Ufahamu ugonjwa wa kideri(newcasle disease).

farmersdesk

Senior Member
May 26, 2012
164
120
Na Dr Khalfan, Farmas cntre
Ugonjwa huu hutokea mara kwa mara kwa kuku wa umri wowote. Ugonjwa huu husababisha vifo vingi ukiingia(flock motality) na vifo hivi hufikia hadi 100% ya kuku ulio nao .
Ugonjwa huu umegawanyika sehemu tatu kulingana na sehemu ya mwili iliyo shambuliwa.
Ugonjwa huu huweza shambulia sehemu sifuatazo
Mfumo wa chakula
Mfumo wa faham
Mfumo wa upamuaji


Kwa ujumla dalili zake ni kama ifuatavyo
1)kuku kuharisha kijani
2)kupumua kwa shida
3)kupinda kwa shingo (toticolis)
4)kushusha mabawa (wing nerve paralisis)
5)kuku kushindwa kula.
6)na hatimae kuku hufa
Tiba
Ugonjwa
huu hauna tiba.
Ugonjwa huu husababishwa na virusi na hivo njia pekee ya kuepukana na ugonjwa huu ni kuwapa chanjo kuku kuku wote. NB kama kuku ni mgonjwa usimpe chanjo.mtibu kwanza apone hafu then mpe chanjo

Vaccination regime.
......Siku ya saba wape vifaranga chanjo ya kwanza.(first newcastle vaccine)
.....siku ya 28 (second newcastle vaccine)
.....baada ya miezi mitatu (third newcasle vaccine)
Halafu utakua unawapa kila baada ya mwaka mmoja. Hakikisha vifaranga wako wanapata stress vita kila baada ya chanjo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom