Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,502
- 51,098
MY TAKE:
1. Profesa, amesema upo utaratibu ambao wanafunzi husali Mabwenini na madarasani, Japo utaratibu huu ni mzuri lakini ni Convenient zaidi kwa Wanafunzi wa Kikristo kuliko waislamu ambao husali swala tano na pia hujumuika na Staff wengine katika kusali, Je inawezekana vipi Staff na Wanafunzi wakajumuika pamoja mabwenini au madarasani kusali?
2. Siyo convenient kuempty darasa five time a day kupisha Waislamu kufanya ibada zao, Je Chuo kitawaacommodate vipi zaidi ya kuwaruhusu Waislamu kuwa na chumba/nyumba yao ya Ibada ambayo Inawatosheleza kufanya Congregation ya Sala zao tano na Ile ya Ijumaa ambayo wanakuwa wengi sana?
3. Profesa nimeona kwenye hii video huku ukijifanya kuvungavunga kwa maneno umeonekana kustaajabishwa kwa uwepo wa hali ya watu wenye imani ya Kiislamu kwamba walikuwa wamekalia nafasi nyeti kama vile Manager wa Estate, HR n.k, Lakini hebu tusemezane Profesa, Laiti hao watu wote wangekuwa wa imani ya Kikristo ungeona hiyo ni ishu kweli?.
Hivi Profesa unaweza kwa ushahidi kabisakabisa pasipo na chembe ya shaka kuthibitisha kuwa hao watu waliwekwa hapo kwa sababu ya dini yao?
Hivi Profesa tukija katika taasisi zote za umma, tukaanalyse haki bin haki kabisa ni taasisi ngapi ambazo vyeo vimekaliwa na watu wa mrengo wa dini moja?, Je umewahi kuumizwa roho au kuumwa na kichwa kwamba nyingi zinakaliwa na Wakiristo? Sasa ikitokea taasisi moja walioshika hivyo vyeo wengi ni Waislamu kwako inakupa shida?. Au mathalan tukiangalia teuzi za mara kwa mara za taasisi za uteuzi hivi ni watu wa mrengo wa dini ipi wanapata hizo teuzi?, au labda mentality hiyo ya kwako ndiyo msingi mzima wa hizi teuzi zilizolalia watu wa dini moja?
5. Profesa , Ukiwahamisha hao watumishi katika nafasi zao za awali lazima nafasi hizo zitajazwa na watu wengine, na kwa kuwa umeshaonyesha kushangazwa kuwa waliozikalia hizo nafasi huko awali ni Waislamu basi itabidi zijazwe na watu wa dini nyingine most likely kwa nature ya demography ya nchi yetu hao watakaowekwa hapo watakuwa ni Wakiristo maana tayari umeshaonyesha kuwa ni ajabu waislamu kukalia hizo nafasi, Hebu Jiulize Umewahamisha Waislamu unawareplace na Wakiristo, Je kwako hii itakuwa ni sawasawa?, kwamba mahali hapo walipo waislamu wakikalia hizo nafasi ni udini lakini zikikaliwa na Wakiristo haina shida, hivi huoni reverse discrimnation hapo?. Au Profesa unataka tubalance dini za watumishi makazini, lakini Profesa hebu tusaidie tangu lini nchi hii ikapanga post za kazi za watumishi kwa kubalance dini zao makazini?
5. Profesa na wenzako mliofanya huu Uamuzi MUOGOPENI MUNGU ANAWAONA HADI NDANI YA MIOYO YENU
KILICHOPELEKEA MJADALA HUU soma > Uonevu dhidi ya Waislam UDOM: Msikiti wavunjwa, wafanyakazi wanataaluma 11 wahamishwa