The Don
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 3,499
- 1,172
Ni muda sasa mgombea uraisi kupitia CHADEMA kupitia mwavuli wa UKAWA mh. Edward N. Lowassa anahusishwa na tuhuma za ufisadi kubwa ikiwa ni Richmond,ufuatao ni ufafanuzi wa kisheria dhidi ya madai hayo;
1. Kwa mujibu wa https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Majadiliano_ya_mtumiaji:UFISADI
Neno hili kwa kawaida lina maana ya maovu au uharibifu wa aina yoyote ile.Aidha laweza kuleta maana ya matumizi ya madaraka au mamlaka ya ofisi za umma au za kibinafsi kwa manufaa ya mtu binafsi au kundi la watu.Wanaojihusisha katika ufisadi hujulikana kama mafisadi au kwa umoja mfisadi.
2. Kwa mujibu wa sheria ufisadi ni kosa la jinai,jinai inamaanisha makosa yenye kuharibu amani pamoja na matakwa mengi ya dola na jamii nzima .hivomshtakiwa baada ya kutiwa hatiani huadhibiwa kwa kifungo,faini au vyote viwili japo faini pekee ni mara chache sana,mfano wa makosa haya ni wizi,uharibifu wa mali,ubakaji,ufisadi n.k
3.Tanzania kesi za jinai huendeshwa na serikali kupitia ofisi ya D.P.P kama ilivoanzishwa na Director of Public Prosecutions Act No.15 of 1984 ambapo hushirikiana na Attorney General office,police n.k
4. Ufisadi/rushwa Tanzania husimamiwa na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Cap.329 kama ilivofanyiwa marekebisho mwaka 2002(the Prevention and Combating of Corruption Act [Cap 329 R.E 2002] kama sheria mama ikisaidiwa na sheria au kanuni zianzishwazo kuisaidia.
5. Kupitia sheria ya rushwa iliyotajwa hapo juu ufisadi/rushwa imeelezewa chini ya kifungu namba 3 na sehemu ya 3(part iii).
6. Kupitia sheria ya rushwa tajwa hapo juu taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ikaanzishwa (TAKUKURU/PCCB) chini ya sehemu ya II,kifungu namba 5 cha sheria hiyo.
7. Sehemu ya iv ya sheria ya rushwa tajwa hapo juu inaelezea uendeshwaji wa kesi za ufisadi kupitia TAKUKURU kama ilivopewa jukumu hilo sehemu ya II ya sheria hiyo.
Baada ya kuona hayo Lowassa si fisadi kama wanasiasa wanavotuaminisha kupitia uchanganuzi ufuatao;
I. Kesi za jinai huendeshwa na serikali na si mtu au kikundi binafsi,hivo hawana mamlaka juu ya hilo(locus standi) dhidi ya Lowassa.
ii. Kesi za jinai huthibitishwa kwa Kiwango cha juu pasipo kuacha shaka yoyote(proving beyond all reasonable doubt), kitu ambacho hakijafanyika.
iii. Kwa mujibu wa ibara ya 107 A ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama irekebishwavo mara kwa mara, mahakama ndicho chombo huru pekee chenye kusikiliza na kutoa maamuzi ya haki,hivo kuishia majukwaa ya siasa kumsema Lowassa ni fisadi ni kuingilia uhuru wa mahakama na kudharau mihimili mikuu ya serikali kama katiba ilivoeleza.
iv. Kupitia ibara ya 13(6)(b) inatoa presumption of innocence kwa mtuhumiwa kabla mahakama haijathibitisha,hivo basi hata kama kesi dhidi ya Lowassa ingekua mahakamani na uthibitisho bado,Lowassa km watuhumiwa wengine asingeitwa fisadi hadi pale mahakama ambapo ingethibitisha kosa lake kwahiyo Lowassa si fisadi.
v. Raisi pekee ndiye mwenye kinga ya kutoshtakiwa,mawaziri hawana kinga hiyo,kwanini serikali inasua kumchukulia hatua kama ni kweli badala yake watu wanaishia kuwa majaji na mahakimu majukwaani kupitia report ya mwakyembe inayopingwa na pande zote mbili?
vi. Mwisho makosa ya jinai, anayeshtaki ndiye mwenye kuthibitisha pasipo mashaka yoyote kwani mtuhumiwa anawekwa ktk nafas ya kiupendeleo dhidi ya mashtaka,Leo wanasiasa wanatuaminisha wananchi Lowassa ni fisadi je tuanze kuchukua sheria mkononi dhidi ya viongozi wote wenye tuhma nchi itakalika? Nini kazi ya TAKUKURU na Mahakama?
Tuache siasa uchwara katika mambo ya msingi, tujenge taifa kwa kuheshimu sheria, karibuni kwa maoni zaidi.