WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wametishia kugoma kuingia darasani, wakati wowote ili kuishinikiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini (HESLB), kuwapatia mikopo. UDSM wanatarajia kufanya hivyo siku chache baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kugoma kuingia madarasani wakipinga kile walichodai kuwa HESLB imewachelewesha mikopo wanayostahili kupata.