Ufahamu ugonjwa wa Tinea Versicolor

doktamathew

Member
Mar 12, 2013
22
43
UGONJWA WA TINEA VESICOLOR (PITYRIASIS VERSICOLOR
Imeandaliwa na @doktamathew

Huu ni ugonjwa wa fangasi ya ngozi ambao hupelekea mgonjwa kuwa na mabaka mabaka meupe, meusi na maeneo mekundu mekundu katika ngozi yake, ugonjwa huu hushambulia sana maeneo ya mgongo ,mabegani na mikono juu ya kiwiko(proximal upper extrimities). Ugonjwa huu upo sana na maarufu miongoni mwa watu wengi tu na wengine huiona hali hii kama kawaida

Ugonjwa huu husababishwa na hamira mpenda mafuta aitwae Malasezzia furfur, Malasezzia globosa na Malasezzia sympodialis,hamira huyu hupenda sana kuwashambulia vijana na watu wenye umri wa kati.ugonjwa huu hauhusiani na uchafu ama usafi wa mtu

WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU
1) Kuwa kijana au mtu mwenye umri wa kati
2) Utapiamlo
3) Wenye kisukari,saratani na HIV
4) Walio kwenye maeneo ya joto
5) Walio kwenye maeneo yenye unyevu unyevu
6) Ujauzito
7) Watu wenye mvurujiko wa homoni
8) Watu wenye ngozi zenye mafuta
.
ITAENDELEA POST IJAYO
Screenshot_20200330-113859.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom