka ni Vita. Kusalia madarakani Siyo jambo jepesi jepesi au lelemama. Ni vita ya Gizani na hata kwenye Mwanga ,Ni vita inayoweza kupiganwa hata katika ulimwengu ambao siyo kila mtu anaweza kuona kwa macho ya kawaida ya Nyama.

Na kuna watu katika kukutisha,kukuonesha misuri yao ,nguvu yao ,Vita yao , mapambano yao na namna walivyojipanga na kujidhatiti ama kudhamiria kukudhoofisha ama kukupa mawazo ama hofu ama uoga wanaweza kwa makusudi kabisa Kuanza Kumaliza na kuwatanguliza Ardhini wale ama watu wako wote wa karibu na waliokuzunguka na unaowaamini na unaowategemea katika mambo na mikakati mbalimbali.

Wakati Mwingine inakuwa kana kwamba wanakwambia kuwa ngoja Tuanze na Hawa halafu tutakuja kukuambia nini tunataka ama kudhamiria . Ama ni kana kwamba wanakwambia wao ni Taasisi ndani ya taasisi yenye uwezo wa kufanya lolote lile. Haya hufanyika Duniani Kote.

Mfano katika uga wa kivita mfano Taifa moja linaweza kuanza kuhujumu Taifa lingine kwa kuanza kuuwa wanasayansi na wataalumu wake wa masuala mbalimbali kama vile wataalamu wa Nyukilia , teknolojia,Makamanda wako wa ngazi za juu wa kijeshi ,Majasusi wako ,wachumi Nguli na wabobezi , wataalamu wa Diplomasia na mambo mbalimbali sana muhimu Kwa Taifa.

Kwa Hiyo usipokaa sawa na kujipanga utakuta kila mwezi au miezi ama kila Mwaka kuna Jabali moja ama Mwamba mmoja unaondoka katika mazingira ya kutatanisha sana na yasiyo eleweka wala kuelezeka. Hivyo usipochukua Hatua za haraka utajikuta umebakia pekee yako Jangwani bila msaada ama nguvu ya aina yoyote ile.

Hivyo kama ni vita ya ndani kwa ndani mambo fulani ya haraka huweza kufanyika . Mambo hayo huwa ni Kama vile kubadilisha ama kupangua Baadhi ya watu katika maeneo fulani fulani kwa Dharura ili uingie katika Uchunguzi wa kina na wa ndani kujua nini tatizo ,nani yupo nyuma ,nani ni mfadhili wa mambo hayo ,nguvu yake ipo wapi, mtandao wake ukoje na unahusisha Watu wa aina gani na makundi gani na uungwaji mkono wake ukoje.

Lakini pia huwa ni muhimu kuongeza na kuimarisha ulinzi kwa Watu nyeti ,muhimu na wa kimkakati na ambao wanaweza kuwa tageti. Narudia kusema kuwa Siasa siyo lelemama. Ni vita ambayo ilianza tangia kuumbwa Kwa Dunia Hii tena ilianzia Mbinguni huko huko. Maana hata shetani mwenyewe alitaka kuabudiwa kama Mungu vile na ndio maana akashushwa Duniani.

Lakini pia katika hali kama hiyo huwa ni muhimu sana kutowaamini Watu . Binadamu siyo wa kuwaamini, wengi ni vigeugeu na wengine wamevaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni Chui ama wamekaa karibu yako kwa ajili ya kukuhujumu na kusoma mwenendo wako na mipango yako ili kupeleka kwa wabaya wako ili iwe rahisi kukudhoofisha.

Narudia tena kusema kuwa usimwamini Binadamu kwa asilimia zote maana unayemuamini ndiye anayeweza kutumika kukuangamiza kwa urahisi na wepesi sana.

Mengine nitarejea kuandika baadaye kidogo. Viongozi wetu najua huwa wanapitia mambo makubwa na mazito sana na wakati mwingine hawalali na kupata usingizi usiku na ndio maana ni muhimu sana kukesha pia tukiwaombea Viongozi wetu. Kama ambavyo mimi huwaombea viongozi wangu ili Mungu awalinde, kuwapigania ,kuwatetea wakati na muda wote dhidi ya adui muovu.

Maana bila uwepo wa Mungu mwanadamu afanya na kukesha bure akilinda maana Mungu ndiye muweza wa yote na vyote. Na ndiye awezaye kumlinda mwanadamu kwa kumpatia maarifa na ufahamu na njia ya masuala mbalimbali.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Ulitaka afe Nani?

Babako? Au mamako? Mtoto wako au mke wako?

Huyu amekufa kifo Cha kawaida wenzetu walikufa na kufukiwa 50 kwenye kaburi moja

Imeandikwa kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti

Mliyiyafanya October 29 mwaka Jana na bado mtalipwa .
Embu acha kujiandikia tu bila kufikiri
 
Back
Top Bottom