Ufalme wa Inshallah

saryia toly

Member
May 29, 2014
6
0
democracy.jpg

UFALME WA INSHALLAH

Huu ni ufalme wa mfano. Ufalme ambao unasifiwa kwamba unapigiwa mfano duniani kote. Ama kwa hakika, raia wa falme mbalimbali wanahusudu kuwa raia wa falme hii iliyosifika kwa miongo mingi kama falme yenye Amani, falme yenye demokrasia, falme yenye diplomaisia madhubuti, uhuru wa habari, falme inayokua kiuchumi kwa kasi kubwa, falme yenye kila sifa njema. Hutaacha kutaja vivutio vya utalii, umoja wa watu wake hali kadhalika utamaduni wake. UFALME WA INSHALLAH

Ufalme unapata bahati ya kupata wafalme shupavu, wenye maono ya mbali, msingi mkubwa ukiwa umesimikwa na muanzilishi wa ufalme huu, Mfalme Banaki. Mfalme huyu mashuhuri anafanikiwa kuweka misingi ambayo ndiyo imeufanya ufalme huu uendelee kuwa imara ingawa wafalme mbalimbali wameongoza baada ya mfalme Banaki. Kila mfalme anayechukua kiti anaongoza kwa kufuata misingi iliyowekwa na mfalme Banaki.

Wafalme wote wanaongoza kwa namna inayofanana kwa kuwa wafalme wote wanatoka katika familia moja, pengine ni kufuatana na mwongozo wa familia yao chini ya Muasisi wa Ufalme huu akiwa ni mfalme Banaki. Wananchi wa ufalme huu wanaupenda sana utawala wao na wanakua watiifu wakifuata miongozo mbalimbali inayotolewa na wafalme wao.

Hata ivyo miaka inakwenda na mabadiliko ya kimaendeleo ya wananchi inapungua kasi, na inaonekana iko nyuma ukilinganisha na falme zingine majirani wa ufalme huu wa Inshallah. Muasisi wa ufalme huu mfalme Banaki anatumia ushawishi wake na anafanikiwa kuanzisha mfumo mpya wa utawala wa kukaribisha familia nyingine zenye karama za uongozi kushiriki katika kuwania nafasi za uongozi za ufalme, ikiwamo pamoja na nafasi kubwa ya Mfalme wa ufalme. Na hii inakua ndio mwisho wa ufalme wa kurithi, na badala yake mfalme anaanza kupatikana kwa kushindanishwa baina ya familia mbalimbali

Tawala kadhaa zinapatikana kwa njia ya kushindanishwa na kupigiwa kura na wananchi, laikini hata hivyo familia ya Banaki inaendelea kuibuka mshindi katika nafasi ya ufalme kila mara uchaguzi unapofanywa. Wazee wa baraza wenye dhamana ya kusimamia kura na kumtangaza mshindi wanalalamikiwa na nyingi za familia zinazoshiriki katika kuwania nafasi ya ufalme kama wanapendelea familia ya Banaki. Wazee wa baraza kwa mujibu wa muongozo wa ufalme wa Inshallah wanateuliwa na mfalme, hivyo washiriki wengine kwenye uchaguzi wanadhani wanapendelea familia ya mfalme kwa kuwa yeye ndio aliyewachagua.

Familia hizi washiriki katika kugombea nafasi ya ufalme zinafanya jitihada ya kutaka muongozo wa ufalme ubadilishwe ili kuwe na usawa uhuru na haki kwenye zoezi la kumchagua mfalme, lakini hawafanikiwi. Utaratibu na muongozo unasalia uleule ulioanzishwa na muasisi wa ufalme, mfalme Banaki. Watawala wanabadilika mara kadhaa lakini wote kutokea katika familia ya Banaki.

Katika uchaguzi mmoja, anachaguliwa mfalme mpya, mfalme Jodo. Huyu anakua mfalme mashuhuri sana, akiwa na sifa kubwa ya ujasiri na uthubutu. Anashangiliwa sana na kuonekana ndiye mfalme ambaye ataleta maendeleo Zaidi. Hata hivyo, baada ya muda mfupi anaonekana kuwa mfalme katili, asiyependa maoni mbadala, wala uhuru wa watu na vyombo vya habari kwenye kujadili masuala yanayohusu ufalme au kukosoa. Anajipambanua kama mfalme anayewajali raia maskini huku akiwakandamiza wale wenye utajiri. Anatangaza vita dhidi ya matajiri akisema kuwa hao ndio sababu ya umaskini uliopo katika ufalme wake.

Hii inawafanya matajiri wengi wenye biashara na uwekezaji katika ufalme huu wa ishallah kuanza kuhamisha mali zao kwenda katika falme zingine, na wengine wanafunga biashara zao kwa kuwa hawaoni mazingira rafiki ya kufanya bishara. Raia wengi maskini wa ufalme huu wanashangilia hatua mbalimbali anazochukua mfalme wao Jodo.

Siku zinakwenda, hali ya maisha ya raia wengi inadorora Zaidi. Raia wanakosa fedha, huduma za kijamii kama dawa hospitalini zinakua tabu kupatikana kwa wananchi wasio na fedha. Mfalme Jodo anawahimiza raia wake wafanye kazi kwa bidi, kwa sababu bila kufanya kazi hatawapa ugali. Hata hivyo, raia hawajui ni wapi pa kupata kazi. Vijana wengi wanaongezeka mtaani, wasomi na wasio wasomi wakiwa hawana ajira. Mfalme Jodo anapata upinzani mkali kutoka familia shindani za ufalme, vilevile anapata ukosoaji mkubwa kutoka falme zingine kama mfalme ambaye ni katili, asiyeshaurika, na asiyependa ushirikiano na falme zingine.

Akiwa katikati ya utawala wake, kunatokea vita iliyohusisha falme mbali mbali. Falme nyingi zinaungana na kuwa na mbinu moja ya kujilinda, lakini mfalme Jopojoma anakataa kushirikiana na falme nyingine na badala yake anaamini na kuwaaminisha wananchi wake kwamba vita hiyo haitawaathiri raia wake kwa kuwa Mungu yupo pamoja nao. Katikati ya vita hiyo adui wanafanikiwa kuingia katika ufalme wa Jodo na kumteka mfalme hatimaye wanamuua.

FUNZO LA HADITHI HII
  • Demokrasia ya vyama vingi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi. Ufalme wa Ishallah katika hadidhi hii ulianza vyema kimaendeleo wakati ulipoasisiwa na mfalme Banaki, lakini baadaye ulianza kulega lega kimaendeleo kwa sababu kulikua hakuna chachu mpya. Wafalme wote walikuwa wanatoka familia moja na ni Dhahiri walikua na mtazamo mmoja. Pale chama kimoja cha siasa kinapoongoza pasipokua na nafasi kwa vyama vingine kupata fursa ya kuongoza, maendeleo yanaweza kuwa ya kasi ndogo
  • Pasipokuwa na demokrasia na uhuru wa habari na kujieleza, ni fursa ya viongozi wasiofaa kuendelea kusalia madarakani kuendelea kukwamisha maendeleo pasipo wananchi kujua kwa sababu vyanzo vya habari haviko huru kuusema ukweli
  • Wananchi wengi wasiokuwa na uelewa mpana wa kutafakari mambo wanarubuniwa kiurahisi na watawala kwa maneno hewa, na hii imekuwa chanzo cha baadhi ya mataifa ya kiafrika kushindwa kufanya mapinduzi ya kiraia kuwa viongozi wa kihimla wanapata ufuasi wa wananchi wengi wasiokuwa na uelewa wa mambo
  • Hakuna maendeleo pasipokuwa na demokrasia, na hakuna maendeleo pindi ambapo uongozi haubadiliki. Kuna uhitaji wa kuwa na viongozi wapya kila baada ya muda Fulani. Uongozi mpya unakuwa na mawazo mapya, nguvu mpya, na kasi mpya
  • Wananchi ni kiungo namba moja katika kuleta mapinduzi ya kidemokrasia. Sauti ya wanachi ni kubwa sana, na hivyo wananchi wanapaswa kupaza sauti zao bila woga. Kukaa kimya au kuwa waoga kusema ni kukubali kuweka rehani uhuru wao, na hatimaye anguko katika Nyanja mbali mbali
  • Penye uwazi hapaharibiki kitu. Penye uwazi panakuwa na fursa ya mawazo yenye kujenga kupata kusikilizwa na kufanyiwa kazi
  • Nchi maskini Zaidi duniani haina demokrasia, na ipo Afrika
 
Back
Top Bottom