Ni siku nyingine tena ambayo wapenzi na wafuatiliaji wa kandanda hususani michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya maarufu kama UEFA CHAMPIONS LEAGUE wakisubiri kushuhudia draw ya michuano hiyo itakayofanyika siku ya leo Alhamisi (27 August 2026) mida ya saa 1 usiku kwa saa za Afrika ya mashariki.
Katikahatua hii kila timu itapangiwa kucheza mechi nane ,mechi nne nyumbani na mechi nne ugenini. Matokeo ya jumla yatakuwa katika mfumo wa ligi ambapo timu nane za kwanza zitakuwa zimefuzu moja kwa moja kuelekea katika hatua ya mtoaano (16 bora) , huku timu ilishika nafasi ya 9 hadi 24 zitacheza playoff kupata timu zingine 8 zitakazo kamilisha timu 16 za hatua ya mtoano na timu nane za mwisho zitakuwa ni rasmi zimeaga mashindano.
Mda je chama lako limo miongoni mwa wababe hao, na je ungependa miamba ipi ikutane. majibu yote hayo yatapatikana usiku wa leo