Ufahamu ugonjwa wa Shigela (Kuhara)

Ufahamu ugonjwa wa Shigela (Kuhara)

doktamathew

Member
Joined
Mar 12, 2013
Posts
21
Reaction score
43
SHIGELA (SHIGELOSIS)
Huu ni ugonjwa hatari wa kuharisha ambao husababishwa na kimelea aitwae Shigella dysenteriae ..kimelea huyu aligundulika kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1897 huko Japan,na mtaalamu wa mikrobiolojia aitwae Kiyoshi Shiga,kipindi hiko kulikua na mlipuko mkubwa wa kuhara.

Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yeyote lakini Watoto wenye umri chini ya miaka 5 na wenye Upungufu wa kinga mwilini hupata Zaidi na pia hupata madhara Zaidi ikiwemo kifo

Kitakwimu ugonjwa wa kuhara huwapata karibu watu Milioni 190 kwa mwaka na kati yao watu 170,000 hupoteza Maisha kila mwaka.

Njia kuu ya kuambukizwa ugonjwa huu ni kupitia kunywa maji au kula chakula ama matunda yaliyochafuliwa na huyu kimelea,kiufupi huu ni ugonjwa wa uchafu tu.

DALILI ZA UGONJWA WA SHIGELA
Dalili za shigella mara nyingi huanza kuonekana kuanzia siku ya 1 hadi ya 5 toka uambukizwe huyu kimelea na kutokea kwa dalili hutegemea na umepata dozi ya kiasi gani ya vimelea;ukipata wengi na dalili hujitokeza mapema kabisa.

1) Homa kali(fever)
2) Maumivu makali ya tumbo,tumbo linakua linakatakata au kunyonga maeneo ya kitovu au chini ya kitovu(abdominal cramps)
3) Kupata mkereketo/hamu ya kwenda chooni iambatanayo na maumivu bila ya hata kua na choo(tenesmus)
4) Kupata choo laini chenye makambakamba au vitu kama makamasi mazito(mucoid diarrhea)
5) Kuharisha damu(Bloody diarrhea)
6) Kuharisha maji(Watery diarrhea):hapa mtu anaweza kuharisha kuanzia mara 8 hadi 10 kwa siku ,kwa hali mbaya mtu huharisha hadi mara 100 kwa siku
7) Kichefuchefu kikali na kutapika

MATIBABU YA SHIGELA
Kwa bahati nzuri ugonjwa unaeza kuisha wenyewe hata bila kuutibu na gonjwa hua anapona kabisa bila ya shida yeyote.Kama baada hali inazidi kuongezeka na kuwa mbaya basi matibabu ni lazima ili kupunguza madhara ya shigela.

Kwa kuwa mtu anakua ameharisha sana hivo atakua amechoka au kuishiwa nguvu sana na hivo basi kitu cha kwanza na kupata maji mengi yenye chumvi na sukari (ORS) ili kurudisha maji na madini uliyopoteza,kama utakua huwezi kunywa basi utapewa drip..baada ya hapo utapata dawa za vidonge ambazo utazitumia kwa siku 7-10.

NB:MGONJWA WA SHIGELA HATAKIWI KUPATA DAWA ZA KUZUIA KUHARISHA KWANI KUFANYA HIVO UNABAKISHA SUMU NDANI NA KUMFANYA AENDELEE KUHARISHA PALE TU DAWA ITAKAPOISHA,MWACHE AHARISHE MPAKA SUMU ITAKAPOISHA.

MADHARA/MATOKEO YA SHIGELA
Kama shigela haitatibiwa yaweza kuleta madhara yafuatayo

1) Degedege (Seizures)
2) Kupata homa kali ya damu(septicaemia, Bacteremia )
3) Kuvimba puru na njia ya haja kubwa kutoka nje(Proctitis or rectal prolapse )
4) Utumbo kuziba/kua mdogo(Intestinal obstruction)
5) Kutanuka utumbo mpana(Toxic megacolon)
6) Kutoboka utumbo mpana(Colonic perforation)
7) Mafigo kushindwa kufanya kazi(Hemolytic-uremic syndrome)

images%20(12).jpg


Sent using Doktamathew phone
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom