UDINI, Zimwi jipya kwa WaTz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDINI, Zimwi jipya kwa WaTz

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by che wa Tz, Jan 18, 2012.

 1. che wa Tz

  che wa Tz JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Habari za leo na mwaka mpya Ndugu zangu wa jf, natumaini wote ni wazima wa Afya na mnaendelea na ujenzi wa Taifa lenu lililopoteza dira yake. Awali ya yote kabla sijaenda kwenye mada iliyonifanya nipoteze muda wangu kuandika hapa ili anayesikia na asikie, anayejifunza ajifunze na asiyehitaji hayo yote na Amani ya Bwana iwe juu yake, basi naomba nafasi ya kuwapa pole Ndugu wote wa Jf kwa kuondokewa na mpambanaji mwenzetu Regia Mtema (R.I.P dada).

  Ndugu zangu wa jf a.k.a great thinkers Family, kabla ya yote naomba kueleza hisia zangu binafsi na kisha kwenda kwenye mada, Ndugu zangu, ktk kitu kinachonikera na kunitia kichefuchefu hapa duniani ni suala la kubaguana, kuchochea na kufanya maamuzi katika misingi ya UDINI haswa kwa sisi WaAfrika. Ndugu zangu, sio siri kuwa suala la imani haswa ya hizi dini mbili kubwa (ukristo na uislamu) kwa WaAfrika na WaTz kwa ujumla ni imani za kimapokeo toka katika jamii za watu waliokuwa na misingi ya utamaduni na mfumo tofauti wa maisha ya WaAfrika. Dini ni mfumo wa maisha, na kila mtu anahaki ya kuchagua mfumo wake wa maisha anayoyataka. Ndugu zangu, katika sifa mojawapo kubwa inayompambanua muAfrika na haswa mTz ni tabia yake ya kuishi na kushirikiana kwa pamoja na watu wote bila ya kujali tofauti zao za udini, rangi wala kabila.
  Ndugu zangu WaTz, sifa hii haikuja hivi hivi, bali ilijengwa na kulindwa kwa nguvu zote tangu enzi za babu zetu na ndio maana leo hii Pamoja na Tanzania kuwa na makabila mengi na dini tofauti tofauti lkn watu wake ni mara chache wamepata kushuhudia ugomvi unaohusisha ama hisia za ukabila au UDINI. Mwalimu nyerere alifanya kazi kubwa sana ktk kutafuta umoja wa WaTz na ndio maana baada ya uhuru aliamua kufanya shule zote zilizokuwa na mtazamo wa UDINI ndani yake na zinazoendeshwa na taasisi za dini, zirudi na kumilikiwa na umma ili kuondoa mgawanyiko katika jamii. Ndugu wana jf, mwalimu aliyafanya haya kutokana na ukweli kuwa, wakati ule jamii ya imani moja ilikuwa ipo nyuma sana katika elimu na hili haswa ilitokana na nature ya ukoloni uliokuwepo ambao haukuzingatia haki za imani za watu haswa wa jamii za WaAFRIKA. Mwalimu alijua na kuona adhari za mgawanyo huu mapema na hvyo kuamua kupambana nayo. Great thinkers, najua mnajua adhari za kuwa na mgawanyiko ktk jamii unaohusisha imani au kabila la mtu (refer Rwanda genocide of 1994 btn tutsi and hutu, Arabs and Nubi's of sudan) na sasa Boko Haram, Nigeria.

  Ndugu wana jf, baada ya kueleza hayo yote hapo juu, naomba sasa kurudi katika kile kilichonifanya kuandika ujumbe huu hapa leo. Ndugu zangu, wahenga walinena "dalili za mvua, ni mawingu, na mchelea mwana kulia, atalia yeye". Ndugu zangu siku zote suala linalohusu imani ya dini ya mtu sio la kuchukulia kimasihala hata kidogo, na haswa mtu huyo anapolalamika juu ya uonevu wowote juu ya imani yake haswa katika jamii iliyo na mchanganyiko wa imani tofauti. Ndugu zangu, siku zote hekima ni Pamoja na kusikiliza na kuheshimu hisia za mtu mwingine hata kama anaonekana ni mwendawazimu. Ndugu zangu, katika kitu kinachonitisha sasa hivi ni ongezeko la kasi la hisia za UDINI kwa WaTz, na mbaya zaidi ni huku nyumbani JF. Ndugu zangu, leo hii si ajabu kukuta humu jf, GT anacomment kwa hisia za UDINI na hata kutukana imani ya mtu mwingine bila hofu yoyote na wala bila kutazama mustakabali wa Taifa lake, jamii yake na familia yake pale kile anachokichukulia kirahisi rahisi leo, kitapokuja kuwa ni disaster. Ndugu zangu, kusoma hatujui, hata picha hatuoni!...............kuwepo kwa Boko Haram ni matokeo ya upuuzwaji kama huu na kutoheshimu imani za dini za watu wengine, au GT mnataka Tz ifike huku? tuache kufikiri na kueleza mambo kirahisi rahisi tu...............Ndugu zangu, sisi ni WaAfrika, na tutaendelea kuwa WaAfrika hadi mwisho wa hii dunia, hizi dini za mapokeo zisituondoe uafrika wetu na kutufanya tuache kufanya mambo yetu kiafrika...............teh teh teh teh teh, eti leo vijana wa kiafrika hawaoani na kujenga familia kisa uarabuni na uyahudi hawafanyi hivyo kutokana na tofauti za tamaduni zao!!

  Gt, nina mengi sana ya kuongea juu ya suala la kuheshimu imani ya kila mmoja wetu na kuzingatia malalamiko ya kila mmoja wetu pasipo kupuuzia, tuache kukashifiana Ndugu zangu, na tena ukiwa katika familia hii, tujenge tabia ya kuongea na kuelezana mambo kwa misingi ya kujenga zaidi, na kwa bahati nzuri, Ndugu zangu, kwa WaTz wengi ktk familia na koo zetu nyingi tunamchanganyiko wa watu wa imani tofauti, sasa je? tukianza kubaguana kwa misingi hii ya UDINI, je tutafika kweli!

  Ndugu zangu nawakilisha hoja, msiniulize mimi ni dini gani coz "my religion is very simple, my religion is kindness". Natanguliza kuomba msamaha kwa yoyote nitakae mkwaza. Kama una la kuongeza, uwanja ni wako
   
 2. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Kuondoa mzizi wa fitina, shule ya Ndanda irudishwe kwa walioijenga!
   
 3. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  "Religion is the opium of the people". Dini inaweza kukufanya ukaunyenyekea na kuupigania ujinga wako, inakufumba macho, unakuwa kipofu wa ukweli. Usipokuwa makini dini inaweza kukugombanisha na ndugu. Usipokuwa makini unaweza kudhani kuwa Mungu alikuumba kwa umakini kuliko wengine. Ukiona dini inakugombanisha, inakufanya usiuone ukweli basi ni kweli kuwa dini ni bangi kwako. Tugombane kwa mengine lakini sio dini.
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  i'll be back!
   
 5. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani hii ndio suluhisho la kudumu
   
 6. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hana maana ya mafundi, bali waliokuwa wamiliki ambao bado wapo hapohapo kiendesha huduma ya hospitari inayotibu bila upendeleo, kiwanda cha uchapaji, na huduma nyingine nyingi zinazotolewa kwa watu wote bila kujali dini ya mtu.
   
 7. che wa Tz

  che wa Tz JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Thank U, nafikiri hicho ndio WaTz tunapaswa kufanya
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mwanzilishi wake Jk
   
Loading...