Ufafanuzi kuhusu faini ya baiskeli

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
30,988
72,186
Leo nliamua nichukue sh 30000 kwenye pochi yangu ili nikanunue mitoko mnadani nkapanda baskeli yangu nikashika njia lkn nlipofika nkashuka nkaanza kuikokota baada ya kupiga kama tambo 50 ndani ya mnada huo mara ghafla nkashangaa mzee mbele yangu akashika bike yangu ikapelekwa zilipokuwepo bike nyengine kumbe ile sehemu huwa ni ya parking ya bike.

Kufika pale naanza kuambiwa soma hicho kibao kukisoma "kimeandikwa ni marufuku kupita na bike kwenye mnada faini 10000".

Nikaanza kuwaomba msamaha coz nlikuwa sifahamu na ni mgeni kwanza mkoa huu me nshagazoea mwanza sizani kama pale sabasaba wanasheria kama hii.. Lakini wakati naingia sikuona kibao chochote cha onyo na nikajiuliza kwann wasikae zile sehemu za kuingilia ili mtu akija tu kama anabike wanamwambia hapohapo anapaki.

Lakini mwishowe nliona isiwe tabu nkawapa. Nachotaka kujua hapa hii sheria ipo kwenye katiba? na ni kwa mamlaka gani inafanya kazi? na hiyo faini ni halali? coz walivyoandka kwenye daftari ni sh 4500 wkt ni buku kumi walinitoza..!
 
Sasa inakuwaje utoe buku 10 kisha uandikiwe 4500? Tuanzie hapo kwanza
 
Hiyo ya juu umepigwa tu ila kuhusu fine hiyo ni kawaida na hizo ni sheria ndogo ambazo hutengenezwa ndani ya local govt kama halmashauri ya mji, jiji, wilaya hata serikali ya kijiji. Na hizo sheria znaruhusiwa kikatiba ingawa ni lazima ziendane na katiba au sheria mama za nchi
 
Sasa inakuwaje utoe buku 10 kisha uandikiwe 4500? Tuanzie hapo kwanza
niliwauliza wakasema hiyo hela wameigawagawa ktk kimahesabu waltaka wanipigie hiyo hesabu me nlkataa coz nlkuwa nawahi na hata kama wangeipiga isinge nisaidia ki2 maana hela ishaenda
 
Ushapigwa!ila ukituliza akili,waweza enda mbele ya vyombo vya sheria wakusaidie kuirudishia hio 5500 waliokuzidishia!kwanu ilo soko liko ktk ngazi gani kisheria!?ni kijiji au?
 
Hiyo ya juu umepigwa tu ila kuhusu fine hiyo ni kawaida na hizo ni sheria ndogo ambazo hutengenezwa ndani ya local govt kama halmashauri ya mji, jiji, wilaya hata serikali ya kijiji. Na hizo sheria znaruhusiwa kikatiba ingawa ni lazima ziendane na katiba au sheria mama za nchi
sasa kama ni sheria kwann wakae mbali na maeneo ambayo watu wanaingilia maana me pale ni mgeni ndo mara yangu ya kwanza kuingia kwenye mnada huo sijui wanapopak bike wala kibao sikukiona
 
Ushapigwa!ila ukituliza akili,waweza enda mbele ya vyombo vya sheria wakusaidie kuirudishia hio 5500 waliokuzidishia!kwanu ilo soko liko ktk ngazi gani kisheria!?ni kijiji au?
sifahamu lipo ktk ngazi gani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom