UDINI NDIYO Uliotufikisha hapa

UDINI NDIYO Uliotufikisha hapa

Status
Not open for further replies.

lonesome

Senior Member
Joined
Oct 10, 2010
Posts
195
Reaction score
66
Ikiwa kila kiongozi tutamwangalia tukiwa tumevaa miwani ya dini hatutaendelea hata siku moja. Na bahati mabaya zaidi hata dini zenyewe hatuzifahamu kwa kiwango kizuri ukilinganishana na hao wanaozifahamu, kwa kutumia ujinga wetu katika mambo ya dini wanatutumia kama daraja kutimiza matakwa yao. Pengine ni kwa kugubikwa na wingu au giza la dini ambalo mara nying hutuzuia tusione mbele. Ni wazi kiongozi wa dini anapohubiri huwa haulizwi maswali, huwa hatuwezi kuhoji. Sasa kwa wengine ambao hawapati muda mzuri wa kupitia maandiko na kuyatafakari husubiri kutafuniwa na kuwekewa mdomoni kila kitu kwa ajili ya utekelezaji.
Kama tumefikia hatua tunampima Rais, kwanza kwa kutanguliza dini yake. Basi si ajabu baadaye pengine tutasogea kuangalia dhehebu. Bado miaka itasonga mbele tukiwa hapa tulipo wakati wenzetu wanatuacha. Huwezi amini kuna watu wanapinga kila alilolifanya Mwal J.K Nyerere kwa sababu ya dini yake. Kuna watu wanapinga kila alilofanya A.H.Mwinyi kwa sababu ya dini yake. Hali kadhalika B.W.Mkapa na J.M.Kikwete kwa sabau ya dini yake. Kuna watu watawatetea watu hao pia kwa minajiri ya dini zao na kusema huyu ni wakwetu. Huu ni zaidi ya ujinga. Ikifikia hatua kuwa tukashindwa kumjadili mtu kwa upande wa mabaya kwa kuwa ni dini yetu au tukashindwa kuyaeleza mabaya ya mtu kwa kuwa wengine watasema ni sababu ya dini yake huu ni zaidi ya ujinga.
Hili nimeliona sana kwenye hoja mbalimbali watu wakimkingia kifua Rais kwa sababu ya dini yake na wengine wakimkosoa kwa sababu ya dini yake. Bahati mbaya zaidi wengi ya hao mnaowahukumu kwa sababu ya dini hata dini zenyewe unakuta hawazifaham vizuri. Kama anashiriki katika ushirikina, kama anaiba pesa yeye na familia yake, kama anasababisha watu wafe/wateseke , kama haoni matatizo ya wananchi anajiangalia yeye na familia yake pamoja na kundi lake. Huyu ana dini kweli? Si mnafiki tu? Pengine tunaangalia majina ya Kikristo na Kiislamu. Pengine tukiana watu hawa wanaenda nyumba za ibada tunadhani ni wa dini zetu. Mi nisingekuwa na tatizo kama Rais anakuwa Sheikh na akatenda mambo kwa haki bila kupendelea dini yoyote. Nasi tukaona kuna maendeleo. Hali kadhalika nisingekuwa na shida kama atakuwa Rais Mchungaji au Padre naye akatenda mema kwa wananchi wote pasipo kujali dini zao.
Tusishindwe kumhukumu matendo ya mtu kwa sababu ya dini yake lakini pia tusimhukumu mtu kwa kuangalia kigezo cha dini yake. Hili tumeliona na tutaendelea kuliona kama tusipojisahihisha. Wanasiasa wengi ni opportunist ( wanatumia nafasi wanazoziona mbele yao) wao ni rahisi kutugawa kwa misingi hiyo ikiwa kama itawasaidia kimaslahi. Kama kiongozi wa siasa atakwambia mchague yeye maana ni wa dini yenu siku nyingine hachelewe kusema achaguliwe yeye kwa kuwa ni wa dhehebu flani. Maana kama atatokea mwanasiasa mwingine ambaye ni wa dini moja unadhani atazungumzia kigezo gani kingine kama si dhehebu? Lakini pia kama ni dhehebu moja usishangae akahamia hata kwenye kanda,mkoa, kabila…ukoo, n.k
Tanzania ni nchi maskini kwa nini? Tuna mito,maziwa,bahari,ardhi,madini,wanyama,watu n.k lakini bado maskini. Je tunajiuliza katika hilo au tunabishania dini za watu flani? Tufikie hatua tusiangalie dini ya mtu. Tumhukumu mtu kwa matendo yake sisi dini yake haituhusu. Kama hafai tuseme hafai na kama anafaa tukubali kuwa anafaa pasipo kuangalia dini yake. Kesho na keshokutwa tutakuja gundua madhara ya kutumia dini kama kigezo yeye akiwa ameshaondoka, na familia yake ni tajiri sisi tunabaki kusema ni mwenzetu. Mwenzetu wa wapi? Anaishi mikocheni, mbezi ,oysterbay na masaki kwa pesa alizopata kutokana na jasho letu? Wewe unaishi haya maeneo yetu tunapambana na vibaka kila kona. Lakini bado pasipo hata haya unasema huyu ni mwenzetu. Watanzania kama tusipogeuka na kuacha uovu huu hukumu inayotujia ni mbaya na hatutaweza kuimudu. Udini huu ndo umetufukisha hapa. Maana hatuwezi kukemea wala kusifia kwa sababu ya dini za kiongozi husika. Tusimkuhumu mtu kwa kumwangalia jina lake linaendena na dini gani. Maana sasa imefikia hatua hata mtu anaposema jambo tunalitafakari kwanza kidini. Tunatanguliza dini kwanza halafu ndo tunakuja kujadili hoja kwa mwelekeo uendanao na dini husika. Ole wetu maana tunajivika gunia tulilochovya kwenye mafuta ya taa halafu tunaenda kuota moto. Ole wetu. Na hili kwa viongozi wengine wao angalau watakuwa na faida chache kwa muda mfupi. Mana moto utakapowaka wao au familia zao hawatakuwa salama kwa asilimia 100.
Tugeuke sasa na kuanza kuwaza kimtazamo wa kitanzania. Hii nchi ni yetu jamani hawa watu wengine watakuja watapita baada ya miaka mitano au kumi. Sasa jiangalie wewe umesiamama wapi katka kipindi hicho? Ukiwa na busara zaidi utawaangalia na ndugu zako na jirani zako. Usidhani wewe una amani unapoishi katikati ya majirani maskini wote wakikutizama wewe tofauti na wao. Hautakuwa salama hata kidogo,ikiwa wanajua kabisa kuwa mafanikio yako ni kutokana na jasho lao. Tukemee kwa nguvu zote suala la udini na tulipinge kwa nguvu zote aiwepo kiongozi wa kutuingiza huko kwa sabau ya kufilisika kwake kisiasa. Huyo tumkatae na kumwogopa zaidi ya ukoma
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom