Ufahamu ugonjwa wa homa ya Chikungunya

Ufahamu ugonjwa wa homa ya Chikungunya

doktamathew

Member
Joined
Mar 12, 2013
Posts
21
Reaction score
43
Imeandaliwa na @doktamathew

Huu ni ugonjwa wa virusi unaoenezwa na mbu aina ya Aedes aegypti na Aedes albopictus. Neno chikungunya limetoholewa kutoka neno la kimakonde(kun-kunyala) ambalo linamaanisha kupinda au kujikunja au kuinamia mbele na hali hio ndio inayawaelezea namna wagonjwa wenye ugonjwa huu huonekana.

Ugonjwa huu uligundilika kwa mara ya kwanza mkoani mtwara mwaka 1952 kutokana na mlipuko ulotokea ya watu walikua wanapinda pinda bila sababu. HIVI KARIBUNI(TAREHE 9/2/2020) KUMEKUA NA MLIPUKO WA HOMA HII NCHINI DR CONGO

NAMNA UGONJWA HUU UNAVOAMBUKIZWA
Homa hii humpata mtu pale anapong’atwa na mbu tajwa hapo juu ambae amebeba kirusi wa chikungunya. Mbu hawa wanang’ata nyakati zote za mchana lakini san asana wanang’ata sana mida ya asubuhi na jioni.ikumbukwe kwamba mbu hawa hawa ndo wanaoeneza magonjwa ya manjano, dengue na zika.

DALILI ZA HOMA YA CHIKUNGUNYA
Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana kati ya siku 3 hadi 7 toka pale mgonjwa ang’atwe na mbu mwenye huyo kirusi

1. Homa(fever): hii ni mojawapo dalili kuu na ya kwanza kutokea,mgonjwa anaweza kua na joto kali la kuanzia 38-39 kwa muda wa siku 3 hadi 5
2. Maumivu ya viungo(anthralgia):
3. Kuvimba viungo(anthritis)
4. Kutokewa na vipele na harara pamoja na malengelenge
5. Mwili kuchoka choka
6. Maumivu ya misuli
7. Maumivu ya kichwa
8. Kichefuchefu na kutapika

NAMNA UGONJWA HUU HUGUNDULIKA
Mgonjwa atahisiwa anaweza kua na ugonjwa wa chikungunya kama anahistoria ya kutoka ama kuishi maeneo yenye mbu wenye mabakamabaka(aedes) na ana dalili tajwa hapo juu. Kama mgonjwa atakuja na mambo hayo basi atafanyiwa vipimo ili kuthibitisha

MATIBABAU YA UGONJWA HUU
Ugonjwa wa chikungunya kwa bahati nzuri sio ugonjwa unaoua watu bali utakuletea maumivu makali na hata ulemavu wa kudumu. Mgonjwa atatibiwa kulingana na namna atakavyokuja na mfumo uliathirika. Mgonjwa atapewa dawa za maumivu,atafanyiwa mazoezi ya viungo,atafanyiwa massage kama anayofanya dada yangu

@happinessmassage,atapewa msaada wa maji ya dawa kulingana na hali ya mgonjwa(supportive treatment), mgonjwa anaweza kuhitaji matibabu makubwa ya mifupa kutokana na uharibifu wa viungo ambavyo anaweza kuupata kama matokeo ya ugonjwa huu.

Kwa bahati nzuri sana wagonjwa wote wa chikungunya hupona na kwenda nyumbani

NAMNA YA KUJILINDA NA CHIKUNGUNYA
Njia za kujikinga na chikungunya ni zile zile za kujikinga na malaria ,mojawapo ya njia ni kama ifuatavyo
1) Kujilinda ili using’atwe na mbu kabisa
2) Haribu vifuu vya nazi,ondoa makopo yote yanayotuamisha maji,ondoa matairi mabovu yanayotuamisha maji.
3) Fyeka majani au nyasi zinazozunguka nyumba yako
4) Visima vya maji na mapipa/matank ya maji yaliyopo nje ya nyumba yafunikwe
5) Pendelea kuvaa mashati ya mikono mirefu na suruali pamoja na soksi
6) Kupulizia dawa ya kuua mbu wa mchana katika maeneo mbalimbali(kazi ya serikali)
7) Vaa nguo zinazofukuza mbu
8) Jipake dawa/mafuta yanayofukuza mbu

images%20(23).jpg

IMG_20200407_200145_011.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Neno chikungunya limetoholewa kutoka neno la kimakonde(kun-kunyala)
KISWAHILI SASA MNAKIHARIBU. chikungunya!! Hebu msilisajili hilo neno ktk lugha yetu ya kiswahili ni nzuri hata kuizungumza mtu unasikia Raha. Sasa mkianza kutuchomekea maneno kama ya kilugha za ndani ndani hicho kinakuwa sio kiswahili.

Wenye asili ya kichagga wao watatumia kichaga chao, wamasai waongee hamna shida. Lakini tukija ktk lugha yetu ya taifa Kiswahili basi kiwe ni kiswahili bila mineno migumugumu kama hiyo tafadhali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom