Uenyekiti wa CCM Taifa: Kielelezo cha ukosefu wa demokrasia chamani na chama dola

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Viongozi na wanachama wetu wa kawaida wa CCM wamekuwa mstari wa mbele kukosoa demokrasia ndani ya vyama vya upinzani. Mhanga mkubwa wa hili ni CHADEMA,chama kikuu cha upinzani nchini. Kuchaguliwa kwa Freeman Mbowe kulikuwa gumzo lenye wingi wa kebehi. Mbowe wa CHADEMA aligombea Uenyekiti na Ndugu Mbarouk wa Tabora.

Sasa,CCM iko mbioni kupata Mwenyekiti mpya wa Taifa. Tayari CCM imedhamiria kumkabidhi uenyekiti Rais John P. Magufuli. Hakuna nafasi chamani ya uenyekiti kugombewa. Wanachama hawaalikwi wala hawataalikwa kugombea uenyekiti wa CCM Taifa. Ni kama Mwenyekiti ameshapatikana.

Uenyekiti wa CCM Taifa ni kielelezo cha ukosefu wa demokrasia chamani na alama ya chama dola. Hakuna ulazima wowote wa kidemokrasia kwa Rais atokanaye na CCM kuwa Mwenyekiti. Kama CCM ni walimu wa demokrasia,tumuache Mwenyekiti Kikwete hadi mwakani 2017 na kuruhusu uenyekiti ugombewe na mwanachama yeyote. Tuseme na kutenda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
mmeshindwa muondoa DJ ZERO chamani kwenu na kuwafukuza kama sio kuwauwa wote wanaoutaka uenyekiti leo mnaingilia ya CCM,,katiba yao iko wazi kabisaa naa mnajua ukweli lakn mnjifanya manyumbu kama kawaida yenu,,rais ndo mwenyekiti wa chama, nyie kwenu n Ndugu wa Mtei ndo mwneyekiti wa chama.. easy
 
Viongozi na wanachama wetu wa kawaida wa CCM wamekuwa mstari wa mbele kukosoa demokrasia ndani ya vyama vya upinzani. Mhanga mkubwa wa hili ni CHADEMA,chama kikuu cha upinzani nchini. Kuchaguliwa kwa Freeman Mbowe kulikuwa gumzo lenye wingi wa kebehi. Mbowe wa CHADEMA aligombea Uenyekiti na Ndugu Mbarouk wa Tabora.

Sasa,CCM iko mbioni kupata Mwenyekiti mpya wa Taifa. Tayari CCM imedhamiria kumkabidhi uenyekiti Rais John P. Magufuli. Hakuna nafasi chamani ya uenyekiti kugombewa. Wanachama hawaalikwi wala hawataalikwa kugombea uenyekiti wa CCM Taifa. Ni kama Mwenyekiti ameshapatikana.

Uenyekiti wa CCM Taifa ni kielelezo cha ukosefu wa demokrasia chamani na alama ya chama dola. Hakuna ulazima wowote wa kidemokrasia kwa Rais atokanaye na CCM kuwa Mwenyekiti. Kama CCM ni walimu wa demokrasia,tumuache Mwenyekiti Kikwete hadi mwakani 2017 na kuruhusu uenyekiti ugombewe na mwanachama yeyote. Tuseme na kutenda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Kinacho nikwaza ni kule kulazimisha mada MFU kuchangiwa humu jamvini, Huisha mada na leta mada zinazoonyesha ubunifu na ukomavu wa mawazo na mijadala, na si ushabiki
 
Ndio ushachangia hivyo tena:(:(
 
ivi wapinzani leo wamekuwa wakumtetea jk? kweli ukiwa huna unachokiamini, utamini na kutoamini chochote ilimradi upate maslai.
 
Nafikiri katiba ya CCM inataka iwe hivyo na kufuata katiba ni sehemu ya demokrasia.
Unapopiga kura ya kumchagua mgombea urais kwa tiketi ya CCM unakua pia unamchagua mwenyekiti wa CCM ajaye na kila mwanachama analijua hilo kwamba kuna kofia mbili ziko pamoja unapoichagua kofia moja ya mgombea urais umemchagua mwenyekiti tayari.
Nafikiri ni mfumo tu unaochanganya ingawa kiuhalisia unapomchagua mgombea urais unakua unamchagua mwenyekiti wa chama.
 
Hata kukiwa na democrasia, chini ya Jecha hakuna kitu, bora muendelee kupeana tu
 
Nafikiri katiba ya CCM inataka iwe hivyo na kufuata katiba ni sehemu ya demokrasia.
Unapopiga kura ya kumchagua mgombea urais kwa tiketi ya CCM unakua pia unamchagua mwenyekiti wa CCM ajaye na kila mwanachama analijua hilo kwamba kuna kofia mbili ziko pamoja unapoichagua kofia moja ya mgombea urais umemchagua mwenyekiti tayari.
Nafikiri ni mfumo tu unaochanganya ingawa kiuhalisia unapomchagua mgombea urais unakua unamchagua mwenyekiti wa chama.
Na asiposhonda uraisi?
 
Back
Top Bottom