UDSM UE is around

Maho gel

JF-Expert Member
Mar 12, 2014
306
93
Habari zenu wakuu.

Zikiwa zimesalia takribani wiki mbili hivi watu kumalizia test two zao ili wapate course work nakuingia UE, inayoanza mnamo tar 23 JUNE - 4 JULY ,kipindi hiki huwa nikigumu sana kwetu sisi wanafunzi wa UDSM kwa maandalizi , kwani ni kipindi cha shida na mateso, pale ambapo course work zisiposoma vizuri, incomplete nying, carry over, ambazo huwafanya watu wawe katka hali isiyo ya kawaida ( kupaniki) .

Jaman inabidi tu mtu u struggle ili Ue upate kuchomoka au kutoka.Kwa sababu haya ndio matokeo yetu ya mwisho wa muhula (SEMISTER) na huwayanapandisha na kushusha GPA so jamani struggle is very important tu hata ukiingia na course work ndogo ukikazana possibilty ya kupata A au B+ inakuepo,Lengo letu ni kutaka kuondokana na hii SEPTEMBER CONFERENCE, Kwni inaumiza ,wenzio wako nyumbani alafu wewe unakuja chuo ku sapua so bored sana, kitu kingne tuwecare na vitu vyetu mfano simu, laptop, tablets na vitu vingne vya kusomea kwanikipindi hiki wizi na uvamizi ni mwingi sana pia unavoenda kusoma mf yombo kule ni vizuri atleast muwe wengi kiusalama zaidi.

WISHiING YOU NICE PREPARATION UD.
 
Ardhi university also 23 june to 4 july.....................!
 
Vilaza huwa wanajipa moyo kusema UDSM ni chuo cha kata kwasababu vilaza huwa hawachaguliwi UDSM, so kijana ww soma hukohuko ulipo tuache tunaopata DIVISION ONE na UDSM yetu, ww na kathree kako soma huko ulipo. But the truth will stand kwamba kibongobongo ukizungumzia CHUO KIKUU unazungumzia MLIMANI

UMEUA mwanangu G ,mchz mpaka ameogopa mwenyewe na concept ulompatia
 
UMEUA mwanangu G ,mchz mpaka ameogopa mwenyewe na concept ulompatia

Yah unajua baadhi ya wanafunz wa vyuo vingne huwa nashindwa kuwaelewa baada ya kuconcentrate na kitabu vyuon mwao wamalize vizur waondokane na umaskini na haswa watafute means za kutotegemea kuajiriwa sana wao kutwa nzima wanakalia kujipa moyo udsm chuo cha kata eti kisa alitakaga kusoma udsm bac akashndw kusoma kutokana na matokeo dhaifu. Tunajua udsm wanachukuaga best products ila Chuo wala sio tija, tija ni uelewa wa mtu tu. Mtu anaweza kufanya chochote sehem popote. Ni kujiongeza tu, ss kama huyu kijana namuonea huruma sana na ukilaza wake. Ila ni kweli naungana na mchangiaji wa juu pale kwamba AKIKUA ATAACHA
 
vijana bishaneni nani anasoma chuo kizuri au cha kata mkimaliza mje kwenye usahili tuwape kazi....

Intellectual huwa akimaliza chuo anatarget zaidi kujiajiri na sio kuajiriwa, huwa anatumia elimu yake kujitajirisha mwenyewe na sio kufany kaz kwa mtu na kutajirisha mtu mwngne, huwa anafanya watu wamuite boss na sio yy kuita mtu boss... ila usijal mkuu wapo pia ambao wanawaza kuajiriwa watakufata uwape kazi
 
Habari zenu wakuu, Zikiwa zimesalia takribani wiki mbili hivi watu kumalizia test two zao ili wapate course work nakuingia UE, inayoanza mnamo tar 23 JUNE - 4 JULY ,kipindi hiki huwa nikigumu sana kwetu sisi wanafunzi wa UDSM kwa maandalizi , kwani ni kipindi cha shida na mateso,pale ambapo course work zisiposoma vizuri,incomplete nying, carry over, ambazo huwafanya watu wawe katka hali isiyo ya kawaida ( kupaniki) .


Jaman inabidi tu mtu u struggle ili Ue upate kuchomoka au kutoka.Kwa sababu haya ndio matokeo yetu ya mwisho wa muhula (SEMISTER) na huwayanapandisha na kushusha GPA so jamani struggle is very important tu hata ukiingia na course work ndogo ukikazana possibilty ya kupata A au B+ inakuepo,Lengo letu ni kutaka kuondokana na hii SEPTEMBER CONFERENCE,Kwni inaumiza ,wenzio wako nyumbani alafu wewe unakuja chuo ku sapua so bored sana, kitu kingne tuwecare na vitu vyetu mfano simu, laptop,tablets na vitu vingne vya kusomea kwanikipindi hiki wizi na uvamizi ni mwingi sana pia unavoenda kusoma mf yombo kule ni vizuri atleast muwe wengi kiusalama zaidi.

WISHiING YOU NICE PREPARATION UD.

Hapo sio kweli, nimekuwa katika hicho chuo kwa miaka minne na sijawahi kukumbwa na hayo uanyoyadai. Nahudhuria mihadhara na semina (karibu zote), najisomea kwa muda wa saa moja kila siku hivyo sina haja ya kuwa na wasiwasi. Nadhani na wengine wanaofuata mfumo huu hawana shida, nimefanya mitihani ya kitaifa mara kadhaa maishani mwangu, nadhani ile ina presha kuliko maksi sitini za hiki chuo cha kuzalisha wasomi ma.vi.
 
Hapo sio kweli, nimekuwa katika hicho chuo kwa miaka minne na sijawahi kukumbwa na hayo uanyoyadai. Nahudhuria mihadhara na semina (karibu zote), najisomea kwa muda wa saa moja kila siku hivyo sina haja ya kuwa na wasiwasi. Nadhani na wengine wanaofuata mfumo huu hawana shida, nimefanya mitihani ya kitaifa mara kadhaa maishani mwangu, nadhani ile ina presha kuliko maksi sitini za hiki chuo cha kuzalisha wasomi ma.vi.

kwahiyo mkuu umemaanisha naww pia ni msomi mavi........ i think umavi wa msomi ni yeye mwnyw na sio chuo
 
vijana bishaneni nani anasoma chuo kizuri au cha kata mkimaliza mje kwenye usahili tuwape kazi....

Anaeshangilia jina la chuo nadhani ni mpuuzi na pengine ni limbukeni. Kuna Idara inaitwa Fiziko Edukesheni endi Spotsi Sayansi (PESS), kuna kozi nilizoma huko semista iliyopita huwezi amini tulifundishwa vipindi viwili hadi mwisho wa semista, mwalimu alipochachiwa akatupa notes za Wikipedia ndio tujiandae na mtihani.

Ndugu zetu wa mikoani hawajawahi kuona vyuo vingi vya elimu ya juu maishani mwao (zaidi ya vile vya ufundi, ualimu ngazi ya cheti, diploma pamoja na madrasa). Sasa anapofika mjini na kukuta bo bo bonge la chuo, kampasi kama kambi ya jeshi miksa maghorofa anachanganyikiwa nakuona haya ndio maisha. Hapo sijazungumzia aina ya wahitimu ambao hata vipaumbele vyao hawavijui, mtu anapewa bum ananunua simu ya laki tatu ambayo anaishia kuingilia fesibuku na wasapu (baba ake mzazi ana simu imefungwa na rababendi) na bado anavimba kuwa yuko chuo bora.

Umaamuma wao unawafanya hata wasipate muda wa kuchunguza vyuo vingine vinafundishaje, wapi ni bora katika kozi gani na kadhalika. Mfano mimi na akili zangu ukiniuliza ni chuo gani cha umma kiko vyema kitaaluma nitakuambia Ardhi, na vigezo ninavyo, kwa upande wa vyuo binafsi ni St. Joseph CoE na vigezo ninavyo pia.

Ushamba mzigo poti...
 
Hapo sio kweli, nimekuwa katika hicho chuo kwa miaka minne na sijawahi kukumbwa na hayo uanyoyadai. Nahudhuria mihadhara na semina (karibu zote), najisomea kwa muda wa saa moja kila siku hivyo sina haja ya kuwa na wasiwasi. Nadhani na wengine wanaofuata mfumo huu hawana shida, nimefanya mitihani ya kitaifa mara kadhaa maishani mwangu, nadhani ile ina presha kuliko maksi sitini za hiki chuo cha kuzalisha wasomi ma.vi.

Acha upuuzi,,wewe ndo mavi.
 
Naona wasomi mnachambuana vilivyo, sisi huku kwetu hata neno "chuo" ni msamiati mgumu sana kijiji kizima. Ukiuliza msomi ni nani utaambulia kutajiwa vijana "tuliohitimu" kidato cha nne ktk shule za upili zilizoanza kujengwa kwa amri ya mzee Ngoyayi.

Wasomi wetu tangu wapate astashahada na shahada zao hawajawahi kujikomboa kutokana na utumwa wa kisiasa uliotamalaki nchini petu.

Wasomi wetu pia pamoja na tafiti zao sijawahi kusikia wameweza kutatua tatizo la umasikini, ajira na huduma za jamii kama maji, umeme na afya.

Heri yao wasomi, sina mengi ila najiuliza ni kwa nini wasomi warumbanie majina ya vyuo badala ya kupanga mipango ya kuleta maendeleo ktk familia, jamii na hata taifa kwa ujumla?
 
Back
Top Bottom