MURUSI
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 4,496
- 8,734
Uwezo wa Ufahamu kwa watangazaji wengi wa hizi FM ni mdogo sana, Mtangazaji anatakiwa kuwa mtu mwenye uelewa mpana sana wa mambo mbali mbali ya Dunia si kwa kusoma habari bali kuyajua kabisa.
Watangazaji wengi ni weupe sana vichwani na asilimia 90 ya vipindi vyao ni ya Udaku mtupu, kama sio kipindi cha Mziki basi ni mambo ya Majungu, Umbea, vipindi ya maana kwao ni labda taarifa za habari basi.
Niliwahi shangaa siku moja mtangazaji wa Radio moja kubwa kabisa ya FM walimuelezea Angela Merkel Chancellor wa Ujerumani kwamba ni Waziri Mkuu wa Ujerumani si kwamba alikosea bali hajui na inaonekana studio nzima walikuwa hawajui kwamba yule ni Chancellor na sio Waziri Mkuu wa Ujerumani.
Ukitaka kujua hili fuatilia vipindi vyao vya kila siku, huwezi wafananisha na watangazaji nguli enzi zile kama wa Radio One au Radio Free Africa, Watangazaji walikuwa full equipped na Dunia.
Hawa wa sasa ni udaku umejaa vichwani mwao