VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Viongozi na wanachama wetu wa kawaida wa CCM wamekuwa mstari wa mbele kukosoa demokrasia ndani ya vyama vya upinzani. Mhanga mkubwa wa hili ni CHADEMA,chama kikuu cha upinzani nchini. Kuchaguliwa kwa Freeman Mbowe kulikuwa gumzo lenye wingi wa kebehi. Mbowe wa CHADEMA aligombea Uenyekiti na Ndugu Mbarouk wa Tabora.
Sasa,CCM iko mbioni kupata Mwenyekiti mpya wa Taifa. Tayari CCM imedhamiria kumkabidhi uenyekiti Rais John P. Magufuli. Hakuna nafasi chamani ya uenyekiti kugombewa. Wanachama hawaalikwi wala hawataalikwa kugombea uenyekiti wa CCM Taifa. Ni kama Mwenyekiti ameshapatikana.
Uenyekiti wa CCM Taifa ni kielelezo cha ukosefu wa demokrasia chamani na alama ya chama dola. Hakuna ulazima wowote wa kidemokrasia kwa Rais atokanaye na CCM kuwa Mwenyekiti. Kama CCM ni walimu wa demokrasia,tumuache Mwenyekiti Kikwete hadi mwakani 2017 na kuruhusu uenyekiti ugombewe na mwanachama yeyote. Tuseme na kutenda!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam