Udom wezi?

kadidu

Member
Apr 2, 2012
39
10
Jamani mimi ni former masters student wa hiki chuo,nimemaliza mwaka jana.chuo hiki kimekuwa na tabia chafu ya kuwatangazia wanafunzi wanaotaka kushiriki sherehe za mahafali kuchangia kiasi fulani cha fedha ili kupata joho la mahafali kwa ahadi ya kurudisha kiasi fulani cha fedha ikiwa mwanafunzi husika atarejesha joho likiwa halina hitilafu yeyote baada ya mahafali

lakini majizi haya yamekuwa hayafanyi hivyo siku mwanafunzi anaporudisha joho na badala yake bila haya yanamwambia mwanafunzi eti aandike akaunti namba yake na wao watamrejeshea kupitia akaunti yake lakini hawafanyi hivyo

kwa mfano mwaka jana sisi wanafunzi wa masters tulilipia 50,000/= na tukaambiwa tutarudishiwa 20,000/= lakini leo ikiwa ni karibu mwaka mzima hawajafanya hivyo.nina ushahidi wangu na wenzangu watano(05) mpaka leo hatujapewa pesa zetu.vivyo hivyo kwa wenzetu wanne(04) waliomaliza mwaka juzi 2011. Tumefuatilia mara kadhaa wanasema watarudisha lakini wapi.wote hatudaiwi hata shilingi na chuo na vyeti tumeshachukua kwahiyo wasije wakaja na hoja hapa kwamba wale ambao hawajarudishiwa eti wanadaiwa na chuo

sasa huu ndio mwisho wao nataka nipeleke swala hili kamati ya bunge ya mashirika ya umma ili ufisadi huu ufike bungeni na kwa baadhi ya wabunge majembe bila kujali chama ili uhuni huu ukome!maana ukienda kiserikali serikali hakuna kitu kwani nasikia yule prof. Mfupi km ki-mba la asubuhi ana kiburi eti sababu analindwa na wakubwa.

Naomba na wengine wahanga wa hili wajitokeze kuunga mkono jambo hili na km kuna mtu anabisha ajitokeze na ushahidi pasipo shaka kwamba amerudishiwa pesa yake

mwisho natoa tahadhali kwa wale wataoshiriki mahafali ya mwaka huu kuwa wajue kile kilichosemwa ni refundable ni kiini macho na msikubali eti mrudishiwe kupitia akaunti bali wawape cash km vipi wakichomoa nanyi msepe na joho.na mwaka huu wametangaza ni 55,000/= na watarejesha 20,000/= km kawaida yao.mohamed-bursar tupe jibu ya dai hili kabla hamjaumbuka kwani mwisho wenu umefika
 
Nina mashaka na master yako labda ni ya magazeti ya udaku, mimi si mwepesi wa kusema na kuchangia mada ambazo hazina msingi lakini kwa hili unadhalilisha master yako na nina mashaka kama unaweza kulea hata familia, SWALA HILI NI LA MSINGI HATA KAMA UNADAI SH. 5 LAKINI ANGALIA MAHALI UNAPOLILETA UNAJAZA JUKWAA TU, EBU FIKIRIA KAMA MTU MZIMA ALAFU UJE NA MAWAZO CHANYA P'SE JITAMBUE NATEGEMEA BAADA YA MIAKA MICHACHE UTAKUWA NA PHD LAKINI KAMA NI HIVI BORA UKA....... ...
 
mimi nina graduate mwezi wa 11 tar 23. Lakini ufisadi wao huo ndo utanifanya niwaze kwende ku graduate au lah.
 
Kaka mimi ckuelewi yani unadai elfu 20?

kuna mtu alikujaga jamvini akasema aliwalalamikia kampuni moja ya mtandao as walimkata 0.3 cent. Sio kwamba anashida na hiyo hela no, anataka kudhibiti michezo hiyo michafu kwa manufaa ya wengine
 
kuna mtu alikujaga jamvini akasema aliwalalamikia kampuni moja ya mtandao as walimkata 0.3 cent. Sio kwamba anashida na hiyo hela no, anataka kudhibiti michezo hiyo michafu kwa manufaa ya wengine
Ndugu kwa hii tanzania tanzania hawatakuelewa mpaka lianzishwe tifu
 
Kaka mimi ckuelewi yani unadai elfu 20?
...anaonyesha tatizo,ishu sio elfu 20. Mfano yupo mfanyakazi wa benki moja alikuwa anadebit shilingi moja kwenye akaunti zoote za wateja. Wenye akaunti hawakuona ni ishu lakini jamaa alikuwa na hela mbaya...
 
Back
Top Bottom