'Kama mshahara wa mwezi huu utakuwa ule ule ambao hauna nyongeza ya mshahara,tunagoma. Hebu angalia,wenzetu wote wameshapata mishahara yao tena yenye nyongeza tangu Mwezi wa saba kwanini sisi bado? Hadi leo tarehe 3/10/2012 hatujapata mishahara. Tunafanyaje kazi? Nadhani tunataniana hapa.Safari hii tunagoma kweli kweli. Ngoja uone'
Ni maneno ya ukali na ya kutia huruma ya Profesa mmojawapo wa UDSM ambaye alinipigia simu leo 'kuniazima' hela ili auanze mwezi huu. Nimemuonea huruma yeye,Wahadhiri wengine na wafanyakazi wa UDSM kwa ujumla. Mkuu wa Kaya yuko nje anakula maisha. Kwanini lakini mambo haya?