UDOM washindwa kuwahoji rais na makamu wa rais wa serikali ya wanafunzi chss kwa kuhofia kutumbuliwa

kilaza mjanja

JF-Expert Member
Jun 2, 2016
654
1,143
Katika hali ya kushangaza na kustahajabisha ni kuwa uongozi wa chuo kikuu dodoma ofisi ya mashauri wa wanafunzi iliopo chini ya Dick Manongi imeshindwa kabisa kuwaita kuwahoji wanafunzi na viongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha sanaa lugha na sayansi ya jamii ndugu Victor A Byemelwa na Rose Maruchu kutokana na woga wa kutumbuliwa majipu kutokana na ubadhilifu uliofanywa na ofisi ya mshauri wa wanafunzi UDOM.

Taharifa hiyo inaenda mbali zaidi kwa kudokezwa na mmoja wa wafanyakazi wa Utawala mkuu chuo kikuu dodoma alie taka kutojulikana kwa jina lake kuwa kinacho wafanya kushindwa kuwaita vijana hao ni kutokana kuwa hawana sababu zozote zile zilizo wafanya kuwasimamisha chuo wanafunzi hao na hivyo kuona kitendo cha kuwaita na kuwahoji wanafunzi hao kutapelekea kuvumbuliwa mambo mengi yaliyo jificha katika ofisi ya mshauri wa wanafunzi kutokana na ubadhilifu huo wa fedha za serikali za wanafunzi.

Ikumbukwe kwamba wanafunzi hao (Victor & Rose) wote wamefukuzwa chuo kwa kile kinachodhaniwa kuwa wao ni wafuasi wa CHADEMA na kuwa wamewekwa pale kwa lengo la kukibeba chama na kuikosoa management ya UDOM.

Mpaka sasa sakata hili lipo mezani kwa waziri wa elimu na pia lilisoma na msemaji wa kambi rasmi ya upinzani (elimu) wakati wa uwasilishwaji wa hotuba ya bajeti mbadala, swala hilo waziri aliulizwa na yeye kama waziri alikihoji chuo kikuu dodoma na hakikuwa na majibu yanayo ridhisha.

Chanzo hicho kinaenda mbali kikisema kuwa hata chuoni hapo ni viongozi wachache walio hafiki kitendo cha kusimamishwa chuo kwa vijana hao kwa kuwa sababu walizo wapa hazina mashiko yoyote zaidi ya kubambikiziwa kesi hizo ili kuwezesha kutekeleza ufisadi huo mkubwa na fedha za serikali za wanafunzi.

Pia katika hali isio tarajiwa Makamu wa rais wa serikali ya wanafuzni UDOM Rose maruchu yeye alifungua kesi mahakamani kupinga uonevu huo na maamuzi ya mahakama kuu Dodoma ilimpatia ushindi wa kishindo makamu huyo wa rais ambae ushindi wake huo uliwashtua viongozi wa chuo na kumfukuza chuo na pia zipo taharifa kuwa mkuu wa mkoa pia anahusika katika sakata la kupinga amri halali ya mahakama ilio mpa ushindi mwana dada huyo.

Mpaka tunavyo zungumza hivi leo wanafunzi hawa Rose & Victor wameendelea kuchunguzwa na kufatiliwa mpaka simu zao za mikononi na kuangaliwa nyendo zao huku pia mpaka sasa walisha kamatwa na kuwekwa ndani kwa masaa kutokana na sababu zisizo na mashiko yoyote,, mgogoro huu umetoka kuwa wa chuo sasa umebeba sura mpya ya kisiasa na baadhi ya viongozi wa chuo wanatumia mgongo huo wa vyama kutekeleza uonevu wao kwa jamii ya wasomi wa vyuoni.

kwa kumalizia pamoja na changamoto wanazo zipitia vijana hao mpaka sasa vijana hao wamefanikiwa kuendelea na shuguli zao za kibunifu na kibiashara na mpaka sasa ndugu Victor A Byemelwa amerejea majuzi tu kutoka marekani alipo kuwa kwenye mikutano ya kimataifa ya kibiashara na ujasiriamali huku pia dada yetu rose maruchu kwa upande wake pia akiwa anaendelea na harakati za maisha na siasa nje ya chuo kwa mafanikio makubwa sana.

OMBI LANGU KWA VIONGOZI WA SERIKALI HII TIZAMENI VIZURI CHUO KIKUU DODOMA NA MFUMO WAKE KAMA KIPO KWAAJILI YA UTOAJI WA ELIMU AMA KIPO KWAAJILI YA KUFURAHISHA VYAMA VYA SIASA,, NIMATUMAINI YANGU KUWA VIONGOZI MBALI MBALI WA SERIKALI WANAPATA FURSA KUPITIA HUMU TAFADHARI WAULIZIE JAMBO LA VIJANA HAWA NA HATMA YAO YA KIMASOMO KWANGU NIMEISHIA HAPA ILA NAKALA HII TAYARI IMEMFIKIA WAZIRI MKUU
 
ubarikiwe kwa kupoteza muda wako kwaajili ya kukusanya taarifa na kuzileta jukwaani
 
Ndo nini sasa.. Si mngejadili huko huko Udom.. Na ww umeongeza comments
 
wadau wote mnakaribishwa kujadili uozo wa UDOM na watawala wake

Kilaza mjanja umeileta Hii mada huku Ila haujauleta UDINI Ila umeleta USIASA.
Hivi unataka kutujulisha UDOM Ni ya CCM tu?
Unaelezea Kuwa wanafunzi walio fukuzwa Rose Na Victor wananyanyaswa Kwa sababu Ni waChadema.
Huo Ni uchonganishi ambao unafanya wachangiaji wasihoji mabaya ya Udom Ila wahoji vyama vyao vya siasa.
Tafadhali sana wacha UBAGUZI wa UDINI Na SIASA ya vyama ili mada yako isikilizwe.
Hivi unataka kutujulisha hakuna wana Chadema waIIslam Au wanaCCM wa Kiristo?
Nakama Hivi ndio fikra yako Basi
Ushindwe Na ulegee Na ukauke.
 
Back
Top Bottom